Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Porojo tupu, kwani hawakupewa ruzuku kwa ajili ya kampeni? Kila mtanzania anajua jinsi hii saccos ilivyo na matumizi mabovu ya rasilimali fedha. Wanaofaidi ni hao top layers tu wengine ndio imekula kwao mazima.
CAG huwa anakagua na hakuna hicho ulichokitaja hapa!
Muulizeni mashinji ambaye yuko huko kwenu na ndiye aliyekuwa anasaini fedha za chama awape siri!Ukiona kimya mjue hizo ni propaganda!
 
Kumbe hata CCM mnajua kua mmewatia umasikini wananchi?.
Kila mabadiliko yanahitaji gharama, hivyo sio mbaya kwa mwananchi kuchangia kwa aliyenacho, kama hana alazimishwi kuna njia nyingine ya kuchangia kiifikia ahadi ya maendeleo ya kweli
Na ile michango ya wabunge ipo wapi hadi mchangishe watu?
 
Mkuu VUTA-NKUVUTE unasahau kwamba:

1) Kampeni siyo za Urais tu, kuna Wabunge na Madiwani. Wote hao wanahitaji fedha kumudu kampeni. Je, chama kilijipangaje mapema, maana muda wa Uchaguzi Mkuu hujulikana?

2) Viongozi wa CHADEMA, na kwenye kampeni zinazoendelea, Lissu mgombea Urais amesikika akidai CCM imeharibu uchumi watu wamekuwa masikini kuliko awamu zilizopita. Hao wanaombwa kuchangia CHADEMA wana uwezo gani au ndio mpango wa kuwafanya masikini ili hayo madai yawe kweli?

3) CHADEMA, kama chama kikuu, kilikuwa kinapata mabilioni ya ruzuku. Isitoshe wabunge nao wamechangia kila mwezi na kufikisha mabilioni. Je, hii fedha imetumikaje maana hata ofisi, japo moja ya chama, haijajengwa.

Hiki ndio chama cha kuomba kuchangiwa gharama za kampeni?
Hawa ni wahuni mkuu, wanadai wananchi wana halimbaya kiuchumi hapohapo wanawachangisha pesa sijui wanatuonaje Hawa watu.
 
Sisi wapenda Uhuru na demokrasia tumeshachanga na tutachangia tena
Mbona alipotoka Zanzibar ndugu Lissu aliongea na wanahabari, alilalamika hali ni mbaya sana kifedha? Kama mnachanga kweli hali ingekuwa hivyo?
 
Kwani ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi? Wananchi wana hali mbaya kwa nini muwachangishe?
Hiyo hali mbaya ya wananchi imeletwa na nani? CHADEMA au CCM inayokusanya Kodi! Iliyotawala miaka 60 sasa?
 
Kwani ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi? Wananchi wana hali mbaya kwa nini muwachangishe?
Muulize MEKO wenu ile RAMBIRAMBI ya WANA KAGERA ameifukia wapiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii?????????????
 
Hiyo hali mbaya ya wananchi imeletwa na nani? CHADEMA au CCM inayokusanya Kodi! Iliyotawala miaka 60 sasa?
Mgombea wenu anazunguka anasema wananchi wana hali mbaya. Sasa kwa nini anawachangisha hata pesa?
 
Sitaki niwachoshe kwa meneno mengi. Nawaambieni tu kwa kifupi na kwa uhakika. Bakuli la michango analolitembeza mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu si la kubezwa au kumezwa. Yaweza kuwa ni kwa kujua au kutokujua, Lissu anaruka kikwazo kikuu kilichosukwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu: ukata kwa vyama vya upinzani. Ukata tata ungewakata na kuwavuta wapinzani nyuma na kuwafanya washindwe kufanya kampeni.

Mipango kabambe ilishasukwa kitambo kuvifanya vyama vya upinzani mwaka huu kuandamwa na ukata wa kifedha. CCM yetu yenyewe, kwakuwa ina rasilimali za kutosha na kutisha na kwakuwa imejibanza kwenye koti la Serikali, ilijiandaa kujidai itakavyo kwenye kampeni hizi huku wapinzani wakishindwa kufanya kampeni. Mipango ilisukwa vyema. Kampeni zina gharama nyingi: usafiri, malazi,mavazi, chakula, vifaa vya sauti, majukwaa na kadhalika.

Mipango ya kuufanya ukata umee kwenye vyama vya upinzani ilianza miaka kadhaa iliyopita. Karibu kila chama kikubwa cha upinzani hapa nchini vikiwemo CHADEMA, ACT na NCCR-Mageuzi kina chama au vyama rafiki nje ya Tanzania. Marafiki hao wa nje husaidia vyama hivyo kifedha hasa kwenye harakati kama hizi za kiuchaguzi. Na hakukuwa na ubaya kuhusu kusaidiana huko. Lakini, mwaka huu misaada hiyo imepigwa pini. Imezibwa. Hakuna misaada tena. Ukata!

Lissu ajaziwe bakuli lake. Achangiwe. Hata mimi, kama mfuasi ninayejinafasi wa demokrasia ya vyama vingi, nimeshamchangia Lissu. Lazima tuwe na mgombea strong wa upinzani ili kutufanya tuchague vyema. Lazima mwaka huu mchuano mkali uwe kati ya Dkt. Magufuli na Lissu. Lazima tusikie sera za kila mmoja wao na tuamue. Bakuli la Lissu, hata kama litakejeliwa na kudhihakiwa, lina maana kubwa: linaruka mipango ya kidhalimu ya kutengeneza ukata kwa wapinzani.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kigoma, Tanzania)

[/QUOTE
Naomba namba nitume 10 hapa shwain hawa ccm
 
... TUONDOE WATAWALA WANAOFUGA UMASIKINI NA UNYONGE WETU ILI WAENDELEE KUTUTAWALA!
🤮🤮🤮🤮
 
Nimekusoma najaribu kukuelewa na "nondo" zako ila sikuelewi.

1. Matumizi ya ruzuku ya Chadema ni kwaajili ya mambo mengi, kuna kulipa mishahara ya wafanyakazi, na mambo mengine ya uendeshaji chama, zaidi unaambiwa ruzuku imekatwa na serikali ya Magufuli, na hata kama ingekuwepo, Chadema wanapata milioni 200 na kitu kwa mwezi, hizo hazitoshi kugawa kwa matumizi ya chama mikoa yote Tz Bara, nakushangaa sijui kitu gani hiki ulichokiandika.

2. Pointi yako namba mbili ndio inazidi kuonesha ulivyo kilaza, sasa kama Chadema inachangiwa na masikini wewe shida yako ni ipi? umeambiwa wale marafiki wao wa nje wamebanwa wasiwachangie na serikali ya Magufuli, sasa wewe ulitaka wachangiwe na nani? kwanini unawadharau watanzania na hali zao mbaya kiuchumi zilizosababishwa na sera mbovu kuwekeza kwenye vitu badala ya watu? hujui hizo mia mia za hao masikini zikijumlishwa kitapatikana kikubwa!.

3. Pointi yako namba tatu nimeshaijibu kwenye namba moja, rudi juu kaisome tena.
Nalazimika tu kujibu ingawa umenijibu kishabiki kuliko kiuchambuzi.

Hata vile nijibu kwa ujumla kuwa uwe mkweli na jasiri kuwauliza viongozi wa CHADEMA matumizi ya fedha za chama (ruzuku, michango ya wabunge, ada za wanachama, misaada ya vyama rafiki vya nje, nk}.

Kuna tuhuma dhidi ya Mbowe zilizotolewa na viongozi waandamizi waliokihama chama, hazijajibiwa hadi muda huu. Labda una majibu tofauti na madai yako kuwa zimetumika kwa shughuli za chama. Au ndiyo hayo ya tuhuma? Km inadaiwa kuwa watumishi wengi wa chama hawalipwi mishahara/posho.

Uchaguzi Mkuu 2015, CHADEMA kilikuwa kimejiandaa kifedha kwa kampeni ikiwa ni pamoja na mabango, TShirt, chopa, nk. Iweje leo kishindwe kumudu gharama za kampeni huku kina vyanzo vya uhakika {ruzuku + michango ya wabunge)?

Kuna vyama vingi tu vinashiriki Uchaguzi Mkuu huu visivyokuwa na ruzuku wala mapato kama CHADEMA, havitembezi bakuli.

Nashauri wafuasi wa CHADEMA, humu JF, waache unafiki kama wana nia nzuri ya kutaka kiwe Chama Tawala, ili isije baadaye kunung'unika kuwa hawakujua. Kuna ushahidi usio na mashaka kuwa CHADEMA hakiendeshwi kama chama cha siasa. Dai hili linakinyima uhalali wa kupewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi.

Bila kumung'unya maneno, naomba kwa Mwenyezi Mungu awajaze ujasiri Watanzania kukiadhibu vibaya sana CHADEMA kwenye sanduku la kura ili viongozi wake warudi mezani kujenga chama upya kama chama cha siasa.
 
Back
Top Bottom