Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

Tuanategemea pia bajeti ijayo bia zitapanda bei na utasikia walevi wakilalamikaa [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].

Hv walevi Huwa kwann hamlalamiki ..[emoji28][emoji28]
 
Kinachoniuma ni yule Mzee wa LATRA alivyosema eti WATANZANIA walishirikishwa ktk kupanga hizi nauli..

Muongo sana yule Mzee
 
Nchi Ya Acha Liende Tu, Mtanikumbuka Siyo Kwa Mabaya Ila Mazuri
 
Ipo siku itafika nauli elfu 2 ya daladala kutoka bunju makumbusho. Bado nko ktk harakat za kuhamia nchi za watu kamili.
 
"Serikali sikivu", walaaniwe wote mpaka chawa,kunguni, mende na viroboto wa chama chao.
 
Gharama za uendeshaji ziko juu sanaa.....mafuta yamepanda sana spare ndio usiguse....nauli ilitakiwa ipande mwaka sasa....mafuta yamepanda mwaka sasa
Gharama za uendeshaji zipo ,akina abood kila siku wanatoa vyuma tu.
Ingekuwa hakuba faida wangelaza magari yao
 
Unaufahamu utaratibu uliopo kisheria unaohusu ushirikishwaji wa wadau wa usafiri? Ni wazi utaratibu huo ulifuatwa na hivyo hakuna namna inabidi tukubaliane na hizo nauli mpya.
Kwamba ww raia huna haki ya kutoa maoni ? Kisa mafuta yamepanda ndo itoshe kusema bei zipande ? Je hakuna namna ya kudhibiti upandaj wa bei wa mafuta au kudhibiti sababu nyingine chochez kupanda kwa nauli

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Kwamba ww raia huna haki ya kutoa maoni ? Kisa mafuta yamepanda ndo itoshe kusema bei zipande ? Je hakuna namna ya kudhibiti upandaj wa bei wa mafuta au kudhibiti sababu nyingine chochez kupanda kwa nauli

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Mimi ninachojua kwenye suala la kupanda nauli taasisi inayosimamia usafiri wa mabasi (LATRA) uwa haipangi nauli kiholela tu pasipo kufuata utaratibu uliopo kisheria. Utaratibu huo utakuwa unahitaji upokeaji wa maombi ya kupandisha nauli kutoka kwa watoa huduma (wenye mabasi) wakiwa wametoa sababu za kuomba kupandisha nauli na pia LATRA kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuitisha mkutano na watoa huduma, LATRA consumers consultative council ambalo usimamia haki za wapewa huduma (wasafiri),

vyombo vingine vinavyosimamia mambo ya barabarani kama polisi wa Usalama barabarani, mwananchi yeyote anaependa kuhudhuria na kutoa maoni au kusikiliza tu kinachojadiliwa kwenye mkutano n.k. Baada ya kupokea maoni kwenye mkutano huo mapendekezo upelekwa ngazi ya juu zaidi ili kupata baraka zake na kisha nauli kutangazwa rasmi. Hata kama nauli siyo rafiki bado naamini LATRA watakuwa wametumia huo utaratibu na kama umetumika tafsiri yake ni kwamba wananchi wameshirikishwa.
 
Back
Top Bottom