Naungana na netanyau Israel imefikia malengo yake ya vita dhidi ya iran

Hiko kituo kitajengwa tu ndani ya mda mfupi sana huwezi fananisha na mtu ambaye anachukua miaka mingi ili apate uzoefu
Kituo sio jengo tu tunazungumizia technologia ambayo Israel ilipambana nayo tokea miaka hiyo 1930 mpaka Israel kufikia vile ilivyo, hiyo technologia, data na devices/materials zimeenda na maji + wataalamu waliokuwa kwenye hicho kituo
 
Mapro israeli wa mbagala kama machawa wa sisiemu tu, kila kitu akisema mama lazima wakisapoti kwa maandamano ya kuunga mkono asilimia mia

Mahaba ni kitu kibaya sana

Sasa israel ilichoachivu ni nini hapo.
 
Kufumuliwa kwa kambi za kijeshi, majengo muhimu ya kijasusi ya MOSSAD na watu wanaouawa sio raia ni wahusika wa kijeshi ila Israel anaficha ukweli.

Iran sio mjinga kulenga majengo muhimu jua kabisa ni maeneo wanayojificha magaidi ya Kiyahudi.

Israel kukubali kusimamisha vita sio kawaida ujue mwili unawasha kila mahali kwa kichapo.
 
 
Iran inasema nuclear bomb ni lazima na watalitengeneza kwasababu sasa wana knowledge yote hawahitaji usa wala atomic agency kuwasimamia.
Tuwape muda.
 
Unaitazama Irani kama TZ, wenzetu hawategemei mtu 1 kuhodhi kila kitu halafu wengine mbaki kushangilia tu. Kwa wenzetu kule kila aliyekuwepo kwenye taasisi ana deliver na mchango wake unaheshimiwa hata na Boss! Usishangae baada ya muda mfupi ukasikia jamaa wana test bomu la nuclear tofauti na matarajio ya wengi
 
Huko makanisani mnadanganyana ujinga kweli kweli
 
Kituo sio jengo tu tunazungumizia technologia ambayo Israel ilipambana nayo tokea miaka hiyo 1930 mpaka Israel kufikia vile ilivyo, hiyo technologia, data na devices/materials zimeenda na maji + wataalamu waliokuwa kwenye hicho kituo
Ndug yangu ulimwengu wa leo uhifadhi wa data ulivyomkubwa technology haipotei kizembe hivyo……
 
Ushabiki maandazi...
Ulitegemea aseme nn...
Netanyau alisema REGIME change ...halafu useme kafanikiwa ....
NETANYAU roho inamuunga kishenzi kwa kuwa .kwake aliona GOLDEN chance imekuja ...lakini amekutana na miscalculations ...kama ni tishio bado lipo pale pale...
 
Mtaongea yoote ila ni kujifariji tuu mnajua na hata Netanyahu anajua kuwa safari hii kakosea mahesabu na kadondokea pua labda ajipange wakati mwingine kama alivyofanya kule Lebanon kwa Hesbulah
 
Huna jipya na taifa teule😀😅😂hicho kichaka kishatiwa moto sasa na ile kauli mbiu taifa teuli halipigwi naona kwishaaaaa
 
Wayahudi wa namtumbo hadi uyole kazi mnayo ya kuwatetea taifa teule. Kichapo mmechezea haswa
 
Ndug yangu ulimwengu wa leo uhifadhi wa data ulivyomkubwa technology haipotei kizembe hivyo……
Ndio wamepoteza kila kitu sasa waondoe vifusi kurudisha hiyo mifumo ya kitaalamu iliyoasisiwa tangia 1930 na kurudisha wataalamu wao kama wapo tena maana wengine wamemaliwa na kuangukiwa na vifusi
 
Imebaki tu Africa kuimba ISRAEL ni taifa teule...
Kumbe US + Western wanaitumia Israel kimkakati wa kimaslahi pale MIDDLE EAST...
...
Kama kuna community imeharibu cristianiry culture..basi ni US + WESTERN....bahati mbaya Christian wa leo washaamini kwamba huwezi kutenganisha Christian mode of life na Christian calture...
 
Nilichaomini,
Israel kaona kabisa,
Katia mguu, kaona Irani ni maji marefu
 
Israel au USA?
 
Iwe walisema au hawakusema, vita yoyote atakayoamua kuipigana Israel dhidi ya Iran, ushindi pekee kwa Israel regime change, bila regime change basi no matter what, credits zote lazima zipelekwe Iran.
Kule palestina waliombwa ceasefire wakakaza fuvu, Hadi misaada ya kibinadamu waliwanyima.

Kichapo alichotembeza iran ndani ya Israel, hasa kwenye hub za teknolojia, kimewafadhaisha sana, ndomana hawakutaka warekodiwe na media
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…