Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Kwa hiyo CCM ndo iliwambia wale pesa za ruzuku?
Mzee tupa sina uhakika kama una mapenzi kwa CCM, sema wewe ni kamanda, maana mada zako zinaonyesha kitambo sana.
 
Endelea kuteseka mkuu. Kachemsha CAG, kachemsha Director wa Taa Kuu Kuu Tu, utaweza wewe uliye nyuma ya keyboard ya Itel?
Mimi nateseka nini? Anateseka mgombea wenu,mara aanguke jukwaani,mara achangishe pesa. Kwa nini asitulie maana hata kura laki mbili hapati.
 
Wacha ajilipe na kuchanga tutachanga.Wako wanaotumbua kodi za wananchi miaka zaidi ya 50 ukiwaona wameshiba kweli kweli na nchi iko vile vile mbona hatusemi.
Yaleyale ya makamanda wasiotumia akili. Ruzuku inatolewa kwa mujibu wa sheria. Ruzuku alikuwa anajilipa mwenyekiti wetu,sema nyie wenzangu mnaogopa kusema ukweli.
 
Mnasema hatupo kwenye uchumi wa Kati.

Wananchi ni maskini,

Halafu mnatembeza bakuli kwa maskini.
Mimi siwezi kuwachangia ni hiyari yangu silazimishwi na wanaochangia ni hiyari yao hawalazimishwi!

Wanachanga kwa utashi wao wenyewe!

Unakelwa na nini Mkuu!?
 
Tunaendelea kuchanga mkuu na hatutachoka mpaka tuikomboe nchi kutoka kwa beberu na dukteta ccm
 
Nilishachanga Laki moja ngoja nikaongeze na hii elfu kumi niliyotaka kunywa Supu muda huu. Najua kwa siku moja sifi njaa.
 
Kwani ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi? Wananchi wana hali mbaya kwa nini muwachangishe?
Wana wa nchi wametoa wapi hiyo hali mbaya awamu hii ya tano, magufuli ametokomeza umaskini Tanzania, yahani wa tz ni matajiri hakuna mfanowe, acha wachangie demokrasia nchini mwao iweze kunawiri na kistawi, ebo!
 
Sio kila jambo utake liandikwe uku kwenye mitandao.We kaa ukijua mambo ni mengi,sio hadi tuiponze Jamii forum ndo ujue mambo ni mengi.watu wanakaa kimya tu.
Ndio haya ambayo yanakitia aibu Cdm. Pesa gani za mifuko ya jamii ambazo Ccm imezichota? Tumia akili kwa manufaa ya Cdm

Zamani serikali ilikuwa inakopa na ilikuwa inachelewa kulipa hiyo mifuko ya jamii. Mimi na Dk Slaa tunajua kwa undani.
 
Obama wa Marekan 200i alichangisha pesa kwa ajili ya kampeni wanashangaa hawa utopolo wa Tandale
 
Maelezo ya point number mbili yamedhihirisha ulivyo sawa na ulichokiandika.
 
Naunga mkono hoja zote
 
Kwani ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi? Wananchi wana hali mbaya kwa nini muwachangishe?
Kumbe hata CCM mnajua kua mmewatia umasikini wananchi?.
Kila mabadiliko yanahitaji gharama, hivyo sio mbaya kwa mwananchi kuchangia kwa aliyenacho, kama hana alazimishwi kuna njia nyingine ya kuchangia kiifikia ahadi ya maendeleo ya kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…