Nawaheshimu sana walimu, lakini mwalimu yeyote akimfanyia mtoto wangu kama inavyoonyesha picha hii nitamtafuta kokote alipo tumalizane

Nawaheshimu sana walimu, lakini mwalimu yeyote akimfanyia mtoto wangu kama inavyoonyesha picha hii nitamtafuta kokote alipo tumalizane

Miaka ya nyuma tumekula sana hizo stiki tena walimu walikua na misuli kweli kweli 😀😀😀, kwa vitoto vya miaka ya karibuni sishauri sana vichapwe fimbo nyingi afya zao ni mgogoro
Unaona sasa licha ya wewe kukutana na adhabu za kikatili lakini haikukusaidia chochote badala yake ukaishia tena kuwa mwalimu.😒

Kama adhabu za viboko zingekusaidia maana yake leo ungekuwa hata daktari mwanasheria ama injinia.

Kwahiyo tunarudi kwenye makubaliano kwamba viboko haviwezi kumsaidia mtoto kufikia ndoto zake badala yake kuzungumza kwa smooth language pengine ingemsaidia zaidi mtoto.
 
Akili kama hizi ndizo zinasababisha jamii yote kuamini ualimu ni kutokuwa na uwezo wa kupambanua mambo.

Hakuna sheria yoyote ile inayotamka kwamba mtoto achapwe viboko 25 hata liwe kosa kubwa kiasi gani.

Mtoto ataadhibiwa viboko vinne pekee kwa kosa kubwa kabisa tena liwe la kuidhalilisha shule na adhabu itatolewa na mwalimu mkuu/mkuu wa shule.

Mwalimu wa kawaida hapaswi kutoa adhabu isipokuwa tu kama atapewa ruhusa ya maandishi na mwalimu mkuu/mkuu wa shule ya kutoa adhabu.

Haya mambo ya kutumia hasira badala ya kuzingatia sheria ndiyo yanawaponza walimu wengi na kujikuta matatani.
Ebu nikupe kisa wakati tupo advance kuna bwana alikua na miaka 22 yule jamaa bwana akawa na analala nyumbani kwa mke wa mtu, siku hiyo wapangaji wakamsanua jamaa aje afumanie, oya jamaa alikua na panga, huyo dogo ashukuru ngumu aliyompiga yule mume wa yule mwanamke ilmkalisha jamaa sekunde kadhaa dogo akakimbia, mbio

Basi jamaa aliporudi skuli ikapigwa tafutwa skul nzima na mgoni wake hadi akapatikana Huyu, watu kama lazima kidogo utumie brutal way mkuu
 
Kwasasa katika jamii kuna kiwango kikubwa cha mmomonyoko wa maadili, kuna watoto shuleni ni wakorofi sana. Wengine wanafikia hatua hata ya kuwatukana walimu wao pamoja na watu waliowazidi umri, heshima hakuna kabisa. Mtoa mada kwa taarifa yako adhabu nyingi zinazotolewa shuleni hazihusiani na mtoto kutokuwa na akili darasani bali ni ukorofi wa watoto kama vile upigaji kelele, uchelewaji, kiburi, kutotii maagizo/maelekezo wanayopewa na walimu, wizi, kutofanya usafi, kutofanya home work, kutoandika notes, kuja na redio na simu shuleni na kusikiliza muziki kwa kupitia earphone wakati wa vipindi. Mwalimu anapoona mwanafunzi anarudia rudia makosa haya anahisi kudharauliwa, hii inapelekea hasira inayosababisha adhabu ya viboko.
Watoto wengi japo sio wote ambao huwa wanachapwa mara kwa mara shuleni ukifatilia mienendo yao hata nyumbani kimaadili hawako vizuri.
Hivyo wazazi tujitajidi kuwalea watoto wetu katika maadili mema, ukiwalea vema hiyo tabia itakuwa reflected hata huko nje.
Tupunguze mihemko, lea watoto wako katika maadili mema ili wawe na nidhamu, fuatilia mienendo ya mwanao, pia fuatilia maendeleo yake kitaaluma. Hutasikia wamechapwa huko shuleni.
 
Umefanya nicheke tu mkuu.
 
Siku hizi hatuwachapii kivilee wengi broiler, mtawachapa nyinyi wenyewe ,unatoka jasho alfu unaua unafungwa kisa toto tundu wa mtu aaghr
Afadhali wewe umeshtukia mchezo mapema.

Ukijeruhi ama kuuwa hilo ni lako peke yako kila mtu atakushambulia ikiwemo serikali.

Jela utaenda peke yako hakuna mwalimu atakayekuja kukusaidia kifungo hata kama alikuwa anakushangilia unavyochapa watoto hovyo.

Ni vema kujiepusha na kutoa adhabu kiholela maana watoto wengi siku hizi afya sio imara anaweza kuwa na magonjwa yake ya muda mrefu lakini siku unamchapa tu ndiyo unammalizia hatimaye msala unakuandama wewe.
 
Kwasasa katika jamii kuna kiwango kikubwa cha mmomonyoko wa maadili, kuna watoto shuleni ni wakorofi sana. Wengine wanafikia hatua hata ya kuwatukana walimu wao pamoja na watu waliowazidi umri, heshima hakuna kabisa. Mtoa mada kwa taarifa yako adhabu nyingi zinazotolewa shuleni hazihusiani na mtoto kutokuwa na akili darasani bali ni ukorofi wa watoto kama vile upigaji kelele, uchelewaji, kiburi, kutotii maagizo/maelekezo wanayopewa na walimu, wizi, kutofanya usafi, kutofanya home work, kutoandika notes, kuja na redio na simu shuleni na kusikiliza muziki kwa kupitia earphone wakati wa vipindi. Mwalimu anapoona mwanafunzi anarudia rudia makosa haya anahisi kudharauliwa, hii inapelekea hasira inayosababisha adhabu ya viboko.
Watoto wengi japo sio wote ambao huwa wanachapwa mara kwa mara shuleni ukifatilia mienendo yao hata nyumbani kimaadili hawako vizuri.
Hivyo wazazi tujitajidi kuwalea watoto wetu katika maadili mema, ukiwalea vema hiyo tabia itakuwa reflected hata huko nje.
Tupunguze mihemko, lea watoto wako katika maadili mema ili wawe na nidhamu, fuatilia mienendo ya mwanao, pia fuatilia maendeleo yake kitaaluma. Hutasikia wamechapwa huko shuleni.
Yote hayo makosa si yameorodheshwa kwenye sheria za shule na hukumu anayostahili kupewa anayezivunja? Ina maana walimu uwa mnatupa form ambazo hata nyie hamzisomi?
 
Inabidi na wao waanze kupewa adhabu wakikosea kama kuita mvua kuchimba visiki, kushika masikio ikibidi na mboko wacharazwe
 
Unaona sasa licha ya wewe kukutana na adhabu za kikatili lakini haikukusaidia chochote badala yake ukaishia tena kuwa mwalimu.😒
Id za jf zisikichanganye bwashee nina kazi nyingine tofauti na ualimu 😀😀, nawafundisha wakubwa na fimbo wanakula kisawasawa
 
Kuchapwa ndiyo njia pekee ya mtoto kuelewa?

Hakika watumwa ni wengi barani Afrika.

Mimi sijawahi kumchapa mtoto wangu lakini nikimuelekeza jambo analifanya kwa haraka kwasababu nimemlea kama rafiki nazungumza naye namna nzuri ya kuishi na wazazi pamoja na jamii kwa ujumla.

Lakini hali ni tofauti kwa watoto wa majirani maana wazazi wao ni aina yako wanaoamini kwenye kuchapa. Wamekuwa wakiwachapa lakini ndiyo kwanza watoto wamekuwa sugu.

Kilichomsababisha achapwe jana anakirudia leo kitu kile kile.

Kama wewe ni mwalimu mfanye mwanafunzi awe rafiki atakusikiliza kwa umakini na kwa upendo mkubwa na hata kuelewa darasani anakuelewa vizuri zaidi kuliko mwalimu chapa chapa ambaye anachukiwa na watoto.

Halikadhalika ukiwa mzazi mfanye mtoto awe rafiki uta enjoy maisha maana hatokuficha kitu chochote kiwe kibaya ama kizuri.
Oya Watoto watachapwa na hufanyi kitu.

Hata miaka yetu Wanafunzi walichapwa.
 
Yote hayo makosa si yameorodheshwa kwenye sheria za shule na hukumu anayostahili kupewa anayezivunja? Ina maana walimu uwa mnatupa form ambazo hata nyie hamzisomi?
mimi ni mzazi sio mwalimu.

Tuwalee watoto wetu kwa kuzingatia maadili, wanapostahili kuchapwa viboko wachapwe si shuleni tu hata nyumbani.

Shida inakuja pale mtoto anapochapwa kwenye matako yeye akajihami kwa kuweka mikono, fimbo inapopiga kwenye mkono/vidole vikivimba halafu akatokea mtu akachukua picha au video kwa kutumia simu then akaisambaza kwenye mitandao yani inakuwa gumzo nchi nzima.
Yani siku hizi tunaleo watoto kimayai mayai tu, hatutaki waguswe. Hi ni shida kubwa mno. Kwa mwendo huu baada ya hiki kizazi chetu kupita kikija kile cha pili (yani cha wajukuu wetu) kitakuwa kizazi cha ajabu sana.
 
Wanadhani kuwalea kimayai ndo kuwasaidia kumbe wanawaharibu
 
Hakuna mwalimu mtabe sababu ya uduni wa mishahara, no disrespect nawaheshimu walimu wote tz.
inabidi tujitokeze kuwatetea walimu kama wao hawawezi kujitetea huku wakijia misingi ya elimu na kanuni za ufundishaji pamoja na haki za watoto
 
Shule za Serikali hizo.
Ofisi imejaa mianzi vitabu Hakuna.
Yani unapiga Mtoto kwa Miguvu ambayo yaweza kutoa nishati ya Umeme vijiji vinne.

Kuna mda nawazaga kazi ya kufunza Mtoto imekaa Sawa kwa KE ...Njemba mje Huku tupike zege Mana kila mauaji ya wanafunzi ME ndio masteringi.
 
Mkuu majitu mengi humu yamepitia malezi ya kikatili kwa wazazi wao hadi mashuleni hivyo wanaamini bila adhabu zenye viashiria vya ukatili mambo hayaendi kitu ambacho sio kweli.

Wapo watu hawakupitia malezi ya kikatili na wana maisha mazuri zaidi ya wale waliopitia malezi ya kikatili ambao huishia kuamini katika mabavu mwisho wa siku wanaishia pabaya.
Mmh!
 
View attachment 3266333

Hii picha sio ya kuigiza. Ni picha halisi ilipigwa na camera ya simu ambayo haikuwa na spidi sana ndio maana unaona kuna sehemu za picha ziko out of focus, kuonyesha zilikuwa zina movement ya kasi zaidi spidi ya camera ya simu.

Na picha inajieleza. Hasira za mwalimu, maumivu ya mwanafunzi na shock usoni mwa wanafunzi wanaotazama tukio hili.

Sasa niambieni. Nipate picha au video clip kama hii na huyo hapo anaesulubiwa awe ni mwanangu, mnafikiri nitamfanya nini huyo mwalimu, kumpeleka kwa polisi wetu hawa ambao wengi ni wala rushwa? Ni kosa gani ambalo huyu mwanafunzi anaweza kuwa amefanya kiasi mwalimu amwadhibu kwa ghadhabu na ukatili namna hii - amembaka mama yake?

Walimu wenye tabia hii chukueni tahadhali. Mtaja kutana na watu ambao akili zao zitakuwa kama zenu, na hamtashinda.
You are Stupid...
 
Back
Top Bottom