Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

Gharama za uendeshaji ziko juu sanaa.....mafuta yamepanda sana spare ndio usiguse....nauli ilitakiwa ipande mwaka sasa....mafuta yamepanda mwaka sasa

Kwa hivyo mwananchi ndio anabebeshwa mzigo wa gharama Hadi za spare?. Acheni fix
 
Unaufahamu utaratibu uliopo kisheria unaohusu ushirikishwaji wa wadau wa usafiri? Ni wazi utaratibu huo ulifuatwa na hivyo hakuna namna inabidi tukubaliane na hizo nauli mpya.

Utaratibu upi ulifuatwa?. Wao walikaa na watoa huduma basi. Mwananchi gani akubali nauli kupanda?.
 
Bi domo kaupiga mwingi kila secta! Tumwongezee mitano!

Hapana hii minne inamtosha. Akipewa mitano Nauli ya Dar Moro itapanda mpaka elfu thelathini. Tumpe mtu urais atakaye Kuja kutatua gharama za maisha.
 
Niwe mkweli mama Samia akichukua fomu 2025, atakuwa anachukua kwaajili ya kwake binafsi na sio wananchi. Yani miaka miwili na ushe nauli imepanda ile mbaya na ghara za maisha juu. Mama angepisha tupate mtu wakija na idea mpya za kiuchumi na sio uchawa Kama Sasa
 
Na wenye nyumba wanapandisha efu 15.patamu hapo
 
Mtu ambae hakushiriki kulinunua basi, kununua spare parts, kununua mafuta nk. unataka ashirikishwe kupanga nauli? Serious?

Kwani hayo ni mabasi ya umma?
 
Huyo Maza hatufai kwakweli, ni mbinafsi na mtu wa kupenda kiki
Alafu hata wala hastuki yy anaona poa tu. Mama mimi nikiwa kama mshauri nakuomba useme neno. Huku chini hali ni mbaya usijitenge sana na wananchi wa chini wapiganie. Usiwe na hofu na uchaguzi ccm wanashindaga miaka yote. Hata msipofanya kampeni bado mtashinda.
 
Tushirikishwe sie kama nani, sisi ni VIZALALA tu nchi hii, wenye nchi wameamua, mtu asiyetaka twende burundi.

Huu ujinga watz ndio tunautaka.. Kadri siku zinavyokwenda hali inakuwa tete.
Ni kama vile unavyotaniana na mtoto, akakushika ndevu, atakupiga kibao unamchekea, atakuti kidole cha jicho unamchekea, ipo siku atakushika kalio mbele za wageni.
[emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom