Nawadharau sana Waingereza kwa kuendeleza utawala wa Kifalme

Best umewafaidi waingereza vilivyo kiufupi wamekupa maisha ...so lazima uwapende monarchy [emoji2957]
 
We unaona primitive ila wapo na amani na Taifa linazdi kuendelea mbele..... usisahau... old is Gold
 
Hujasikia mzazi alikemea vijana waache kuwafuata wasichana halafu yeye ana wake watatu na vimada?
 
 
Mbona nyie chadema mnaamini mbowe na familia yake ndo wanaweza kuwavusha?
 
Mawazo hayana tofauti na yale ya shetani alipotafuta usawa na Mungu na hivyo kupelekea kutupwa kutoka mbinguni kuja huku duniani ambako amebaki anaswampa huku na kule!
 
Unawadharau sasa bora kipi huu uongozi wa kifalme au huo uongozi wahuku wachama kimoja sema tu hatuna tofauti fisim wanapeana vijiti tu kuanzia tupate uhuru.
Mrema kafariki hajashika hata mbowe na yule mwingine hivyo hivyoo .

Sasa hatunatofauti na nchi za africa hakuna democrasia hata kidogo .
 
Siyo kweli Angekuwa sisi wangeshatuwekea sijui sanctions sijui upuuzi gani na kutuita wajinga.Waache ujinga huu mara moja wazingatia demokrasia!
Hiyo dharau yako hata haiwapi shida

Afu acha kuwapangia wenzio Panga Yako
 

Salary Slip: Hiyo system unayoidharau labda ndio iliyoifanya ikawa taifa lililoweza tawala mataifa kama 56 uliangalia Commonwealth. Kumbuka pia kuna nchi kama 14 mpaka leo unatambua mtawala wa kifalme/Malkia wa uingereza ndio kiongozi wao!

Usisahau pia mapinduzi ya viwanda ambayo yamezaliwa Uingereza 1700 na ndio yaliyoibadili dunia hii! Swali kubwa ni kwa nini ilitokea Uingereza? Huwezi kuukimbia ukweli kuwa mfumo wa utawala unaouona wa Kijima ulitengeneza pia stability kubwa iliyozaa maendeleo na kuwawezesha Waingereza kutoka kwenda kutafuta malifghafi kwa ajili ya viwanda vyao na kuanza kujitwalia makoloni.

Ni huo ujima unaoudharau umelifanya taifa hilo kutuachia lugha ambayo kwa sehemu kubwa ndio inayounganisha ulimwengu!
Kumbuka pia kama Waingereza waliohamia Marekani wasingegoma kuwa chini ya huo mfumo, leo hata Marekani iingekuwa mali ya Ufalme huo!

Labda ni sisi kujifunza kipi hasa Utawala huo wa Kifalme ulileta kwa wananchi wake na kufanya Uitawale Nusu ya dunia!
Ni kweli usiokimbilika Ukoloni ni kitu kibaya sana, lakini lazima tukubali ukoloni uliwezekana tu kwa vile Mkoloni alikua na uwezo dhidi ya mataifa ambayo aliyatiishi chini yake, utawala wa kifamle uliifanya Uingereza kuwa ni taifa lenye uwezo wa uchumi na teknolojia kuanzia miaka ya 1700, falme na tawala nyingi miaka hiyo zilikua nyuma sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…