Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Hapo zilikua zimeshapita week mbili mkuu nikimpigia hapokei sms hajibu nilimtumia break up text nione kama ata make effort kuokoa mahusiano ndo nikarealize kama alidhamiria tuachane
Asilimia kubwa ya sisi wanaume hatuwi tested. Kitendo cha kuthubutu kuandika tuachane wanaume wengi hatuwezi jisumbua wala kujigusa inakuwa imeisha.

Pia kukaa kimya kwa muda fulani ni njia ya kuacha mambo yapite salama kama kulikuwa na tofauti. Na hii tunafanya kwa wanawake wanaongea sana kwa lugha mbovu na hawataki kujishusha.

Kuna hili lingine nikisema litakuumiza ukiona bado harespond kubali yaishe
 
Pole sana, hakuna mwanaume ambaye anampenda mwanamke akafanya kitendo cha kikatili kama hicho, lakini pia nahisi kutakuwa na red flag ambazo ulishindwa kuziona hapo awali. Naomba nikuulize maswali machache, Nini kilikuwa kinatokea baada ya sex, i mean alikuwa anakuthamini na kukucare baada ya tendo like cuddle, hug, kiss, talk to you. !!? Mwanaume asiyekupenda most of time he will detach from you, wengine wata escape na kujifanya wapo bize na simu, kukimbilia kuoga au kulala. Haimaanishi kama you have bad taste but hii hutofautisha kati ya love and sex.
 
Principle apo ni kwamba,staycalm dont disturbe the man and dont quit,until 3 months,wewe mcheki tu hata kama hajibu kwq miezi mitatu .
 
Pole sana Mjukuu

Imani yangu kwamba, Kila jambo hutokea Kwa sababu.

Huenda huyo mpenzi wako, angekusumbua mbele ya safari

Hivyo Mungu ameamua kukuepusha na mengi

Wito wangu kwako, ni kuendelea kuwa imara ukizidisha maombi. Yupo Mume sahihi ambaye Mungu amekuandalia.

Kama nafasi inapatikana, uje Kijijini utusalimie Mimi na Bibi yako.

Kuna Kijana hapa jirani wa Mzee Mkwizi hajaoa, unaweza ukaja tukawakutanisha mkawa marafiki 😜
 
Be positive. Hakuna kinachofanyika bila sababu,
Shukuru Mungu sana maana safari ya mapenzi ina ngazi ambazo Kila unapopanda maumivu hungezeka iwapo itatokea kuachana.Namaanisha umeumia lakini sio kama aliyeachwa baada ya ndoa ya miaka 25 yenye familia kubwa. Yupo atakayekupenda kweli lakini pia chunga usinmuumize mtu.
 
Njoo inbox tuyajenge.

Namimi ni mhanga.

Mke niliyetaka kumuona kaingia mitini
 
Aibu nishaipata sababu mahusiano yetu yalikua open Sana
Wala uisone aibu. Watu wanafunga ndoa wanaachana sembuse boyfriend. Achana na tabia ya kuwekeza moyo wako kwa mtu. Jijali mwenyewe. Atayekupenda arakuja tu. Ndoa kama ipo ipo tu. By the way, ndoa zenyewe za siku hizi ni majanga matupu. Tuliza moyo wako na jipe furaha mwenyewe kwanza. Usitegemee kupata furaha kwa watu utaishia kuumizwa tu.
 
Kuanza mapenzi mapema ni changamoto. Kuivunja hiyo Roho yake ndan yako ni SHIDA utakuja msumbua mumeo. Tafuta uso wa Mungu acha zinaa
 
Au ndo yule mwenye maTatooo
 
Ahsante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…