Nawachukia sana hawa matapeli wanaouza dawa mbele ya misikiti

Hivi kuna dawa ya kienyeji iliyouzwa kama ile ya kuitwa ngetwa? Mwenyewe alipoona mzigo unakubalika sokoni akawa anatoa matoleo tu ngetwa 1,ngetwa 2 nk😅
Yule mhuni alipiga sana hela; babu wa Loliondo anasubiri.
 
Ulichukua hatua gani? Ulirudi pale na kumchana live kwamba dawa yake ni feki na ni unga wa muhogo?
 
Yupo yule wa star TV muhindi..hii inaitwaa ujanaaa. Ila tunapigwa
 
Umewahi kukutana na dawa ya kienyeji inaitwa MKUYATI?? Acha kabisa... Dawa zipo, tatizo ni utapeli.
 
Uzi wako umeusuka kitaalam Sana, lengo sio ku adress kutapeliwa. Lengo lilikuwa kutaka kuonyesh connection yao , ushirikina na huko wanako swali watu.

But umeuwek fresh ili upate hata mchango wao. Ngoja tuone
 
Ulichukua hatua gani? Ulirudi pale na kumchana live kwamba dawa yake ni feki na ni unga wa muhogo?
Hawa jamaa wanaishi kama digidigi mkuu. Wanahama mkoa hadi mkoa na msikiti hadi msikiti. Kwa utapeli wao, kama wangekaa mahali pamoja kwa muda mrefu, wateja wangewashusha mshipa.
 
Asante mkuu. Kivumbasi ni nn na nachanganya kwa ratio gani mkuu?
Matapeli wa dawa hawako mbele ya misikiti tu. Wamejaa kila mahali na pengine wale wa sehemu nyingine ndiyo hatari zaidi. Ogopa wale wanaotangaza au kuwa na vipindi kwenye TV... sijui mnawaita kina dr Mwaka....
 
Uzi wako umeusuka kitaalam Sana, lengo sio ku adress kutapeliwa. Lengo lilikuwa kutaka kuonyesh connection yao , ushirikina na huko wanako swali watu.

But umeuwek fresh ili upate hata mchango wao. Ngoja tuone
Hiyo ni tafsiri yako mkuu. Mimi nimeshusha uzi kama ulivyo na watu wote wanaruhusiwa kureply bila kuzingatia itikadi zao including FaizaFoxy
 
Matapeli wa dawa hawako mbele ya misikiti tu. Wamejaa kila mahali na pengine wale wa sehemu nyingine ndiyo hatari zaidi. Ogopa wale wanaotangaza au kuwa na vipindi kwenye TV... sijui mnawaita kina dr Mwaka....
Wale wa kwenye TV na redio ndio wezi na matapeli kuliko maelezo. Jana nilisikia mmoja akiongea redioni kuwa UTI inasababisha upungufu wa nguvu za kiume. Na alisisitiza kuwa bakteria wanaosababisha UTI hushambulia red blood cells na kupelekea upungufu wa nguvu za kume. Hili ni janga la kitaifa.
 
Sijawahi kuona tunguli mbele ya msikiti zaidi ya kuwepo dawa za asili. Acha kuongeza chumvi mkuu. Umeweka na picha kabisa Ili kuthibitisha uongo wako.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Sijawahi kuona tunguli mbele ya msikiti zaidi ya kuwepo dawa za asili. Acha kuongeza chumvi mkuu. Umeweka na picha kabisa Ili kuthibitisha uongo wako.
Mkuu hebu fanya uchunguzi. Hawa watu wanakuwa na tunguli, vibuyu na vifaa vingine vya ajabu ajabu.

Siku niliyotapelewa, yule tapeli alikuwa na vifaa hivyo vyote pamoja na miti na matunda yenye shape za ajabu ajabu ambayo ameyaokota huko mwituni na kuyatumia kama.vifaa vya utapeli.
 
Waislamu wanauziana mambo ya kichawi wenyewe kwa wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…