Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Serikali yetu ibaki kwenye kutoa huduma zipi? elimu? afya? maji? umeme? kote huko bado kuna matatizo miaka 60 baada ya kupata uhuru.

Narudia tena, serikali yetu nayo ibinafsishwe kwanza, kabla hatujafikiria kubinafsisha hizo taasisi nyingine.
wewe ndio inatakiwa ubinafsishwe maana huwezi hata kujiendesha mwenyewe
 
Serikali yetu ibaki kwenye kutoa huduma zipi? elimu? afya? maji? umeme? kote huko bado kuna matatizo miaka 60 baada ya kupata uhuru.

Narudia tena, serikali yetu nayo ibinafsishwe kwanza, kabla hatujafikiria kubinafsisha hizo taasisi nyingine.
Uko sawa.
 
Marekani inadaiwa na china sana tu. Kukopa ni moja ya maendeleo chanya. Ungesema ungejua. Shida ya nyie elimu ndo tatizo

Unajua kitu kinaitwa Modigliani theories? Unajua input and output models and how they work?
Kwa hiyo unalinganisha uchumi wa Marekani na kwetu? kwamba nao wanakopa hovyo hovyo kila siku kama tufanyavyo sisi?!

Hujui hata kufanya comparison, kigezo cha kwanza hakikisha unaowa- compare wanafanana kwa kiasi kikubwa, kama level ya uchumi, uendeshwaji wa serikali, uwajibikaji.. sio una compare mbingu na ardhi we mchumi wa modigliani theory!.

Pili, hakikisha hayo madesa yako uliyokariri yanaendana na mazingira tuliyomo, jiulize; hiyo theory uliyoandika { + input/output} iko applicable kwa viongozi wetu? au wanatumia kigezo cha hiyo theory kuficha udhaifu wao?

Hiyo modigliani theory yako sijui nini inasaidia nini kuondoa ujinga vichwani mwa viongozi wetu? wanaweza kufanya nini? hata huduma za msingi za binadamu zimewashinda kutoa, hatuna hata matundu ya vyoo mashuleni!, halafu wewe "msomi" unaleta ujuaji wa kukariri madesa yako wa modegliani....
 
Ifike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na ushakuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji.

Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.

Hiyo Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.

Tanesco angali utendaji wao, lazima wafuatwe offisini uwe unajuama na mfanya kazi mmoja wapo, na sio tu kufuatana na kuwapa rushwa juu, sasa ingekuwa inasimamiwa na watu weupe unazani kungekuwa na kufuatana offisini?

Angalia TTCL haijulikani kazi zao kwa sasa, hivi TTCL ilikuwa ni ya kushindwa hadi na wakina Haloteli? TTCL ilipaswa kuwa sawa na Vodacom, ila Kwa sababu ni Mali ya Umma hakuna anaye jali pale na imejaa wafanya kazi wengi kuliko ufanisi na hakuna anajali.

Mamlaka za maji zimejaa upigaji tupu, unafuatilia kuunganishiwa maji hadi unachoka na lazima uhonge la sivyo hutakaa uunganishiwe maji.

Kwani Bandari ikikodishwa hao wanao kodisha watakuja kuondoka nayo? Wataihamisha? Tuachane na ujamaaa
Unafikiri tatizo ni nini?
 
kubinafsisha kupo kwa aina mbili. mojawapo ni kuwapa watu wa ndani na aina nyingine ni kuwapa wawekezaji wa nje. Hapa kweli tunaweza kuwawezesha wawekezaji wetu wa ndani na kuisimamia bandari na mashirika mengine yakaendeshwa kwa tija na kwa faida zaidi kuliko kuiachia serikali wakati kila mwaka mwaka wanazalisha hasara tu. serikali ibaki kwenye majukumu yake ya msingi ambayo ni kutoa huduma za msingi na kudhibiti ubora wa huduma na viwango pamoja na kukusanya kodi katika hizo taasisi.
Kwa Tanzania hii? Tulibinafsisha mshirika mengi mwisho wakaja wajanja wakavuna wakasepa na kuyaacha yakijifia
 
Hio Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.

Hata mimi kwa hili naunga mkono zaid ya 1000000% serikali inashindwa kuwasimamia watu iliyo waajir yenyewe
Na hapo ndo machina alikuwa anapataka bandari ya dar ingekufa natural death
 
Kama hadi Bandari inatushinda kuiendesha, basi hakuna kitu Watanzania tutaweza kukisimamia na kukiendesha kwa Ufanisi.

Hapo Bandari na mashirika mengine ya Umma kilichotakiwa ni kubadiri namna ya kuwapata Wakurugenzi Watendaji yaani CEOs, badala ya kuteuliwa kisiasa basi Wangechujwa kupitia Interviews pamoja na kuruhusu Mtu yeyote mwenye sifa kuomba hata kama atakuwa Sio raia wa Tanzania.

Upatikanaji wao uangalie zaidi Merits.

Hao maCEOs wapewe malengo na Serikali iache Utaalamu ufanye kazi badala ya kuingiza Siasa zao

Umetoa hoja nzuri but hii syteam isiwe kwa viongozi wa juu tuu bali iende mpaka kwa wafanyakazi wa chini kila mtu ajue jukumu lake ni lipi
 
Serikali yetu ibaki kwenye kutoa huduma zipi? elimu? afya? maji? umeme? kote huko bado kuna matatizo miaka 60 baada ya kupata uhuru.

Narudia tena, serikali yetu nayo ibinafsishwe kwanza, kabla hatujafikiria kubinafsisha hizo taasisi nyingine.
Hawa jamaa kula mbengu kwao sio ishu wamelitia umasikini taifa laki bado tu wanata wauze kilatiku.

Siwezi kuwalaumu ccm na serekali zake hapa wajinga ni watanzania wenye nchi yako.
 
Akili za hovyo kabisa hizi, kwa hiyo furaha yako uwape wageni wakuendeshee mambo yako wewe uendelee na story za pwagu na pwaguzi kwenye kijiwe cha kahawa.

Kama mnataka kubinafsisha kwa nini msiwambie watanzania wenyewe waunde makampuni waiendesha, au ndo ule jenerali Ulimwengu aliuita ugenishaji.​
Samia hataki shida kabisa yeye kila kinachomkera anabonafsisha
 
Lengo la kubinafsisha ni kwa ajili ya kuwapa Waarabu au Wachina hakuna jambo jingine hapo.

Watu wenyewe ni akina Mwigulu Nchema,January Makamba na Ridhiwani Kikwete chini ya Bunge bubu la Tulia Acksoni nchi itabaki mifupa tu.
Watu ni kama wamekatwa vichwa, washindwe kuendesha bandari eti wanasubiri mwingine aje awaendeshee wao kazi yao kwenda kukusanya pesa. Labda kama huyo mwekezaji ni mjinga

Anaanza na kuwekeza trilioni 1, hawajui katoa masharti gani. Pengine mmeambiwa msubiri mwaka mzima arudishe kwanza hiyo trillion 1 ndio mkusanye Kodi. Na hapo kwenye Kodi anaweza ku-declare hasara
 
kubinafsisha kupo kwa aina mbili. mojawapo ni kuwapa watu wa ndani na aina nyingine ni kuwapa wawekezaji wa nje. Hapa kweli tunaweza kuwawezesha wawekezaji wetu wa ndani na kuisimamia bandari na mashirika mengine yakaendeshwa kwa tija na kwa faida zaidi kuliko kuiachia serikali wakati kila mwaka mwaka wanazalisha hasara tu. serikali ibaki kwenye majukumu yake ya msingi ambayo ni kutoa huduma za msingi na kudhibiti ubora wa huduma na viwango pamoja na kukusanya kodi katika hizo taasisi.

Nimeona kavideo clip mtandaoni U tube just a blink of an eye. Ka dinner ya yanga jana hapo Afisi Kuu Takatifu. Hizo sura za wahudumu wa misosi na vinywaji ni kastuka kidogo au ubinafsishaji ulianzia hapo kwa huduma za misosi huku bandarini/TPA ni muendelezo tu
 
Naungana na wewe serikali kufanya biashara ni kunufaisha watu wachache tu maana wizi ni asili ya watanzania ziwekwe terms nzuri kimkataba ambazo zitaipa pesa za uhakika serikali wawaachie wawekezaji.hata ufanisi utakuwepo sana na malalamiko yatapungua sana
Sasa si wataiba hizo kiduchu zitakazopatikana kutoka kwenye hayo makampuni?
 
Marekani inadaiwa na china sana tu. Kukopa ni moja ya maendeleo chanya. Ungesema ungejua. Shida ya nyie elimu ndo tatizo

Unajua kitu kinaitwa Modigliani theories? Unajua input and output models and how they work?
Hili si tatizo lako, ni tatizo la teenagers wengi wapo hivi. Akijua kitu huwa anaamini hakuna wengine wanaojua

Leo unaniuliza kuhusu Modigliani-miller? Hunijui lakini unaassume hakuna kitu najua
 
Ndiyo mkuu uko sahihi wezi wanafikiria namna ya kunufaisha familia zao.
Na njia moja kubwa wanayotumia kwenye kujinufaisha hi hii ya MIKATABA. Ukisikia kuna MKATABA umesainiwa, angalia kwa jicho la tatu, utaona nia halisi ya nyuma ya pazia.
 
Ifike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na ushakuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji.

Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.

Hiyo Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.

Tanesco angali utendaji wao, lazima wafuatwe offisini uwe unajuama na mfanya kazi mmoja wapo, na sio tu kufuatana na kuwapa rushwa juu, sasa ingekuwa inasimamiwa na watu weupe unazani kungekuwa na kufuatana offisini?

Angalia TTCL haijulikani kazi zao kwa sasa, hivi TTCL ilikuwa ni ya kushindwa hadi na wakina Haloteli? TTCL ilipaswa kuwa sawa na Vodacom, ila Kwa sababu ni Mali ya Umma hakuna anaye jali pale na imejaa wafanya kazi wengi kuliko ufanisi na hakuna anajali.

Mamlaka za maji zimejaa upigaji tupu, unafuatilia kuunganishiwa maji hadi unachoka na lazima uhonge la sivyo hutakaa uunganishiwe maji.

Kwani Bandari ikikodishwa hao wanao kodisha watakuja kuondoka nayo? Wataihamisha? Tuachane na ujamaaa
Uafrika hasa utanzania ni LAANA.
 
Kuwaachia kila kitu wawekezaji maana yake tunakiri hatuwezi kujitawala, ni bora sasa tumrudishe mkoloni arudi kwasababu naamini kabisa, jinsi mambo yanavyoendelea serikalini kwa sasa, pia tunahitaji kuibinafsisha serikali yetu.

Hivyo sioni sababu kwanini tuendelee kuwaza kubinafsisha vitu vidogo dogo, wakati kule juu penye tatizo la msingi tunaendelea kupaacha kama palivyo, alaah, kumbe inawezekana hata vichwa vyetu pia vinatakiwa kubinafsishwa, kwasababu fikra zetu nazo ni mgando.
Mwafrika hawezi kujiongoza mwenyewe inabidi mkoloni arudi kutu tawala kwa viboko.

Mwafrika akipata nafasi tu ya uongozi anachowaza ni kuji tajirisha yeye kwanza.

Mjerumani inabidi kutawala hii nchi kwa Viboko.

Uafrika hasa Utanzania ni LAANA.
 
Watanzania ni wezi imeshindikana kuwadhibiti kutokana na aina ya viongozi iliyopo na wanalindana sana kwenye wizi wao hivyo serikali haipati pesa zinazo stahiLi kupitia badari bora kuwapa wawekezaji tuu
Wala hawajashindikana. Tatizo lilianza pale mwizi wa kuku anafungwa miaka 10 ila mwizi wa mabiliano kifungo cha miaka Mitano au kulipa faini.
 
Back
Top Bottom