Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Kwani ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi? Wananchi wana hali mbaya kwa nini muwachangishe?
Kwani kwa kipindi cha miaka 5 shughuli za chama chao ziligharamiwa na fedha ipi???

Au nawe unaamini kuwa chama kilizimia ama kufa???
 
Hata kidogo hicho kionekane kimefanya jambo lenye utaifa. Je, vyama visivyo na ruzuku?

Jambo lenye utaifa kwani wao wanakusanya kodi?

Ww mshahara wako mbona ujaenda kujenga barabara?
 
Wangeweka namba za simu mtandaoni watu wachange,tigo,voda,eatel,halotel na zantel.kila mwenye nacho na mapenzi mema angechanga,hata 500 mtu atachanga.kwani zile faini zilichangwaje hii ya kampeni oshindikane
 
hata mie naamini kamanda!
Kitendo cha risasi 16 kupigwa kutokea kushoto, zikaukwepa mguu wa kushoto kisha zikakata kona kuupiga mguu wa kulia ili kumuokoa dereva aliyekuwa amekaa kulia kwa Lisu - Huo lazima uwe muujiza.

Ww ukilalia kiti Cha dereva kama vile unavyomlalia wife wako, miguu inakuwa Sawa na kama ukikaa kawaida?
 
Sitaki niwachoshe kwa meneno mengi. Nawaambieni tu kwa kifupi na kwa uhakika. Bakuli la michango analolitembeza mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu si la kubezwa au kumezwa. Yaweza kuwa ni kwa kujua au kutokujua, Lissu anaruka kikwazo kikuu kilichosukwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu: ukata kwa vyama vya upinzani. Ukata tata ungewakata na kuwavuta wapinzani nyuma na kuwafanya washindwe kufanya kampeni.

Mipango kabambe ilishasukwa kitambo kuvifanya vyama vya upinzani mwaka huu kuandamwa na ukata wa kifedha. CCM yetu yenyewe, kwakuwa ina rasilimali za kutosha na kutisha na kwakuwa imejibanza kwenye koti la Serikali, ilijiandaa kujidai itakavyo kwenye kampeni hizi huku wapinzani wakishindwa kufanya kampeni. Mipango ilisukwa vyema. Kampeni zina gharama nyingi: usafiri, malazi,mavazi, chakula, vifaa vya sauti, majukwaa na kadhalika.

Mipango ya kuufanya ukata umee kwenye vyama vya upinzani ilianza miaka kadhaa iliyopita. Karibu kila chama kikubwa cha upinzani hapa nchini vikiwemo CHADEMA, ACT na NCCR-Mageuzi kina chama au vyama rafiki nje ya Tanzania. Marafiki hao wa nje husaidia vyama hivyo kifedha hasa kwenye harakati kama hizi za kiuchaguzi. Na hakukuwa na ubaya kuhusu kusaidiana huko. Lakini, mwaka huu misaada hiyo imepigwa pini. Imezibwa. Hakuna misaada tena. Ukata!

Lissu ajaziwe bakuli lake. Achangiwe. Hata mimi, kama mfuasi ninayejinafasi wa demokrasia ya vyama vingi, nimeshamchangia Lissu. Lazima tuwe na mgombea strong wa upinzani ili kutufanya tuchague vyema. Lazima mwaka huu mchuano mkali uwe kati ya Dkt. Magufuli na Lissu. Lazima tusikie sera za kila mmoja wao na tuamue. Bakuli la Lissu, hata kama litakejeliwa na kudhihakiwa, lina maana kubwa: linaruka mipango ya kidhalimu ya kutengeneza ukata kwa wapinzani.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kigoma, Tanzania)
Hivi zile pesa za wabunge wa Chadema walizokuwa wanachangia kutoka kwenye mishahara yao kwa ajili ya uchaguzi zimeenda wapi mkuu?
 
Lissu ni mpango wa Mungu kwa Watanzania. Haiwezekani kawaida tu mtu akapona risasi 16 alafu asiwe mpango wa Mungu.

Mwaka huu historia kuu ya kuangushwa Chama cha mapinduzi inaenda kuandikwa Tanzania.
Mungu tu pamoja na Lissu!

Amen Mkuu
 
Mwl Nyerere, Baba wa Taifa aliwahi kusema kwa lugha yake ya kuzaliwa akimaanisha "anayeficha ugonjwa mauti inamuumbua".

Si wajibu wangu kutafuta ukweli wa tuhuma dhidi ya M/Kiti wa CHADEMA kwa kuwa siyo mwanachama. Mimi kamwe nitakuwa mwanachama wa chama kinachoendeshwa kama SACCOS. Huo ndio ukweli mtupu.
Bado mweupe sana kichwani, endelea kujifunza kupitia darasa la jf.
 
Kama huelewi nyamaza, gharama za uchaguzi unajua ni kiasi gani? Na chama tawala unajua vyanzo vyake vya pesa?
Kwanini unataka kuzuia watu kuhoji. Nyie jamaa sio kabisa! Asiyeelewa anaeleweshwa sio kunyamazishwa.
 
Mbowe hata tukichanga yee anakura ela tu. Ndo maana mimi niriachaga kuchanga
Tangu lini uliichangia chadema wewe?. Kanunue zile chupi za chama chakafu nasikia ziko sokoni ukavae kisha kakeshe kwenye mwenge.
 
Mkuu VUTA-NKUVUTE unasahau kwamba:

1) Kampeni siyo za Urais tu, kuna Wabunge na Madiwani. Wote hao wanahitaji fedha kumudu kampeni. Je, chama kilijipangaje mapema, maana muda wa Uchaguzi Mkuu hujulikana?

2) Viongozi wa CHADEMA, na kwenye kampeni zinazoendelea, Lissu mgombea Urais amesikika akidai CCM imeharibu uchumi watu wamekuwa masikini kuliko awamu zilizopita. Hao wanaombwa kuchangia CHADEMA wana uwezo gani au ndio mpango wa kuwafanya masikini ili hayo madai yawe kweli?

3) CHADEMA, kama chama kikuu, kilikuwa kinapata mabilioni ya ruzuku. Isitoshe wabunge nao wamechangia kila mwezi na kufikisha mabilioni. Je, hii fedha imetumikaje maana hata ofisi, japo moja ya chama, haijajengwa.

Hiki ndio chama cha kuomba kuchangiwa gharama za kampeni?
Hivi ukiwa CCM unakua MPUUZI kiasi hiki? Kuwa masikini haimaanishi mtu atashindwa kuchangia hata 100 au 500 Mkuu.
 
Attachments

  • Lumumba Buku 7.jpg
    Lumumba Buku 7.jpg
    20.8 KB · Views: 1
Mnasema hatupo kwenye uchumi wa Kati.

Wananchi ni maskini,

Halafu mnatembeza bakuli kwa maskini.
Ungependa kuona Tanzania ambayo wabunge wote, madiwani wote na raisi wawe ni ccm?
 
Jibu swali langu la kwanza. Mimi namnukuu Lissu anadai wananchi wapo hoi kwa miaka mitano,kwa nini anawachangisha?
Hajawapa kiwango cha kuchangia. Kila mwenyekupenda mabadiliko achangie kwa kadiri ya uwezo wake. Hata ww mwenyewe umewachangia indirect. Uliponunua bandle ili uweze kuingia humu JF, yule aliyekuuzia kapata faida kidogo nae akachingia CHADEMA direct.
 
Mkuu VUTA-NKUVUTE unasahau kwamba:

1) Kampeni siyo za Urais tu, kuna Wabunge na Madiwani. Wote hao wanahitaji fedha kumudu kampeni. Je, chama kilijipangaje mapema, maana muda wa Uchaguzi Mkuu hujulikana?

2) Viongozi wa CHADEMA, na kwenye kampeni zinazoendelea, Lissu mgombea Urais amesikika akidai CCM imeharibu uchumi watu wamekuwa masikini kuliko awamu zilizopita. Hao wanaombwa kuchangia CHADEMA wana uwezo gani au ndio mpango wa kuwafanya masikini ili hayo madai yawe kweli?

3) CHADEMA, kama chama kikuu, kilikuwa kinapata mabilioni ya ruzuku. Isitoshe wabunge nao wamechangia kila mwezi na kufikisha mabilioni. Je, hii fedha imetumikaje maana hata ofisi, japo moja ya chama, haijajengwa.

Hiki ndio chama cha kuomba kuchangiwa gharama za kampeni?

Inawauma sana kuona mbinu zenu za kuzimu zinashindwa. Wanasaikolojia walishaliona hili mapema: "where your treasure is there your heart will be also"

Watu wakikuchangia hata senti moja, ujue kura yao unayo pia. Watanzania na umasikini wao wanataka ukombozi. Wanaichukia mno CCM kiasi cha kuchangia chochote toka kwenye umasikini wao waliolazimishwa na CCM kwa maiak yote hii.

Tundu Lissu ni aina nyingine ya mwanasiasa, na Si size ya Jiwe. Wanaomlinganisha na Lowassa 2015 ni mfano mzuri wa wanaCCM wengi waliorigwa kiakili.
 
Kwa kuwa hupendi kuhoji maovu yahusuyo CHADEMA, ficheni ugonjwa mauti itawaumbua
 
Back
Top Bottom