Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

KIZIMKAZI hana muda na Watanganyika. Majizi yanajipangia nauli tu. YY anasubilia majanga ndio atulie ndani y nchi. Kama majanga hakuna anasepa majuu huku anawachia wajipigie.
Bongo kikubwa Uhai 2
 
Sipingi kupanda sababu ni kweli baada ya muda lazima kutakuwa na mabadiliko ya bei, ila navyoona kiwango kimekuwa kikubwa sana kwa ghafla, ingeongezeka kidogo ni gnumu hata kuyaona machungu
Last time nauli imepanda mafuta both diesel na petrol yalikuwa yanauzwaje kwa litre? Kiukweli gjaram zimepanda sana, mtu mpaka unaanza kuhisi gari imeharibika kumbe ni bei ya wese
 
USAFIRISHAJI: Leo Desemba 8, 2023 Watumiaji wa huduma za Usafiri za Mabasi ya Masafa Marefu (Mabasi ya Mikoni) na Mafupi (Daladala) wanakutana na gharama mpya za Nauli.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), nauli za Mabasi yote zimepanda baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Watoa Huduma na Wadau wa Usafiri (Wananchi).
In short huyu maza 2025 hatufai kwa kweli may b akaiyongoze KIZIMKAZI....
 
Nauli ni rafiki sana hasa ukizingatia tumepandishiwa mshahara, hakuna mtanzania aneishi kwa chini ya milioni moja kwa mwezi, hakika serikali ya mama inaupiga mwingi tuwape maua yao. Chaajabu Bei ya Mafuta imeshukaa.
Jaribu tuu Kuwa mkweli. N muhimu sana. Jobless na wamemaliza vyuo tena vya maana zaid yako na wana ufaulu wa zaidi yako wanaonekana kama wasaliti kwenye famlia zao. Hoyo millioni unayosema naamini kwa commwnt hyo hata wewe hujawai itumia au ipata kwa mwezi. Ni vile tyuu kuna target ya kuonekana sehem flan unapopajua unailenga. Nachoamini n kuwa Maisha yet n magumu kwahyo tuvumiliane kwa hali tuliyonayo kwenye transition period
 
Hiiii serikali inaongea vitu vya uongo sana hili kaa na mwananchi gan yeyote akakubali nauli ipande kama sio wao wenyewe ndio wanapandisha nauli kisa wanamiliki mabasi
Hii ni serikali ya kipuuzi sana ambayo haijawahi kutokea kwenye hii i nchi
Kwan ata mafuta ya kishuka nauli azishuki wako na ujinga sana mafuta yameshuka juzi kwa nn leo nauli zimepanda
 
Jaribu tuu Kuwait mkweli. N muhimu
Umeongezewa ww na sio wote wanafanya kazi serikalini kumbuka kuna watu weng wamemaliza chuo awana kwa hiyo maisha unayo ishi ww sio wote tunaishi na ww ungekua auna kazi usinge Sema mama ako anakupiga mwingi
 
Nauli ni rafiki sana hasa ukizingatia tumepandishiwa mshahara, hakuna mtanzania aneishi kwa chini ya milioni moja kwa mwezi, hakika serikali ya mama inaupiga mwingi tuwape maua yao. Chaajabu Bei ya Mafuta imeshukaa.
Yaan ww unaongea utaila kabisa yaan hiyo milioni moja unawapa ww kichwa kama drum ya HOWO ww
 
Watanzania ni wa kupelekwa pelekwa tu, wanaamua wanavyotaka na hamna cha kuwafanya.
 
Wadau gani wa usafiri walishirikishwa? Mbona sikuona mikutano ya adhara kwenye vituo vya mabasi ili kupata maoni ya wadau halisi wa usafiri?!

Mnaowaita wadau ni wanaoendesha V8 wanajua nini kuhusu adha ya usafiri?!
 
NILITOKA NA PIK NYUMBAN KUFIKA KITUON 1000..NKAPANDA 700 MBEZI
NKAENDA BUCHA 600 NKAPANDA BK TO.MBEZI 600

NKAENDA STAKISHARI 800..K
X2
NIKARUDI NYUMBAN GAFLA NAITWA BOKO MAGENGEN HUKU NIKAKOMA
900 NAULI JAMAN TUTAFIKA TU
 
Tunaiomba mamlaka husika kulitizama hili kwani vigezo vilivyotumika havifahamiki ukizingatia mafuta yameshuka bei kwa shs 200/-

MAMLAKA HUSIKA USAIDIENI UMMA HUU WA WANYONGE,SHUSHENI NAULI NA ONGEZENI SHS 50/- KWA NAULI ZA MIJINI, INAUMIZA MNO.
#Based on town trips!
Na sio nauli / safari za mikoani.
 

Attachments

  • FB_IMG_1702322298463.jpg
    FB_IMG_1702322298463.jpg
    56.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom