Mkuu
VUTA-NKUVUTE unasahau kwamba:
1) Kampeni siyo za Urais tu, kuna Wabunge na Madiwani. Wote hao wanahitaji fedha kumudu kampeni. Je, chama kilijipangaje mapema, maana muda wa Uchaguzi Mkuu hujulikana?
2) Viongozi wa CHADEMA, na kwenye kampeni zinazoendelea, Lissu mgombea Urais amesikika akidai CCM imeharibu uchumi watu wamekuwa masikini kuliko awamu zilizopita. Hao wanaombwa kuchangia CHADEMA wana uwezo gani au ndio mpango wa kuwafanya masikini ili hayo madai yawe kweli?
3) CHADEMA, kama chama kikuu, kilikuwa kinapata mabilioni ya ruzuku. Isitoshe wabunge nao wamechangia kila mwezi na kufikisha mabilioni. Je, hii fedha imetumikaje maana hata ofisi, japo moja ya chama, haijajengwa.
Hiki ndio chama cha kuomba kuchangiwa gharama za kampeni?