View attachment 3266333
Hii picha sio ya kuigiza. Ni picha halisi ilipigwa na camera ya simu ambayo haikuwa na spidi sana ndio maana unaona kuna sehemu za picha ziko out of focus, kuonyesha zilikuwa zina movement ya kasi zaidi spidi ya camera ya simu.
Na picha inajieleza. Hasira za mwalimu, maumivu ya mwanafunzi na shock usoni mwa wanafunzi wanaotazama tukio hili.
Sasa niambieni. Nipate picha au video clip kama hii na huyo hapo anaesulubiwa awe ni mwanangu, mnafikiri nitamfanya nini huyo mwalimu, kumpeleka kwa polisi wetu hawa ambao wengi ni wala rushwa? Ni kosa gani ambalo huyu mwanafunzi anaweza kuwa amefanya kiasi mwalimu amwadhibu kwa ghadhabu na ukatili namna hii - amembaka mama yake?
Walimu wenye tabia hii chukueni tahadhali. Mtaja kutana na watu ambao akili zao zitakuwa kama zenu, na hamtashinda.