Nawaheshimu sana walimu, lakini mwalimu yeyote akimfanyia mtoto wangu kama inavyoonyesha picha hii nitamtafuta kokote alipo tumalizane

Nawaheshimu sana walimu, lakini mwalimu yeyote akimfanyia mtoto wangu kama inavyoonyesha picha hii nitamtafuta kokote alipo tumalizane

Watoto watukutu wataendelea kunyukwa tu mashuleni hakuna wa kuzuia hili. Haki za wato zinazingatiwa
Umewahi kukutana na shule yeyote inapima afya za watoto kabla ya kuwachapa? Kuna mtu unampiga kofi tu anaanguka na kufa, halafu unakuwa na murder case. Hadi wamalize uchunguzi na kusema ni kweli sio kofi tu lilimuua umeshalaa ndani miaka sita. Murder case haina dhamana
 
Mkuu, ndio maana basi alikuwa anawapa kichapo sana watoto wake wasipofanya vizuri darasani. Sasa walimu kama Magufuli hawatakiwi kabisa, wana mental issues. Si unaona mentality ya "kuchapa watu bila huruma" aliileta hadi kwenye uraisi? Akamchapa na Ben Saanane. Anaweza kuwa alifanya vizuri katika baadhi ya sehemu,lakini kwenye hili la kuchapa alikuwa na tatizo la afya ya akili
Inshu sio mental health
Inshu walikuwa wana akili au hawana akili ?
Ndio msingi wa hii hoja
Mental health issues ipo kwa kila mtu ila inategea ipo kwenye jambo gani
 
Miaka ya nyuma tumekula sana hizo stiki tena walimu walikua na misuli kweli kweli 😀😀😀, kwa vitoto vya miaka ya karibuni sishauri sana vichapwe fimbo nyingi afya zao ni mgogoro
Sasa chief unakuta mtoto anapigana denda na mwenzie hivi watoto kama utawaacha tu hivo hivo
 
Tuonyeshe hao watoto wanaoongooza kwa ubunifu bongo hii ambao hawajawahi kuchapwa viboko.
Wamebuni nini?
Nenda shule kama Feza, Shamsiye na IST kwa uchache uone vipaji wa watoto na nidhamu waliyokuwa nayo.

Ikumbukwe shule hizo hakuna adhabu ya viboko hata kwa bahati mbaya.

Mkuu, unajua kwa mujibu wa muongozo wa adhabu mashuleni mwalimu yeyote hatakiwi hata kuonekana ameshika kiboko anazurura nacho?
 
View attachment 3266333

Hii picha sio ya kuigiza. Ni picha halisi ilipigwa na camera ya simu ambayo haikuwa na spidi sana ndio maana unaona kuna sehemu za picha ziko out of focus, kuonyesha zilikuwa zina movement ya kasi zaidi spidi ya camera ya simu.

Na picha inajieleza. Hasira za mwalimu, maumivu ya mwanafunzi na shock usoni mwa wanafunzi wanaotazama tukio hili.

Sasa niambieni. Nipate picha au video clip kama hii na huyo hapo anaesulubiwa awe ni mwanangu, mnafikiri nitamfanya nini huyo mwalimu, kumpeleka kwa polisi wetu hawa ambao wengi ni wala rushwa? Ni kosa gani ambalo huyu mwanafunzi anaweza kuwa amefanya kiasi mwalimu amwadhibu kwa ghadhabu na ukatili namna hii - amembaka mama yake?

Walimu wenye tabia hii chukueni tahadhali. Mtaja kutana na watu ambao akili zao zitakuwa kama zenu, na hamtashinda.
Ifike muda tuseme ukweli tu yaani hizi shule zetu zimejaa ukatiri kwa wanafunzi. Hebu fikiria hapo unatengeneza raia wa namna wa baadae kwa sababu naye atakuja kuamini njia pekee ya kufikia suluhu kwa kila jambo ni kwa kutumia nguvu na adhabu ngumu kama hivyo. Haiko sawa namna hii, kwani kumrekebisha mtu kwa upendo na akakuelewa inaleta shida gani!
 
Inshu sio mental health
Inshu walikuwa wana akili au hawana akili ?
Ndio msingi wa hii hoja
Mental health issues ipo kwa kila mtu ila inategea ipo kwenye jambo gani
Kwani wewe kipimo cha akili ni kipi kwako?
 
Ifike muda tuseme ukweli tu yaani hizi shule zetu zimejaa ukatiri kwa wanafunzi. Hebu fikiria hapo unatengeneza raia wa namna wa baadae kwa sababu naye atakuja kuamini njia pekee ya kufikia suluhu kwa kila jambo ni kwa kutumia nguvu na adhabu ngumu kama hivyo. Haiko sawa namna hii, kwani kumrekebisha mtu kwa upendo na akakuelewa inaleta shida gani!
Ndio maana tunaishia kuwa na maraisi ukimpinga anaamuru dola ikuue, au Polisi wakuweke ndani bila dhamana!

Na katika level ya familia, adhabu za kupiga watoto shuleni wanapokuja kuwa watu wazima zinaleta mentality kwa waumekuwa mke akikosea alikurekebishwa lazima apigwe, na mke akikosea anaona nihalali mume ampige!

Mtoto wa kiume au kike aliekulia katika nyumba ambayo baba anampiga mama ana uwezekano mkubwa wa kumpiga mkewe atakapooa, na wa kike kuona kupigwa na mume ni sawa anapokosea. Ndio maana suala la kupiga wake huko Musoma sio rahisi kuliondoa!
 
Nenda shule kama Feza, Shamsiye na IST kwa uchache uone vipaji wa watoto na nidhamu waliyokuwa nayo.

Ikumbukwe shule hizo hakuna adhabu ya viboko hata kwa bahati mbaya.

Mkuu, unajua kwa mujibu wa muongozo wa adhabu mashuleni mwalimu yeyote hatakiwi hata kuonekana ameshika kiboko anazurura nacho?
Hao wana akili za darasani lakini hawana ubunifu wowote wa kushangaza.
Feza ina miaka mingi tangu ianzishwe..ni mtu gani amesoma pale amebuni chochote tunachojivunia kama Taifa?
 
Ifike muda tuseme ukweli tu yaani hizi shule zetu zimejaa ukatiri kwa wanafunzi. Hebu fikiria hapo unatengeneza raia wa namna wa baadae kwa sababu naye atakuja kuamini njia pekee ya kufikia suluhu kwa kila jambo ni kwa kutumia nguvu na adhabu ngumu kama hivyo. Haiko sawa namna hii, kwani kumrekebisha mtu kwa upendo na akakuelewa inaleta shida gani!
Mkuu majitu mengi humu yamepitia malezi ya kikatili kwa wazazi wao hadi mashuleni hivyo wanaamini bila adhabu zenye viashiria vya ukatili mambo hayaendi kitu ambacho sio kweli.

Wapo watu hawakupitia malezi ya kikatili na wana maisha mazuri zaidi ya wale waliopitia malezi ya kikatili ambao huishia kuamini katika mabavu mwisho wa siku wanaishia pabaya.
 
Kwani wewe kipimo cha akili ni kipi kwako?
Inategemea upo wapi ndio utapimwa akili
Kama upo chooni utakuwa na akili za chooni
Kama upo bar utakuwa na akili za bar
 
Tafsiri ya ukatili kwa mtoto iko wazi kimazingira. Mtoto mtukutu ataadhibiwa kwa kwa uzito wa kosa lake. Hauliwi wala hajeruhiwi mpaka damu zimtoke. Atachapwa au kufinywa au kurudishwa nyumbani akamlete mzazi wake. Zipo adhabu kwa watoto watukutu, wenye malezi mabaya ya wazazi wake yaishie kwao. Mtoto wako akija shuleni na tabia zenu mbaya huko kwenu atanyooshwa tu
 
Sasa chief unakuta mtoto anapigana denda na mwenzie hivi watoto kama utawaacha tu hivo hivo
Kuna madogo waling'oa mabeseni ya kunawia mapya kabisa karibu 8 kwenye shule x ya sekondari , hawakuishia hapo wakapulizia spray ya rangi ukutani rangi iliyopakwa na fedha za walipa kodi tena wasio na kipato na kuandika matusi siku hiyo hiyo walikutwa wanalawitiana huko vyooni wewe kama mwalimu utawapa adhabu gani..?
 
Hao wana akili za darasani lakini hawana ubunifu wowote wa kushangaza.
Feza ina miaka mingi tangu ianzishwe..ni mtu gani amesoma pale amebuni chochote tunachojivunia kama Taifa?
Kwani lengo la nyinyi walimu kutoa adhabu za kikatili ni kwasababu ya kumfanya mtoto awe mbunifu ama kumfanya mtoto awe mwenye nidhamu?

Kama suala ni nidhamu basi ndiyo maana tunasisitiza nidhamu haiji kwa vipigo bali kuongea lugha nzuri yenye ushawishi kwa mtoto.

Nimekutolea mfano mimi binafsi sijawahi hata kwa bahati mbaya kumchapa mwanangu lakini namna ninavuoongea nao kama marafiki zangu huwa wananiheshimu mno na chochote ninachowaelekeza wanakifanya without any exception.
 
Kuna madogo waling'oa mabeseni ya kunawia mapya kabisa karibu 8 kwenye shule x ya sekondari , hawakuishia hapo wakapulizia spray ya rangi ukutani rangi iliyopakwa na fedha za walipa kodi tena wasio na kipato na kuandika matusi siku hiyo hiyo walikutwa wanalawitiana huko vyooni wewe kama mwalimu utawapa adhabu gani..?
Ukiwachapa ndiyo wataacha tabia hizo?

Mbona kuna watoto mnaadhibu karibu kila siku na bado wanaishia kuwa watukutu hadi wamefikia hatua hawawaogopi wala kuwaheshimu walimu mnapigana nao.
 
Umewahi kukutana na shule yeyote inapima afya za watoto kabla ya kuwachapa? Kuna mtu unampiga kofi tu anaanguka na kufa, halafu unakuwa na murder case. Hadi wamalize uchunguzi na kusema ni kweli sio kofi tu lilimuua umeshalaa ndani miaka sita. Murder case haina dhamana
huwezi kukaa na watoto rundo halafu usiwajue afya zao, akili zao na mahali wanapotoka. Watoto wenye matatizo ya afya wanajulikana na huwa hawaguswi adhabu yao ni kuwatoa darasani waende nyumbani kama wanakuwa ni wasumbufu
 
Back
Top Bottom