Nawachukia sana hawa matapeli wanaouza dawa mbele ya misikiti

Nawachukia sana hawa matapeli wanaouza dawa mbele ya misikiti

Lakini kwanini uongozi wa misikiti naruhusu hawa wahuni wananing'iniza tunguli mbele ya misikiti? Na unakuta wanauza hadi dawa ya kufukuza majini. Hivi wanafahamu umuhimu wa majini kwa waislamu?
 
Kila baada ya swala ya Ijumaa utawakuta watu mbele ya misikiti wametundika tunguli, vibuyu na dawa wanazozinadi kuwa zinatibu maradhi mbalimbali ya binadamu. Mara nyingi wanaenda kwenye misikiti ya BAKWATA; ni nadra kuwakuta kwenye misikiti ya Sunni.
View attachment 2935829
Nimebaini hawa watu si waganga wala waganguzi bali ni matapeli wa kutupwa. Baadhi ya magonjwa wanayojinadi kutibu ni nguvu za kiume, bawasili, ngiri, mshipa, kukojoa kitandani, figo, kumrudisha mpenzi aliye mbali, nk. Kabla sijaenda mbali, naomba kuweka wazi kuwa mimi ni mhanga mmojawapo niliyewahi kutapeliwa mchana kweupe.

Siku moja nilipita mbele ya msikiti nikakuta watu wamekusanyika huku katikati yao kukiwa na mwanaume wa makamo aliyekuwa anaongea kwa uhodari sana. Nikasogea karibu kuchungulia kulikoni. Nikamsikia yule mwanaume akijinadi kuuza dawa mbalimbali za asili. Baada ya ushawishi wa kutosha nikanunua dawa moja iliyokuwa katika umbo la unga nikaenda kuitumia kwa mujibu wa masharti ya mganga yule. Baada ya kuitumia ile dawa nakuona haileti matokeo chanya, nikaamua kuifanyia uchunguzi wa kina. Lahaula! Kumbe haikuwa dawa bali unga wa muhogo.

Kwa kweli kitendo kile kiliniuma sana. Fikiria nimelipa fedha nyingi kununua dawa initibu maradhi yangu na usiku ule tayari nilishajiandaa kutest mitambo halafu nakuja kudhalilika mbele ya mpenzi wangu. Tangu siku ile niliwachukia sana hawa matapeli wanaofanya utapeli wao mbele ya misikiti.

MAONI YANGU
Inasikitisha sana jinsi watu wanavyotumia udhaifu wa maradhi kuwatapeli raia kwa kuwauzia dawa bandia misikitini. Hapa asilauimiwe shehe, imamu wala mwadhini. Hawa watu wanauza dawa feki kwa tamaa zao wenyewe. Hawatumwi msikiti, shehe au mtu yeyote.

Aidha, wagonjwa wanaonunua dawa hizi wanasukumwa na maradhi yao na kiranga chao wenyewe. Bawasili ilishakomaa unadanganywa kwamba itapakwa dawa iishe? Umerogwa. Nenda hospitali ukfanyiwe upasuaji. Ni muhimu kabla ya kununua dawa ukajiridhishe kama inafanya kazi au la.

Nawasilisha.
Walio kutapeli umewaacha huko unakuja hapa kulalamika tukusaidieje nenda kawaambie huko
 
Walio kutapeli umewaacha huko unakuja hapa kulalamika tukusaidieje nenda kawaambie huko
Mkuu huwa hawakai mahali pamoja. Wanahama kutoka mkoa hadi mkoa na kutoka msikiti hadi msikiti. Ni vigumu kuwapata. Natoa wito kwa serikali inisaidie kuwasaka wahuni hawa.
 
wanapendelea misikiti gani 🤣

hapo kawe mbona pia kuna watu wengi baada ya ibada, iweje wajikite humo tu.
waache ubaguzi wa kidini, kuna wengine wa dini nyingine pia huenda wanahitaji huduma yao baada ya kutoka kwenye ibada zao pia. wapanue hiyo huduma bas 🐒
Hawa wanakuwa wamevaa kanzu kabisa mkuu. Inaonekna ni wafia dini. Hawawezi kuuza dawa kwenye makanisa ya makafir
 
Tumia chai ya tangawiz
Juis ya tende
Tikiti Kwa wingi usisahau mazoezi
Polesana 😃
Asante sana mkuu. Nitafuata ushauri wako kisha nitaleta mrejesho hapa.
 
Wanaziita tiba za kisuni kumbe hamna kitu wanaweza hata kukusagia mavi yao waliyoyakausha
Kweli kabisa. Wanakuwa wameweka pale watu wao wanajichanganya na raia wanajifanya wateja kumbe matapeli wenzao.
 
Back
Top Bottom