rip faza_nelly
JF-Expert Member
- Feb 19, 2018
- 5,749
- 7,038
Ujuaji mwingi sana humuNdugu naomba niseme kitu hapa kwanza mleta mada yupo sahihi kabisa na hao bata ni kweli ni bei juu hata mimi nawafuga pia, pili ningaliwaomba tusiwe tunapenda kumjadili na kukashifu vitu bila kuwa na uhakika navyo. Ndugu kama kifaranga wa Bukini anauzwa sh 60,000 elf unafikiria wa kuanzia umri huo atakuwa bei gani? Nawaombeni sana tuheshimu na kujali kila liletwalo na mfugaji mwenzetu ili tuweze kusonga kwa ujumla.
Uko sehemu gani ndugu? maana Mbuzi wapo wa bei tofauti na wa aina tofauti, wanyama au wa maziwa? naomba tu ukubaliane nae bei ya bukini ni kubwa na kuna Mbuzi pia wana bei kubwa pia. Nakuomba usimsemee mwenzetu sivyo.Niliko huku mbuzi wa sh 40,000 Ni yule akipata dume anapandwa na kuzaa, huyu jamaa ana utani Na 1M ,juzi nimeemda mnadani 200K unapata ng'ombe.
Ana utani? Serious? Hivi unajua bei ya Bukini? Au unadhani jamaa ameamua tu kujiuzia hiyo bei? Nenda popote kalete bata bukini sita wa umri huo kwa hiyo bei ya jamaa kama utawapata niletee.Niliko huku mbuzi wa sh 40,000 Ni yule akipata dume anapandwa na kuzaa, huyu jamaa ana utani Na 1M ,juzi nimeemda mnadani 200K unapata ng'ombe.
Ni jambo la kuombana radhi na kuomba ushairi mwisho wote tutaelimika juu ya ufugaji maana uanda wa ufugaji ni mapana sana. mf Mimi nauza bukini 2 jike na dume sh laki3 na nusu. Mbuzi ninae Dume Isiolo nilimnunuwa laki 5 wa mbegu hapo bado usafiri wa kumtoa Arusha mpaka Dar, kwahiyo kikubwa ni kuuliza na kuelimishana tu taratibu.Ujuaji mwingi sana humu
Umesema ukweli Barikiwa sana ndugu.Ana utani? Serious? Hivi unajua bei ya Bukini? Au unadhani jamaa ameamua tu kujiuzia hiyo bei? Nenda popote kalete bata bukini sita wa umri huo kwa hiyo bei ya jamaa kama utawapata niletee.
Mungu akubariki na kukujaalia njia iliyo bora ktk hitaji lako.Habari
Nauza bata bukini 6 kwa bei ya shillingi million moja (1,000,000). Bata wana umri wa miezi 8 na wana chanjo zote. .
Hawa bata nawajali sana nahakikisha wanakula kabichi na spinach kila siku. Nawanunulia chakula top quality ni wenye afya nzuri sana. Nauza wote sita siuzi mmoja mmoja kama unahitaji nicheki 0714829688. .
NIKO MANZESE SWEETCORNER
Ndugu naomba uwavumilie wote hatuwezi kufanana ktk lile tulifanyalo, ufugaji una gharama zake na changamoto zake.Acheni roho za ajabu
Hakuna aliyelazimishwa kununua. Kama hujawahi kufuga chochote acheni kelele
Bata nawanunulia chakula na nawagharamia sana, kwani kuna mfugo unaojifuga wenyewe?
Acheni roho mbaya sio jambo la kiungwana hata kidogo
Tupeni tofauti ya hao bukini na bata wa kawaidaNi jambo la kuombana radhi na kuomba ushairi mwisho wote tutaelimika juu ya ufugaji maana uanda wa ufugaji ni mapana sana. mf Mimi nauza bukini 2 jike na dume sh laki3 na nusu. Mbuzi ninae Dume Isiolo nilimnunuwa laki 5 wa mbegu hapo bado usafiri wa kumtoa Arusha mpaka Dar, kwahiyo kikubwa ni kuuliza na kuelimishana tu taratibu.
Bukini ni bata wa urembo sio kula, halafu ni makubwa kinyama katika aina za bata. Uchache wao unafanya upatikanaji wake kuwa wa gharama zaidi. Mengine watajazia wengine. Inaaminika pia kwamba ukifuga hao mchawi hasogei kwakoTupeni tofauti ya hao bukini na bata wa kawaida
Tupeni tofauti ya hao bukini na bata wa kawaida
Ni bata ambao ufugaji wake ni mrahisi pia hata ukuwaji wake ni mzuri, wanakula zaidi majani mf kabichi,spinach,ukokoka,majani ya migomba. wanapendelea sana kuogelea na niwasafi sana utakapo wa fuga unashauriwa uwawekee mahala wapate kuogelea, ni Bata wa aiana ambayo wana umoja sana kipindi chote hasa wakati wa kulalia na kukuza vifaranga. Na ni walinzi wazuri wa familia na mazingira ya Nyumbani pindi waonapo mgeni hutoa taarifa kwa njia ya sauti ya juu. Nakushauri nunuwa vifaranga wa mwezi mmoja kwenda juu ndio uanze nao itakusadia kuweza kuwatambuwa vyema.Natamani Sana kuwafuga Hawa viumbe ila nachemka kwenye Bei TU...
Kwa urembo kweli wanapendeza kuwaangalia ila ni mboga pia, utagaji wao ndio mtihani na ndio kisababishi kikubwa cha kufanya uongezakaji wao kuwa mchache. Wao huwa hawatagi sana kama Pekini au Mallard au hawa wakawaida.Bukini ni bata wa urembo sio kula, halafu ni makubwa kinyama katika aina za bata. Uchache wao unafanya upatikanaji wake kuwa wa gharama zaidi. Mengine watajazia wengine. Inaaminika pia kwamba ukifuga hao mchawi hasogei kwako
Ahsante mkuuNi bata ambao ufugaji wake ni mrahisi pia hata ukuwaji wake ni mzuri, wanakula zaidi majani mf kabichi,spinach,ukokoka,majani ya migomba. wanapendelea sana kuogelea na niwasafi sana utakapo wa fuga unashauriwa uwawekee mahala wapate kuogelea, ni Bata wa aiana ambayo wana umoja sana kipindi chote hasa wakati wa kulalia na kukuza vifaranga. Na ni walinzi wazuri wa familia na mazingira ya Nyumbani pindi waonapo mgeni hutoa taarifa kwa njia ya sauti ya juu. Nakushauri nunuwa vifaranga wa mwezi mmoja kwenda juu ndio uanze nao itakusadia kuweza kuwatambuwa vyema.
Karibu sana mimi nawafuga ninakauzoefi kidogo kwakweli ila naamini kuna wajuzi zaidi yangu hapa watakuja kutusaidia elimu zaidi, ila ni wazuri na nniwatamu pia kwa mboga. 🤣 🤣Ahsante mkuu
Ndio mkuuIvi si ndo aina hii ya Bata hutumika kwenye ulinzi pia?
Wakubwa.Sikujua Mkuu,