Nawaheshimu sana walimu, lakini mwalimu yeyote akimfanyia mtoto wangu kama inavyoonyesha picha hii nitamtafuta kokote alipo tumalizane

Nawaheshimu sana walimu, lakini mwalimu yeyote akimfanyia mtoto wangu kama inavyoonyesha picha hii nitamtafuta kokote alipo tumalizane

Sasa chief unakuta mtoto anapigana denda na mwenzie hivi watoto kama utawaacha tu hivo hivo
Sheria za shule zinasemaje kuhusu hilo suala? Kumbe mnavyowapa wazazi joining instructions form hata nyie hamsomi kilichoandikwa 😂

Sometimes dharau kwa walimu zinatengenezwa na wenyewe
 
View attachment 3266333

Hii picha sio ya kuigiza. Ni picha halisi ilipigwa na camera ya simu ambayo haikuwa na spidi sana ndio maana unaona kuna sehemu za picha ziko out of focus, kuonyesha zilikuwa zina movement ya kasi zaidi spidi ya camera ya simu.

Na picha inajieleza. Hasira za mwalimu, maumivu ya mwanafunzi na shock usoni mwa wanafunzi wanaotazama tukio hili.

Sasa niambieni. Nipate picha au video clip kama hii na huyo hapo anaesulubiwa awe ni mwanangu, mnafikiri nitamfanya nini huyo mwalimu, kumpeleka kwa polisi wetu hawa ambao wengi ni wala rushwa? Ni kosa gani ambalo huyu mwanafunzi anaweza kuwa amefanya kiasi mwalimu amwadhibu kwa ghadhabu na ukatili namna hii - amembaka mama yake?

Walimu wenye tabia hii chukueni tahadhali. Mtaja kutana na watu ambao akili zao zitakuwa kama zenu, na hamtashinda.
Shule za manunda huko uswazi kawaida sana. Na litoto likitoka hapo bado lipo kamili gado. Sasa wewe mpeleke mtoto wa blubendi hapo kama hajazikwa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ukiwachapa ndiyo wataacha tabia hizo?

Mbona kuna watoto mnaadhibu karibu kila siku na bado wanaishia kuwa watukutu hadi wamefikia hatua hawawaogopi wala kuwaheshimu walimu mnapigana nao.
Ndiyo maana wanachapwa halafu wanaitwa wazazi wao, na kufukuzwa shule
 
Hao wana akili za darasani lakini hawana ubunifu wowote wa kushangaza.
Feza ina miaka mingi tangu ianzishwe..ni mtu gani amesoma pale amebuni chochote tunachojivunia kama Taifa?
January Makamba hakusoma Feza? Alibuni kuwagawia wabunge mitungi ya gas ili wapitishe muswaada wa wizara ya nishati!!!

Hii kanuni hadi leo inatumika na CCM kutafuta kura!
 
Tafsiri ya ukatili kwa mtoto iko wazi kimazingira. Mtoto mtukutu ataadhibiwa kwa kwa uzito wa kosa lake. Hauliwi wala hajeruhiwi mpaka damu zimtoke. Atachapwa au kufinywa au kurudishwa nyumbani akamlete mzazi wake. Zipo adhabu kwa watoto watukutu, wenye malezi mabaya ya wazazi wake yaishie kwao. Mtoto wako akija shuleni na tabia zenu mbaya huko kwenu atanyooshwa tu
Mkuu mbona watoto watukutu wanaongezeka kila uchwao licha ya hizo adhabu za kikoloni mnazotoa?

Kumshirikisha mzazi wa mtoto ni jambo zuri huenda kwa pamoja mkaongea ukajikuta mtoto anabadilika kuwa mwenye nidhamu.

Nina mifano halisi ya watoto watukutu waliobadilika na kuwa wema baada ya mimi binafsi, mtoto, mzazi wake pamoja na walimu kukaa pamoja kumsihi mtoto faida za yeye kuwa mtoto mwema katika jamii.

Ikumbukwe kabla ya hapo mtoto alishazoea kupewa adhabu za viboko wala hajali lakini njia ya mazungumzo tu ilitatua changamoto yote hadi leo wapo wazazi na walimu wakuu/wakuu wa shule huwa wananihitaji niende ili kwa pamoja tuzungumze na watoto.
 
Hao wana akili za darasani lakini hawana ubunifu wowote wa kushangaza.
Feza ina miaka mingi tangu ianzishwe..ni mtu gani amesoma pale amebuni chochote tunachojivunia kama Taifa?
Una masikhara wewe, sema hujui ujuzwe. Ukiona mtoto anasoma Feza halafu mnakutana naye mtaani anazurula basi ndio hao hao ambao wazazi wao akili finyu. Wazazi wenye akili timamu anapeleka mtoto Feza huku ana connection za kutosha, tafuta wahitimu wa Feza halafu uulize wengi kati ya waliosoma nai wako wapi, jibu utalipata
 
Shuleni kila mtoto huadhibiwa kulingana na afya yake na utimamu wa akili, wengine viboko, wengine vifinyo, nkenzi, wengine hutolewa darasani waende kwao, wengine kung'oa nyasi, visiki, kufagia, wengine hawafuatiliwi wanachoandika ni nini, wengine daftari zao hazisaihihishwi. Wazazi wafundisheni watoto wenu tabia njema wawapo nyumbani na waendapo shuleni wakafanye vema
 
Sheria za shule zinasemaje kuhusu hilo suala? Kumbe mnavyowapa wazazi joining instructions form hata nyie hamsomi kilichoandikwa 😂

Sometimes dharau kwa walimu zinatengenezwa na wenyewe
🤔Hujanijibu mtoto kama Huyu ungemfanyaje?
 
Kuna madogo waling'oa mabeseni ya kunawia mapya kabisa karibu 8 kwenye shule x ya sekondari , hawakuishia hapo wakapulizia spray ya rangi ukutani rangi iliyopakwa na fedha za walipa kodi tena wasio na kipato na kuandika matusi siku hiyo hiyo walikutwa wanalawitiana huko vyooni wewe kama mwalimu utawapa adhabu gani..?
Hawa ni fimbo 25 Kila mmoja na kufukuzwa shule basi 🤔huez acha watoto wanafokoana Vinyeo shuleni waje wafokoe na wengine🤔
 
Wito wangu kwa walimu jiepusheni sana na kuwaadhibu watoto bila kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa.

Ukipelekwa mahakamani kule ni sheria ndiyo inazungumza sio suala la maneno mtupu.

Utaambiwa kama ulimuadhibu mtoto kwa kufuata sheria, taratibu, muongozo na kanuni lete ushahidi.

Kumbuka mtumishi wa umma ukipatikana na hatia tu basi ajira huna na hutoajiriwa popote pale kwenye idara za serikali kwasababu una rekodi za uhalifu/jinai.

Fuateni utaratibu hata ikitokea bahati mbaya ukamjeruhi mtoto basi kile kitendo cha wewe kufuata utaratibu tu kinakulinda na kitatumika kama defense.

Hasira na kutaka sifa mbele ya walimu wenzako zitakufikisha pabaya na hakuna mwalimu mwenzako atakayekuja kukunasua bali wataendelea na majukumu yao kama kawaida huku wewe ukiwa matatizoni.
 
Nina asili hiyo toka nimezaliwa nilizaliwa ijumaa sambili usku
Sasa kama ni asili yako kwa nini upigwe? Ni sawa na greenkwanja JKT kumpiga kilema wa mguu kwa sababu hatembei vizuri
 
Shule za manunda huko uswazi kawaida sana. Na litoto likitoka hapo bado lipo kamili gado. Sasa wewe mpeleke mtoto wa blubendi hapo kama hajazikwa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Bahati mbaya mauaji ya wanafunzi 99.9% yanatokea kwenye hizo shule the so called za manunda
 
Back
Top Bottom