Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Bi Tozo atakuja kutetea hizo nauli kama alivyoitetea Tanesco na ujambazi wao wa kuunganishiwa umeme... yaani nalipa kila kitu halafu bado sio mali yangu. Na bado nakuwa mteja nisiye na mamlaka na bidhaa zangu. Kaujinga amaizing
 
Wapanga bei wana mabasi yao. Je wakiweka bei ndogo ya treni nani atapanda basi?
 
Naisubiria na Bwawa la Nyerere likamilike niyakumbuke maneno ya wanasiasa yalivyo matamu kama asali ila matendo machungu kama shubiri. Wakati wanaanzisha hizo harakati ilisemekana SGR ikikamilika bei yake itakuwa nafuu sana hata kushinda nauli za mabasi, Hilo limetoka tusubirie umeme kwa sababu huo tuambiwa unit moja haitozidi 150tsh tofauti na Sasa inauzwa karibia 380tsh ili tuweze kuzalisha bidhaa viwandani kwa gharama nafuu. Tulitolewa mpk na mfano baadhi ya nchi km marekani wao unit moja mpk inamfikia mlaji hifiki hata 100 ya kitanzania ndio maana wanazalisha bidhaa kwa gharama nafuu
 

Hadi mwenyewe wameni surprise.
 
Au wanafanya kama kampuni ya apple walivyo tufanyia??wanataja kua simu zetu tutaziuza millioni 3,mtapaniki mtasonya mtapaza sauti kua gharama kubwa,but siku ya uzinduzi wanatangaza wanawapenda na wamepokea maoni yenu,wanauza million 1...hapo mind games inachezwa MTU anaenda kupunguza nauli ili aombe Kura...na bado haitakua reasonable price..
 
sasa utashangaa yanavyojaza, rejea mwendokasi,
Tatizo la tanzania tunatukuza Umasikini mno.

Binafsi naona bei iko sawa, kuna watu wanakereka na muda mrefu kutumika barabarani yaani km 450 masaa 7-9
Wakati kwa treni unaweza kutumia masaa 4
Na pia ni adventure

Kikifanyika kitu utasikia sisi wanyonge itakuwaje
 
Mkuu ili wazo ni nzuri, tatizo mfumo wa maisha yetu waafrika hasa viongozi siyo wa kutatua changamoto+ kama hiyo bali wao wataongeza matatizo.
 
Mbona ndogo sana hio nauli. Ishu sio nauli ishu na mda. Kukaa masaa manne kwenye basi na kukaa Saa moja kwenye treni kipi bora
 
Hizo bei ziko juu sana kwa Mwananchi wa hali ya chini.
Hata sh 500 ya daladala ni nyingi Sana kwa mwananchi wa kawaida.
Kusafiri ni mipango kwani wanatakuwa KILA siku unasifiri
 
Huwezi kapande bus, huwezi kanyaga Moro sio mbali siku nne tu umefika kwa mguu.
 
Iwapo CHADEMA tutapewa ridhaa ya kuongoza Nchi hii tutashusha nauli za Treni ya SGR.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…