Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Kukosoa ni kazi nyepesi sana. Nyerere alirithi nchi mbovu zaidi. Barabara ya kwanza ya lami ilijengwa mwaka 1956 na marehemu Kikenya, tumetoka mbali.

Haina tija yoyote kumsimanga marehemu asiyeweza kujitetea, alifanya kazi ngumu katika kuujenga msingi wa kitaifa.
Mkoloni alijenga lami hadi chalinze,acha uwongo jombaa,na nyerere mwenyewe kwenye lami ndiyo bure kabisa,hakuna cha maana alichofanya,kikwete pekee alijenga lami zaidi ya awamu tatu za kabla yake kwa ujumla
 
Hujui lolote mkuu, lami ya kwanza alijenga marehemu James Kikenya mwaka 1956 niliyasikia haya kutoka kwake mwenyewe aliishi hapa mbezi beach,

Nyerere apewe heshima yake aliongoza Tanganyika iliyojaa wajinga wengii hivyo asingeweza kwa mara moja tu akaleta mabadiliko yote tunayoyaona leo hii. Kuongoza nchi ni tofauti na hizi soga zetu humu jukwaani.
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukari, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni nchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Ndio, sera zake za kiuchumi zilifeli vibaya mno
 
watu wengi wanamuona Nyerere kama nabii ,kwamba alipaswa kuanzisha na kumaliza yeye kila kitu .
wanasahau kuwa Nyerere ni mwanadamu japo na kwa zama zake alifanya makubwa sana

Kipindi tunapata uhuru, vitu vya msingi vilikuwa ni
1.Disunity
2.Ujinga
3.Ukabila
4.Decentralized Settlements
5.Udini
yote haya yakifanikiwa ndo huduma za kijamii zingefanikia kutolewa kwa watu wengi ndani ya muda mfupi

Nyerere alipokea nchi ikiwa bado ipo jehanam , asingeweza maliza kil kitu yeye binafsi

Alianzisha nia ila waliofuata wakabadili njia na ndo matokeo ya haya tunayaona sasa
1.Ufisadi
2.Utekaji
3.Mikopo ya hovyo
4.Mikataba ya hovyo
Kwenye Udini alichemka
 
Unaijua hadithi ya mwinyi ya kuoga bafuni na mwendawazimu kupitia nguo zako?..ulisikia alichokisema kwenye hotuba yake inayofichwa ya mikuki mitatu?..hapo alikua 'anamkoga' tu
Unanieleza mambo ya kipumbavu unategemea mimi nitayajuwa vipi!
Sipotezi muda na hadithi za huko vijiweni kama ulivyo wewe. Ngazi yangu ni tofauti kabisa na hiyo yako.

Unatoa mfano wa Mwinyi, huyo ndiye kiongozi aliye kukoga wewe? Basi anzisha mada juu yake.
 
Mimi na wewe nani ambae hana akili? Nimetaja mambo ambayo yalikuwepo katika uongozi wake lakini wewe reply yako imejaa dhihaka na vijembe mwanzo mwisho, nilitegemea wewe mwenye akili upinge nilichoandika kwa mifano anuai. Katika uongozi wa teacher nchi haikutumbukia kwenye umasiki?, watu hawakukimbia nchini kwenda kuishi uamishoni?
Bado huelewi unacho ambiwa. Wewe ulitaka Tanzania iwe dunia gani ya kipekee sana ambayo matatizo yaliyo ikumba dunia nzima yaliyumbisha kila sehemu?
Kwa sababu akili yako haina upeo wa kuangalia mbali zaidi ya pua yako, hayo unayo yazungumzia hapa hujui kwamba kulikuwa na matatizo mengi duniani wakati huo. Badala ya kupanua akili yako, unaishia kulaumu kwa msukumo wa unaoujuwa mwenyewe. Hapo unataka usaidiwe vipi, kama si kukuacha uendelee na ujinga/upumbavu wako!
 
Tatizo la njaa lilisababishwa na nini? Kama lilitokea kwa majirani zetu jr ni halali kutokea kwetu?. Uko Kenya sehemu kubwa ya ardhi yao haikubalinkilimo kama hapa kwetu, kwa wao kukumbana na tatizo la huaba wa chakula ni kawaida.

Reply zako unashambulia mtu binafsi badala ya kushambulia hoja.
Nashambulia mtu binafsi kwa sababu mtu huyo ni mjinga. Kwa mtu wa aina hiyo unatakaje?
Wewe kama umezaliwa miaka yote hiyo, lakini muda wote huo hukuweza hata kujitambua, unataka watu wakuchukulie vipi?
 
Bado huelewi unacho ambiwa. Wewe ulitaka Tanzania iwe dunia gani ya kipekee sana ambayo matatizo yaliyo ikumba dunia nzima yaliyumbisha kila sehemu?
Kwa sababu akili yako haina upeo wa kuangalia mbali zaidi ya pua yako, hayo unayo yazungumzia hapa hujui kwamba kulikuwa na matatizo mengi duniani wakati huo. Badala ya kupanua akili yako, unaishia kulaumu kwa msukumo wa unaoujuwa mwenyewe. Hapo unataka usaidiwe vipi, kama si kukuacha uendelee na ujinga/upumbavu wako!
Sasa si ndo ifafanue hayo matatizo sasa, hivi we jamaa una akili kweli.
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukari, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni nchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Kwa mentality za most humu na hasa chakadomozzzz

Kila kiongozi hapa bongo ni failure

Za kuambiwa?
 
Unanieleza mambo ya kipumbavu unategemea mimi nitayajuwa vipi!
Sipotezi muda na hadithi za huko vijiweni kama ulivyo wewe. Ngazi yangu ni tofauti kabisa na hiyo yako.

Unatoa mfano wa Mwinyi, huyo ndiye kiongozi aliye kukoga wewe? Basi anzisha mada juu yake.
Mungu wako alipozidi kumfuatafuata,akatoa simulizi ya mwendawazimu kupitia nguo zako,akatukumbusha kuwa alitutoa foleni za unga,mtu uliwatia tabu za maisha uliowatawala lakini huchoki kubwekea uongozi ulioondoa tabu ulizowatwika watu,kana kwamba ulifanya la maana
 
Hujui lolote mkuu, lami ya kwanza alijenga marehemu James Kikenya mwaka 1956 niliyasikia haya kutoka kwake mwenyewe aliishi hapa mbezi beach,

Nyerere apewe heshima yake aliongoza Tanganyika iliyojaa wajinga wengii hivyo asingeweza kwa mara moja tu akaleta mabadiliko yote tunayoyaona leo hii. Kuongoza nchi ni tofauti na hizi soga zetu humu jukwaani.
Unamsikiliza mtu kumbukumbu zake zimeliwa na mchwa,una uhakika gani hasumbuliwi na dimentia!?..rais' wa nchi kikwete alirudia mara kadhaa kuwa lami aliyoacha mkoloni ni dar-chalinze
 
Kuna msemo unasema 'huwezi kutumia akili iliyosababisha tatizo kutatua tatizo'..haishangazi kuona kwamba hakuona tatizo kwenye ujamaa wake,ujamaa kwake ulikua dini,alichukia sana mtu kuwa tajiri
Nyerere alikua kiongozi mzuri, na tunampenda ila sera yake ya ujamaa haikuweza, isingeweza kutoa matunda kwa jamii hizi za kitanzania.

It was a day dream, na alifeli pakubwa.

Ange adopt na ujamaa mapema tangu uhuru, hata kenya tungekua tunakimbizana kiuchumi.
 
Kenya ina uchumi wa kuufanya kuwa benchmark yetu?.. acheni akili za kutukuza vya nje
 
Nyerere last time alikuwa Raisi wa Tanzania almost 40 years ago, leo bado mnafikiri shida zenu ni Nyerere, at least shukuru hakutuachia vita kama haya matekaji ya siku hizi yanapotupeleka, na Kwa msio jua Nyerere alikuwa ahead of his time, yeye ndio alipigania nchi iwe na vyama vingi huku CCM aliyoianzishia walikuwa wanatutisha vyama vingi vitaleta vita, Nyerere nakubali sera zake za uchumi zilituletea umaskini lakini alionekana kubadilika mwishoni, alikuwa mtu wa haki na hakuwahi na Tamaa, alikufa maskini kabisa, na ingekuwa anaishi Nina uhakika asingekubaliana na siasa za CCM za wizi wa kura, kubambikia kesi, utekaji au kuuza maliasiri za nchi. He was a good man
Wewe mbinguni utaenda kwa kusema ukweli.

Na huu ndo ukweli wazee wa miaka 70, hawataki kuskia. Kwenye sera za uchumi nyerere alifeli, Huko kwingine kote Alikua vizuri lkn kwenye uchumi ni 0.

Sasaivi, tuko na sera angalau ila hatuzitekelezi kama tunavo zi strategize mwisho wa siku results/Impacts inakua below targets.

Nyerere sera iko kushoto, utekelezaji uko juu, matokeo zero 🤣.
 
Back
Top Bottom