Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Uchaguzi 2020 Nawamegea siri: 'Bakuli la Lissu' lijazwe michango, linasaidia kuruka kiunzi kikuu mwaka huu

Kama waliweza dhibiti media ili kuuwa coverage ya upinzani na bado coverage imekuwa kubwa nini Sasa wanaweza zuia.
Huwezi ukafanikisha mind control zama hizi Ni kuupiga ngumi ukuta
 
Kwani ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi? Wananchi wana hali mbaya kwa nini muwachangishe?
Wananchi wa wapi wana hali mbaga comrade?? Akisikia mr President hii statement yako kitakukuta kitu.. sisi ni tajiri
 
.....ninayejinafasi wa demokrasia ya vyama vingi, nimeshamchangia....
Naipenda Tanzania kwa 'ukubwa' wake!

Katu Tanzania haitakuja kuathiriwa na wale wanaoinenea mabaya Tanzania, bali hizo ni changamoto za kuimarisha Tanzania. Yaani naiona Tanzania Imara kabisa ulimwenguni katika nyanja zote za kimaendeleo siku si nyingi.

Kwa kifupi, hatuko tayari 'kuuzwa kwa mafungu' kama Mgombea urais wa chama cha Mbowe anavyojinasibu. Bila aibu anasema wazi kabisa kuwa Tanzania siyo lazima kuwepo siku za usoni! Hiyo kwa lugha rahisi ni kuwa ameishafika makubaliano na 'wanunuzi' kutuuza!

Mkuu, VUTA-NKUVUTE mmeyataka wenyewe, tusilaumiane!
 
Lissu anasema wananchi ni masikini, harafu masikini hao hao anawaomba michango, huu ni unyama wa hali ya juu sana.
 
Sitaki niwachoshe kwa meneno mengi. Nawaambieni tu kwa kifupi na kwa uhakika. Bakuli la michango analolitembeza mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu si la kubezwa au kumezwa. Yaweza kuwa ni kwa kujua au kutokujua, Lissu anaruka kikwazo kikuu kilichosukwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu: ukata kwa vyama vya upinzani. Ukata tata ungewakata na kuwavuta wapinzani nyuma na kuwafanya washindwe kufanya kampeni.

Mipango kabambe ilishasukwa kitambo kuvifanya vyama vya upinzani mwaka huu kuandamwa na ukata wa kifedha. CCM yetu yenyewe, kwakuwa ina rasilimali za kutosha na kutisha na kwakuwa imejibanza kwenye koti la Serikali, ilijiandaa kujidai itakavyo kwenye kampeni hizi huku wapinzani wakishindwa kufanya kampeni. Mipango ilisukwa vyema. Kampeni zina gharama nyingi: usafiri, malazi,mavazi, chakula, vifaa vya sauti, majukwaa na kadhalika.

Mipango ya kuufanya ukata umee kwenye vyama vya upinzani ilianza miaka kadhaa iliyopita. Karibu kila chama kikubwa cha upinzani hapa nchini vikiwemo CHADEMA, ACT na NCCR-Mageuzi kina chama au vyama rafiki nje ya Tanzania. Marafiki hao wa nje husaidia vyama hivyo kifedha hasa kwenye harakati kama hizi za kiuchaguzi. Na hakukuwa na ubaya kuhusu kusaidiana huko. Lakini, mwaka huu misaada hiyo imepigwa pini. Imezibwa. Hakuna misaada tena. Ukata!

Lissu ajaziwe bakuli lake. Achangiwe. Hata mimi, kama mfuasi ninayejinafasi wa demokrasia ya vyama vingi, nimeshamchangia Lissu. Lazima tuwe na mgombea strong wa upinzani ili kutufanya tuchague vyema. Lazima mwaka huu mchuano mkali uwe kati ya Dkt. Magufuli na Lissu. Lazima tusikie sera za kila mmoja wao na tuamue. Bakuli la Lissu, hata kama litakejeliwa na kudhihakiwa, lina maana kubwa: linaruka mipango ya kidhalimu ya kutengeneza ukata kwa wapinzani.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kigoma, Tanzania)
Kwa mara ya kwanza tangu 2015 ndio nakuunga mkono. Hasa hapo kwenye kuchagua vyema.
Twende na JPM atatuvusha.
 
Lissu anasema wananchi ni masikini, harafu masikini hao hao anawaomba michango, huu ni unyama wa hali ya juu sana.
Kweli tu masikini wengi wetu lakini unapima faida ya kuchangia na gharama ya kuchangia, kama faida ni kubwa basi twende. Kuchangia hata jero, buku etc inatosha. It is a game of numbers.
 
Lissu anasema wananchi ni masikini, harafu masikini hao hao anawaomba michango, huu ni unyama wa hali ya juu sana.
hivi jaman Lisu ni lini unakuja Arusha?
sisi wananchi michango yetu inatuwasha tunataka tumchangie Rais wetu mtarajiwa Lissu ali tutegue mtego wa hila za maccm yamemzibia vyanzo vyote vya mapato
 
Kuna mtu aliniambia ukiona mwanamke ana sura nzuri, ujue kichwani hamna kitu, kama vile naanza kumuamini, kweli Mungu hakupi vyote.
Mkuu,nani sasa mwenye sura nzuri hapo?
Usidanganyike na hiyo picha,si yeye huyo.
 
Nilimshangaa Magu kubeza michango ya kusaidia kampeni..hajui hata vyama vikubwa vya Marekani wanafanya fund raising...jana Lissu kamjibu Sumbawanga kamwambi yeye Lissu sio mwizi na wala hapigi deal..
 
Kwani ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi? Wananchi wana hali mbaya kwa nini muwachangishe?
Wananchi wapi wenye hali mbaya, hawa wa Tz ya uchumi wa kati?!

Meko alisema asisikie mtu anasema vyuma 'vimekaza' au nawe umeanza uchochezi tukushughulikie?
 
Mkuu VUTA-NKUVUTE unasahau kwamba:

1) Kampeni siyo za Urais tu, kuna Wabunge na Madiwani. Wote hao wanahitaji fedha kumudu kampeni. Je, chama kilijipangaje mapema, maana muda wa Uchaguzi Mkuu hujulikana?

2) Viongozi wa CHADEMA, na kwenye kampeni zinazoendelea, Lissu mgombea Urais amesikika akidai CCM imeharibu uchumi watu wamekuwa masikini kuliko awamu zilizopita. Hao wanaombwa kuchangia CHADEMA wana uwezo gani au ndio mpango wa kuwafanya masikini ili hayo madai yawe kweli?

3) CHADEMA, kama chama kikuu, kilikuwa kinapata mabilioni ya ruzuku. Isitoshe wabunge nao wamechangia kila mwezi na kufikisha mabilioni. Je, hii fedha imetumikaje maana hata ofisi, japo moja ya chama, haijajengwa.

Hiki ndio chama cha kuomba kuchangiwa gharama za kampeni?
Unafahamu kama ccm pamoja na umri wake na rasilimali kilizo jimilikisha bado kinachangiwa tena kwa 'kuwalazimisha' wachangiaji ambao hata sio wanachama/wapenzi wala wafuasi wake?
 
Nimemegewa Siri ruzuku ya vyama ilikatwa tangu January kwa kisingizio tunajenga Flyover 🔧
Hiyo siri uliyomegewa na kama umeiamini basi wewe ni kilaza wa mwisho. Yaani chadema wakatwe ruzuku halafu iwe siri?? Unawajua wachaga au unawasikia tu?
 
Hiyo siri uliyomegewa na kama umeiamini basi wewe ni kilaza wa mwisho. Yaani chadema wakatwe ruzuku halafu iwe siri?? Unawajua wachaga au unawasikia tu?

Wewe kweli mpumbavu ruzuku zimepigwa pini uliza credible sources utaambiwa.
 
Kwa hiyo unadanganya watu ili iweje? Kama Chadema ingekuwa inapeleka pesa wilaya zote Tanzania kungekuwa na hali kama hii?
Ofisi nyingi katika wilaya zimefungwa, au unajifanya hujui?
Ruzuku ilikuwa mil 360, deni la mbowe mil 100. Mil 50 anajilipa yeye. Sasa hapo za kulipa watu wilayani zingetoka wapi?

Changisheni wapuuzi wenzenu.
Wewe umechangishwa?? Mnachota PESA za Kodi zetu kulazimisha kupendwa. Poor CCM
 
Back
Top Bottom