The mission 2017
JF-Expert Member
- Aug 14, 2017
- 1,748
- 3,229
Umeongea vzuri sana juu ya malezi.Kuchapwa ndiyo njia pekee ya mtoto kuelewa?
Hakika watumwa ni wengi barani Afrika.
Mimi sijawahi kumchapa mtoto wangu lakini nikimuelekeza jambo analifanya kwa haraka kwasababu nimemlea kama rafiki nazungumza naye namna nzuri ya kuishi na wazazi pamoja na jamii kwa ujumla.
Lakini hali ni tofauti kwa watoto wa majirani maana wazazi wao ni aina yako wanaoamini kwenye kuchapa. Wamekuwa wakiwachapa lakini ndiyo kwanza watoto wamekuwa sugu.
Kilichomsababisha achapwe jana anakirudia leo kitu kile kile.
Kama wewe ni mwalimu mfanye mwanafunzi awe rafiki atakusikiliza kwa umakini na kwa upendo mkubwa na hata kuelewa darasani anakuelewa vizuri zaidi kuliko mwalimu chapa chapa ambaye anachukiwa na watoto.
Halikadhalika ukiwa mzazi mfanye mtoto awe rafiki uta enjoy maisha maana hatokuficha kitu chochote kiwe kibaya ama kizuri.
Sasa fikiria juu ya watoto wa majirani, Ambao hawasikii kwa wazazi wao mpaka wapate viboko.
wanaweza kusikia shuleni bira viboko? Na mind you viboko vingi shuleni sio kwa sababu ya kuto kuelewa darasani mara nyingi ni Mambo madogo madogo mfn: Kuwai shuleni, Kufanya Usafi wa mazingira, Kuvaa vzuri na kuvaa nguo safi, Kutokuoiga kelele darasani, N.k
Unawezaje kudisclipline watoto 200 kutoka buza, Tandale na Kimara bila kutumia kiboko, Ikiwa tu wazazi wao, wano miliki watoto wa3 wanatumia kiboko ndo mtoto anaoga