Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Mimi siwezi kuwachangia ni hiyari yangu silazimishwi na wanaochangia ni hiyari yao hawalazimishwi!

Wanachanga kwa utashi wao wenyewe!

Unakelwa na nini Mkuu!?
Anayekereka hapa ni wewe mkuu maana sijui unakereka nini Mimi kutoa maoni.
 
Poa...ntachangia sana. Kwa kweli kupigwa risasi kwake mchana saa saba kumenifanya nimwonee huruma na hapohapo kanyimwa matibabu na ujira wake pia kanyang'anywa.
Kweli wewe ni nyumbu, tunazungumzia mchango wa pesa za kampeni sio hizo zakindugu.
 
Sitaki niwachoshe kwa meneno mengi. Nawaambieni tu kwa kifupi na kwa uhakika. Bakuli la michango analolitembeza mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu si la kubezwa au kumezwa. Yaweza kuwa ni kwa kujua au kutokujua, Lissu anaruka kikwazo kikuu kilichosukwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu: ukata kwa vyama vya upinzani. Ukata tata ungewakata na kuwavuta wapinzani nyuma na kuwafanya washindwe kufanya kampeni.

Mipango kabambe ilishasukwa kitambo kuvifanya vyama vya upinzani mwaka huu kuandamwa na ukata wa kifedha. CCM yetu yenyewe, kwakuwa ina rasilimali za kutosha na kutisha na kwakuwa imejibanza kwenye koti la Serikali, ilijiandaa kujidai itakavyo kwenye kampeni hizi huku wapinzani wakishindwa kufanya kampeni. Mipango ilisukwa vyema. Kampeni zina gharama nyingi: usafiri, malazi,mavazi, chakula, vifaa vya sauti, majukwaa na kadhalika.

Mipango ya kuufanya ukata umee kwenye vyama vya upinzani ilianza miaka kadhaa iliyopita. Karibu kila chama kikubwa cha upinzani hapa nchini vikiwemo CHADEMA, ACT na NCCR-Mageuzi kina chama au vyama rafiki nje ya Tanzania. Marafiki hao wa nje husaidia vyama hivyo kifedha hasa kwenye harakati kama hizi za kiuchaguzi. Na hakukuwa na ubaya kuhusu kusaidiana huko. Lakini, mwaka huu misaada hiyo imepigwa pini. Imezibwa. Hakuna misaada tena. Ukata!

Lissu ajaziwe bakuli lake. Achangiwe. Hata mimi, kama mfuasi ninayejinafasi wa demokrasia ya vyama vingi, nimeshamchangia Lissu. Lazima tuwe na mgombea strong wa upinzani ili kutufanya tuchague vyema. Lazima mwaka huu mchuano mkali uwe kati ya Dkt. Magufuli na Lissu. Lazima tusikie sera za kila mmoja wao na tuamue. Bakuli la Lissu, hata kama litakejeliwa na kudhihakiwa, lina maana kubwa: linaruka mipango ya kidhalimu ya kutengeneza ukata kwa wapinzani.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kigoma, Tanzania)
Tulioliona hilo tuaendelea kuchangia bakuli. Himahima wapenda demokrasia; tusichoke kuchangia mpaka kieleweke.
 
Ilikuwa kwa ajiri ya kuimarisha chama ndiyo maana wamweza kuwa na mtandao nchi nzima hata baada ya kukaa mika mitano bila kuruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa.
Hicho chama kimeimarishwa wapi? Mkoa gani, wilaya gani au kata gani? Mbona mnakuwa waongo hivi mnapata faida gani?
 
Mbowe hata tukichanga yee anakura ela tu. Ndo maana mimi niriachaga kuchanga

Sura yako uloiweka kwenye profile ni nzuri wala haiendani na matamshi ya kishamba yanayotoka kwenye kinywa cha mtoto mwenye sura nzuri hivyo eti
"anakura =anakula"
"Nirichanga=nilichanga". Nilijua uko vizuri upstairs kumbe kichwa chenyewe ndo kinatapika errors hivyo?hufai hata kuolewa!![emoji16][emoji16]
 
kuchanga ni hiari sio lazima,pili chadema ni chama kilichoenea nchi nzima kina watumishi waajiriwa wa cha ukiacha gharama za uchaguzi pia kuna gharama za kukiendesha hiki chama kilicho fanyika ni kuwadhibiti watu wote na njia zingine zote ili vife kifo cha kawaida,UKATA, lakini cha ajabu watu wanajitolea kwa kila namna vyama vya upinzani visife,ole wetu tukubari CCM aviuwe vyama hivi tumekwisha Tanzania kama sasa ni hivi je CCM akibaki peke yake atatutenda yapi!
Jibu kwanza, nimekuuliza bajeti ya uchaguzi ya Chama ni kiasi gani?
Walikusanya kiasi gani kutokana na ruzuku pamoja na michango yawabunge?
Maana michango yawabunge tuliambiwa ni kwaajili ya uchaguzi. Hadi leo zipo ngapi?
 
Mnasema hatupo kwenye uchumi wa Kati.

Wananchi ni maskini,

Halafu mnatembeza bakuli kwa maskini.
kwa hiyo masikini huwa hawachangiani kwenye mambo yao? yaani wewe ni pimbi sijawahi kuona
 
Jibu kwanza, nimekuuliza bajeti ya uchaguzi ya Chama ni kiasi gani?
Walikusanya kiasi gani kutokana na ruzuku pamoja na michango yawabunge?
Maana michango yawabunge tuliambiwa ni kwaajili ya uchaguzi. Hadi leo zipo ngapi?
wewe na mimi ni makatibu wakuu wa vyama vya siasa maana nina uhakika hata wewe hujui jibu sahihi hata kama nitakudanganya kwa hiyo jitahidi kuuliza maswali yanayoweza kujibiwa na mtu wa kawaida,
 
kwa hiyo masikini huwa hawachangiani kwenye mambo yao? yaani wewe ni pimbi sijawahi kuona
Huu ni wizi,

Chadema sio maskini bali kuna ufujaji wa fedha za kuendeshea Chama,

Kuna Ruzuku na michango ya wabunge iko wapi??
 
Sitaki niwachoshe kwa meneno mengi. Nawaambieni tu kwa kifupi na kwa uhakika. Bakuli la michango analolitembeza mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu si la kubezwa au kumezwa. Yaweza kuwa ni kwa kujua au kutokujua, Lissu anaruka kikwazo kikuu kilichosukwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu: ukata kwa vyama vya upinzani. Ukata tata ungewakata na kuwavuta wapinzani nyuma na kuwafanya washindwe kufanya kampeni.

Mipango kabambe ilishasukwa kitambo kuvifanya vyama vya upinzani mwaka huu kuandamwa na ukata wa kifedha. CCM yetu yenyewe, kwakuwa ina rasilimali za kutosha na kutisha na kwakuwa imejibanza kwenye koti la Serikali, ilijiandaa kujidai itakavyo kwenye kampeni hizi huku wapinzani wakishindwa kufanya kampeni. Mipango ilisukwa vyema. Kampeni zina gharama nyingi: usafiri, malazi,mavazi, chakula, vifaa vya sauti, majukwaa na kadhalika.

Mipango ya kuufanya ukata umee kwenye vyama vya upinzani ilianza miaka kadhaa iliyopita. Karibu kila chama kikubwa cha upinzani hapa nchini vikiwemo CHADEMA, ACT na NCCR-Mageuzi kina chama au vyama rafiki nje ya Tanzania. Marafiki hao wa nje husaidia vyama hivyo kifedha hasa kwenye harakati kama hizi za kiuchaguzi. Na hakukuwa na ubaya kuhusu kusaidiana huko. Lakini, mwaka huu misaada hiyo imepigwa pini. Imezibwa. Hakuna misaada tena. Ukata!

Lissu ajaziwe bakuli lake. Achangiwe. Hata mimi, kama mfuasi ninayejinafasi wa demokrasia ya vyama vingi, nimeshamchangia Lissu. Lazima tuwe na mgombea strong wa upinzani ili kutufanya tuchague vyema. Lazima mwaka huu mchuano mkali uwe kati ya Dkt. Magufuli na Lissu. Lazima tusikie sera za kila mmoja wao na tuamue. Bakuli la Lissu, hata kama litakejeliwa na kudhihakiwa, lina maana kubwa: linaruka mipango ya kidhalimu ya kutengeneza ukata kwa wapinzani.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kigoma, Tanzania)
Chadema siyo wa kuhurumiwa hapo unatetea wapigaji, mahesabu yaliwekwa hadharani na wabunge wao kuwa walikuwa wanakatwa 1.5mil kila mwezi, kwa miaka 5 ziko wapi pesa.Mpango wa kuwakata wabunge hata ccm upo na fedha za ccm zilikuwa kwenye fixed deposit. Sasa leo ccm wakifanya kampeni za kitajiri mnalalamika nini? Wafuasi wa chadema hawana ubavu kuhoji kazi yao ni kufia chama hata kama wizi umetamalaki ndani ya chama.Kampeni ya siku 60 kwa wagombea takribani 350 wabunge na 50,000 madiwani siyo mchezo.Chadema siyo wa kupewa nchi wataifilisi na hawatataka kuhojiwa.
 
mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe. popote duniani mabadiliko huletwa na tabaka la chini.mwaka huu maskini wa Tanzania wameamua.
Wameamua kutembea na Magufuli siyo nyie viwavi jeshi msiotaka kusikia harufu ya pesa
 
Chama pekee Tanzania ambacho kinapata billion plus kwenye ruzuku ni ccm

Kwa taarifa yako chadema hata Milion Mia mbili za ruzuku haifiki kwa mwez
Hata kidogo hicho kionekane kimefanya jambo lenye utaifa. Je, vyama visivyo na ruzuku?
 
wewe na mimi ni makatibu wakuu wa vyama vya siasa maana nina uhakika hata wewe hujui jibu sahihi hata kama nitakudanganya kwa hiyo jitahidi kuuliza maswali yanayoweza kujibiwa na mtu wa kawaida,
Acha uzwazwa. Chama ni taasisi sio mali ya mtu binafsi, mapato na matumizi lazima yawe wazi.
 
Kama huelewi nyamaza, gharama za uchaguzi unajua ni kiasi gani? Na chama tawala unajua vyanzo vyake vya pesa?
wewe ndo huelewei nyumbu mkubwa wewe. hivi toka Chadema wameanza kupokea ruzuku 2016 mpaka leo ni takribani bilioni 40. wamezifanyia nini? hawajajenga hata ofisi za wilaya. bado kuna michango ya wabunge walikua wanachukua kila mwezi viti maalum mil.2 na wabunge wa majimbo mil 1.5. fedha hizi zote walishindwa kutenga fedha za kugharamia uchaguzi? waache kuwatapeli watanzania
 
azima tuwe na mgombea strong wa upinzani ili kutufanya tuchague vyema. Lazima mwaka huu mchuano mkali uwe kati ya Dkt. Magufuli na Lissu. Lazima tusikie sera za kila mmoja wao na tuamue.
Ni kweli kabisa. Lazima tuwe na mpinzani imara mmoja atakayemenyana vilivyo na mgombea urais wa ccm. Hapo ndipo tutaona uchaguzi mtamu mwaka huu
 
Back
Top Bottom