Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Ni sawa tu. Maana tofauti kati ya treni ya Umeme na ndege ni mwendokasi na njia inayotumika. Maana wanaotakiwa kupanda hizo treni ni wale wenye haja ama sababu ya kwenda kwa kasi kuliko mabasi, Kama huna haraka hakuna sababu za kupanda treni hizo.
Tatizo watu wanataka walazimishe kila kitu kiwe bei ya kila mtu
 
Basi tuhamie Kenya
 
Treni ya Umeme haina kawaida ya kuvuta wagons nyingi
 
Kama 500 tu inawashinda watu nauli na wapo mjini, kihehere cha nini kukaa dar kufanya Kazi Moro kama ujimudu kiuchumi.
Afu hii treni haijatengenezwa ili ibebe watu milioni 61
Watanzania tunapenda jiendekeza ndo maana hatupati vitu vizuri kwani kila mtu anaogopa leta.
Mtu anakubali kaa masaa 9 road ili alipe 30,000 wakati akiongeza 40 anaenda Dodoma kwa haraka,
 
Ndio maana hata vilio vyetu kuhusu ugumu wa maisha hawavijali. Nauli waliyopanga tu ni ushahidi hawajali shida zetu!
 
Na dar-moro unatumia muda gani!??

Wangeweka na hiyo ndo wadau tungejua tunachangia vipi, ili kupimanisha kati ya nauli tajwa na muda maana kuhusu huduma ukiwa ndani hatujui.
 
Badala ya huduma kuanza kabla ya Xmas wao wataanza January '23! Muda huo watu watakuwa hoi! Watu gani watapanda treni kuzurura? Halafu time table vipi? Sio nilipie nauli Tsh 70k Dar - Moro kwa masaa 3 badala ya Tsh 15-20k ya basi muda huo huo!
 
Hiyo ni bei ya nauli walizopendekeza wao trc then latra watakusanya maoni ya wadau ili wacrosscheck pande zote kupata bei sahihi ya mlaji. Kama mlaji napendekeza nauli ya dar moro iwe 6000
Swali ni kwamba hayo mapendekezo waliyafikia vipi? Siamini kama ni bahati mbaya.
 
Myopic thinking hivi unajua sio ajabu kwa mtu kukaa morogoro na kufanya kazi Dar ? , Usafiri ukiwa rafiki hii inaweza ikawa safari ya mtu kila siku kwenda na kurudi
Ni kazi zipi hizo mkuu ambazo wafanyakazi wake wanaweza kuishi moro wakati kazi zinafanyika dar?
 
Badala ya huduma kuanza kabla ya Xmas wao wataanza January '23! Muda huo watu watakuwa hoi! Watu gani watapanda treni kuzurura? Halafu time table vipi? Sio nilipie nauli Tsh 70k Dar - Moro kwa masaa 3 badala ya Tsh 15-20k ya basi muda huo huo!
Dar - Moro haitapungua masaa mawili! Tatizo hii nchi maswala ya kitaalamu huwa yanazungumzwa na wanasiasa wasiojua kitu..
 
Ni kazi zipi hizo mkuu ambazo wafanyakazi wake wanaweza kuishi moro wakati kazi zinafanyika dar?
Ni kitu gani ambacho ni hindrance ya mtu kukaa point A na kufanya Kazi point B..., Kama kuna usafiri unadhani kuna shida gani ya mtu kukaa popote pale na hii inapunguza population density kubwa sehemu moja
 
Aisee! Basi sawa mkuu wangu..
 
Si nyienyie mnalilia bullet trains? Watu ni wajinga sana humu ndani wanataka mabehewa ya bullet train ila kulipa tshs 24000 kwenda Morogoro ni mgogoro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…