Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Hapo zilikua zimeshapita week mbili mkuu nikimpigia hapokei sms hajibu nilimtumia break up text nione kama ata make effort kuokoa mahusiano ndo nikarealize kama alidhamiria tuachane
Asilimia kubwa ya sisi wanaume hatuwi tested. Kitendo cha kuthubutu kuandika tuachane wanaume wengi hatuwezi jisumbua wala kujigusa inakuwa imeisha.

Pia kukaa kimya kwa muda fulani ni njia ya kuacha mambo yapite salama kama kulikuwa na tofauti. Na hii tunafanya kwa wanawake wanaongea sana kwa lugha mbovu na hawataki kujishusha.

Kuna hili lingine nikisema litakuumiza ukiona bado harespond kubali yaishe
 
Pole sana, hakuna mwanaume ambaye anampenda mwanamke akafanya kitendo cha kikatili kama hicho, lakini pia nahisi kutakuwa na red flag ambazo ulishindwa kuziona hapo awali. Naomba nikuulize maswali machache, Nini kilikuwa kinatokea baada ya sex, i mean alikuwa anakuthamini na kukucare baada ya tendo like cuddle, hug, kiss, talk to you. !!? Mwanaume asiyekupenda most of time he will detach from you, wengine wata escape na kujifanya wapo bize na simu, kukimbilia kuoga au kulala. Haimaanishi kama you have bad taste but hii hutofautisha kati ya love and sex.
 
Principle apo ni kwamba,staycalm dont disturbe the man and dont quit,until 3 months,wewe mcheki tu hata kama hajibu kwq miezi mitatu .
 
Pole sana Mjukuu

Imani yangu kwamba, Kila jambo hutokea Kwa sababu.

Huenda huyo mpenzi wako, angekusumbua mbele ya safari

Hivyo Mungu ameamua kukuepusha na mengi

Wito wangu kwako, ni kuendelea kuwa imara ukizidisha maombi. Yupo Mume sahihi ambaye Mungu amekuandalia.

Kama nafasi inapatikana, uje Kijijini utusalimie Mimi na Bibi yako.

Kuna Kijana hapa jirani wa Mzee Mkwizi hajaoa, unaweza ukaja tukawakutanisha mkawa marafiki 😜
 
Be positive. Hakuna kinachofanyika bila sababu,
Shukuru Mungu sana maana safari ya mapenzi ina ngazi ambazo Kila unapopanda maumivu hungezeka iwapo itatokea kuachana.Namaanisha umeumia lakini sio kama aliyeachwa baada ya ndoa ya miaka 25 yenye familia kubwa. Yupo atakayekupenda kweli lakini pia chunga usinmuumize mtu.
 
Hello wakuu,

Nimeona nishare sababu niko katika hali mbaya. Mawazo mabaya ya kujidhuru yananijia kichwani. Sijawahi kupenda kama nilivyompenda yeye. Kila kitu kilikuwa vizuri, ghafla akakata mawasiliano. Wiki 3 sasa nikimpigia hapokei, sms hajibu.

Nimehangaika, nikaongea na dada na kaka yake lakini bado alinikalia kimya. Mara ya mwisho kuwasiliana naye tulizungumza vizuri tu. Mipango yetu ilikuwa tufunge ndoa na alipanga mwezi huu aje nyumbani kujitambulisha. Lakini ghafla kimya chake kikatokea.

Baada ya kimya kirefu, siku 5 zilizopita nikamtumia sms ya kuachana lakini hakunijibu kitu. Naumia sana. Sijawahi kumkosea chochote ila ameamua kunifanyia ukatili huu. Naumia na najiuliza maswali ambayo sipati majibu.
Njoo inbox tuyajenge.

Namimi ni mhanga.

Mke niliyetaka kumuona kaingia mitini
 
Aibu nishaipata sababu mahusiano yetu yalikua open Sana
Wala uisone aibu. Watu wanafunga ndoa wanaachana sembuse boyfriend. Achana na tabia ya kuwekeza moyo wako kwa mtu. Jijali mwenyewe. Atayekupenda arakuja tu. Ndoa kama ipo ipo tu. By the way, ndoa zenyewe za siku hizi ni majanga matupu. Tuliza moyo wako na jipe furaha mwenyewe kwanza. Usitegemee kupata furaha kwa watu utaishia kuumizwa tu.
 
Kuanza mapenzi mapema ni changamoto. Kuivunja hiyo Roho yake ndan yako ni SHIDA utakuja msumbua mumeo. Tafuta uso wa Mungu acha zinaa
 
Hello wakuu,

Nimeona nishare sababu niko katika hali mbaya. Mawazo mabaya ya kujidhuru yananijia kichwani. Sijawahi kupenda kama nilivyompenda yeye. Kila kitu kilikuwa vizuri, ghafla akakata mawasiliano. Wiki 3 sasa nikimpigia hapokei, sms hajibu.

Nimehangaika, nikaongea na dada na kaka yake lakini bado alinikalia kimya. Mara ya mwisho kuwasiliana naye tulizungumza vizuri tu. Mipango yetu ilikuwa tufunge ndoa na alipanga mwezi huu aje nyumbani kujitambulisha. Lakini ghafla kimya chake kikatokea.

Baada ya kimya kirefu, siku 5 zilizopita nikamtumia sms ya kuachana lakini hakunijibu kitu. Naumia sana. Sijawahi kumkosea chochote ila ameamua kunifanyia ukatili huu. Naumia na najiuliza maswali ambayo sipati majibu.
Au ndo yule mwenye maTatooo
 
Letting go is the best way to go!!.

1-Tafuta namna utakayoweza kukusaidia usimuone machoni mwako, iwe laivuu au mitandao ya kijamiii Kisha jijali nafasi yako na Maisha yako ya uchumi kwakua siku hizi mwanadam anataka kwanza ajue una nn ili apime kiwango Cha Heshima anachoweza kuendelea kukupa.

2-Kama una Moyo wa kuugulia ndan Kwa ndan bila MTU kujua, Usifute namba yake Wala usimblok,kwenye mitandao ya kijamii, ILA HAKIKISHA UNAPOST PICHA UKIWA NA FURAHAA SANAAA na nyingine ukiwa Sehem ambazo hakuwahi kukupeleka ... Watu wanaotupitisha kwenye maumivu Huwa wanawakawaida ya kutamani kutuona tunawalilia ,watuone tunatoka machozi ,watuone tumeharibikiwa, kwao wao hiyo ndo Furaha yako Kuu, Sasa ukifanikiwa kumpa matokeo Kinyume ya kile ambacho walikitegemea Huwa wanaumia sanaaa , na usishangae akaanza kujirudisha.

3-Mapenzi Kwa wanadamu hayatakiwi kua Kipaumbele Chao Cha Maisha Kwa sababu watu wanabadilika , hivo hupaswi kumtumainia mwanadamu na kumpa matarajio makubwa asiyostahili.

4/ Kama mmekua kwenye Uhusiano muda mrefu na mwezi Huu ndio alipanga kujitambulisha, basi huyo Hana mpango wa kukuoa , anasubiri mwezi wa kujitambulisha upite Kisha atarudi....Hana utayari wowote kwako.

5/Inawezekana ni Moja ya wanaume ambao Huwa wanaamua kutoa mitego ya kupima MTU , Huenda anataka kuona Ukomo wa uvumilivu wako


Sasa ufanye nini??.

Chagua Kati ya namba Moja au Mbili, lipi uende nalo.

Kivyovyote vile akijirudisha iwe aliamua kukupima au kaona we ndio sahihi, au Kwa namna yoyote Ile, SHARITI LAKO WEWE KURUDIAMA NAYE IWE NI NDOA, YAAN AJITAMBULISHE, NA MCHAKATO WA NDOA UANZE MARA MOJA BILA KUMPA MZIGO , YAAN KWA MAUMIVU ALOKUPITISHA , MPE MZIGO KWENYE NDOA TU.

Usikubali tena kua Mjinga.
Ahsante mkuu
 
Back
Top Bottom