Nawatazama hawa Wanawake waliofanikiwa kimaisha Clouds Tv, ila Shuhuda zao za Mafanikio hazinishawishi

Nawatazama hawa Wanawake waliofanikiwa kimaisha Clouds Tv, ila Shuhuda zao za Mafanikio hazinishawishi

Wanaume mmekuwa very unafair kwenye hii thread..hivi kweli hakuna wanawake wanaopambana wenyewe bila nguvu ya wanaume? Au ndio ile notion ya mwanaume akipandishwa cheo ni kwa sababu ya uchapakazi ila mwanamke ni kwa sababu mwili wake? Ni watoto wangapi Tanzania hii kwa mfano tu waliolelewa na wazazi wa kike pekee mpaka wakaweza kujisimamia wenyewe. Humu JF kwenyewe mmejaa kibao. Leo mnakuja with such negative opinions. Acheni hizo. Hata kama wapo waliopitia njia hizo, hamuwezi kuja with such generalizations....
 
Mkuu unaweza kuwa ni mtizamo wako binafsi
Ila mimi pia ni mmoja wa hao walioanza na mtaji mdogo sana
Na unaendelea kukua.
Sijui ni kwa nini uone ni fake story!

Labda ungesema backups na changamoto za kurudisha mtu chini hazikosekani.
Msingi wa hoja hii ni kwa baadhi ambao sio wa kweli............ lakini tunajua wapo ambao wanaanza kwa mtaji mdogo bila kumtegemea mtu
 
kanisani pia nakukatalia, huwa nastaajabu shuhuda za kwa mzee wa upaka, mwanamke anasema, "mwaka jana sikua na gari, baada ya kuanza kuja kanisani na kupata upako, sa ivi nina gari langu, lipo hapo nje"
Sasa unajiuliza kwanini huwa hawaelezee walifanyaje, hupati jibu.
Hao nao ni watu wa fix tu
 
Wanaume mmekuwa very unafair kwenye hii thread..hivi kweli hakuna wanawake wanaopambana wenyewe bila nguvu ya wanaume? Au ndio ile notion ya mwanaume akipandishwa cheo ni kwa sababu ya uchapakazi ila mwanamke ni kwa sababu mwili wake? Ni watoto wangapi Tanzania hii kwa mfano tu waliolelewa na wazazi wa kike pekee mpaka wakaweza kujisimamia wenyewe. Humu JF kwenyewe mmejaa kibao. Leo mnakuja with such negative opinions. Acheni hizo. Hata kama wapo waliopitia njia hizo, hamuwezi kuja with such generalizations....
Umesahau jf ni ya matajiri
 
Halafu wanavyojitahidi kutudanganya wanadhani Watu wote tunaowaangalia ni ' Wapuuzi ' huku wakisahau kuwa kuna wengine wapo hapo ' Upuuzi ' wao wa kuharibu na kuingilia ' Ndoa ' za Watu ili tu nao waweze ' Kuwachuna ' na ' Kuwatumia ' hao Wanaume wenye Mamlaka na Nyadhifa unajulikana na Sisi Watoto wa Mjini. Wanadhani wametuweza lakini kumbe ndiyo tumezidi kuwadharau tu! Kweli jamani kuna Watu mishipa yao ya aibu imekatika kabisa hapa duniani. Yaani unajitutumua kabisa kutoa ' Shuhuda ' katika Television wakati moyoni mwako unajua kabisa kuwa umewezeshwa ' Kibaiolojia ' tena na Waume za Watu hata aibu huna!
Kiukweli ukitafuta mwanamke ambaye kafanikiwa bila ya kutenda dhambi ya kuvuliwa nguo ya ndani ili kupata pesa, mali, cheo,elimu ama ushawishi katika jamii nadhani hawafiki kumi katika mia.

Wengi wamefika hapo walipo kwa mtaji wa kuvuliwa nguo ya ndani ambapo mwili ulihusika sana katika hatua fulani za harakati za kutafuta.
 
kanisani pia nakukatalia, huwa nastaajabu shuhuda za kwa mzee wa upaka, mwanamke anasema, "mwaka jana sikua na gari, baada ya kuanza kuja kanisani na kupata upako, sa ivi nina gari langu, lipo hapo nje"
Sasa unajiuliza kwanini huwa hawaelezee walifanyaje, hupati jibu.
Wauzaji hao wanatoa ushuhuda wa uwongo,mafanikio huletwa na juhudi zako mwenyewe....mzee wa upako nae mlevi tu anatupia konyagi balaa
 
Wanaume mmekuwa very unafair kwenye hii thread..hivi kweli hakuna wanawake wanaopambana wenyewe bila nguvu ya wanaume? Au ndio ile notion ya mwanaume akipandishwa cheo ni kwa sababu ya uchapakazi ila mwanamke ni kwa sababu mwili wake? Ni watoto wangapi Tanzania hii kwa mfano tu waliolelewa na wazazi wa kike pekee mpaka wakaweza kujisimamia wenyewe. Humu JF kwenyewe mmejaa kibao. Leo mnakuja with such negative opinions. Acheni hizo. Hata kama wapo waliopitia njia hizo, hamuwezi kuja with such generalizations....

Vipi Mkuu na Wewe ulikuwa ni mmoja wa wale Wanawake waliokuwa wamekaa pale ' Grano Coffee ' Mlimani City nini ile jana wakati wa Kipindi? Manake si kwa ' Povu ' hili Dada yangu. Muwe mnasema basi ukweli kwani wengi wenu hata kudanganya tu hamjui na ndiyo maana wenye ' akili ' na ' IQ ' zilizotukukuka tunawashukieni asubuhi tu / mapema sana.
 
Utajiri wa wapi bwana..aah....mitaji waliyokuwa nayo akina mama ilikuwa hii hii ya mayai na maandazi...na watoto wakasoma.
Sio wote ila ni baadhi kuna ambao wamefanikiwa kwa elimu zao au biashara,ila hawa tunawaona kwenye majukwaa wakifundisha ujasiriamali wengi waongo sana.
Mitaji yao wamepata kwa kudanga tu..kuna wengine wanajiita madirector kumbe ni wauzaji tu
 
Kiukweli ukitafuta mwanamke ambaye kafanikiwa bila ya kutenda dhambi ya kuvuliwa nguo ya ndani ili kupata pesa, mali, cheo,elimu ama ushawishi katika jamii nadhani hawafiki kumi katika mia.

Wengi wamefika hapo walipo kwa mtaji wa kuvuliwa nguo ya ndani ambapo mwili ulihusika sana katika hatua fulani za harakati za kutafuta.

Nakubaliana nawe kwa 99.9999999999% Mkuu. Umemaliza kila Kitu.
 
Kila anayehojiwa na Mtangazaji ' Critical ' na ninayempenda na kumkubali kabisa Siza wa Cloudstv 360 on Saturday wakiwa ' mubashara ' kabisa kutokea Mlimani City kuwa aelezee Historia ya Mafanikio yake hadi leo wamefanikiwa Kimaisha unaona tu wanazunguka zunguka huku mengi tukifichwa.

Nikilitumia sana ' jicho ' langu Kali la ' Kisaikolojia ' na kwa jinsi ninavyowakodolea hawa Wanawake wakiwa ' mubashara ' wanatiririka na wanaserereka naona Shuhuda zao za Kimafanikio hayo waliyonayo zimejaa ' Unafiki ' mtupu hasa kwa wawili mmoja wapo akiwa anapatikana sana Millenium Tower Kijitonyama na mwingine akiwa mara kwa mara humkosi katika Vipindi vyake Channel Ten ambao ' Channels ' zao za hayo mafanikio yao zina mkono wa ' Kimahaba ' wa waliokuwa na Mamlaka yao / wenye Nyadhifa zao hapa Tanzania.

Wito tu Kwenu ambao huwa mnapenda ' Kutudanganya ' kuhusu mlivyopata hayo mafanikio yenu itapendeza sana na hata kutushawishi zaidi kama siyo kutufundisha endapo mtakuwa mnatupa zile Shuhuda zenu halisi hata kama zinatisha au kutia aibu kuliko kudhani kuwa huu uwongo wenu hatutaugundua haraka.

Ngoja niendelee kuwaangalia na nizidi Kudanganyika. Kazi ipo hakyanani!

Nawasilisha.

Ukiwaondoa kina Mengi, Bakhresa, Dewji, Manji....kwa kweli hawa wengine ni wababaishaji tu, haswa hawa macelebrities na ndiyo maana sijawahi kuwasikiliza kwa chochote kile wa sababu stories zao zimeshamiri uwongo na fantasies za kijinga wakati watu wana ukweli na maisha yao ya jinsi walivyofanikiwa. Wengi wanakuwa wanahongwa na hii imekuwa a wish ya kila mwanamke wa Dar (mjini)....anafanya vituko ili asifikane aje kuhongwa na kusaidia wazazi na nduguze hapo baadaye.
 
Vipi Mkuu na Wewe ulikuwa ni mmoja wa wale Wanawake waliokuwa wamekaa pale ' Grano Coffee ' Mlimani City nini ile jana wakati wa Kipindi? Manake si kwa ' Povu ' hili Dada yangu. Muwe mnasema basi ukweli kwani wengi wenu hata kudanganya tu hamjui na ndiyo maana wenye ' akili ' na ' IQ ' zilizotukukuka tunawashukieni asubuhi tu / mapema sana.

Owkey…nilifikiri upo kwenye kujadili hoja…kumbe kuna waliokaa 'Grano Coffee' ndio walikuwa wanakusumbua….

Lihesabu kama povu or not, in short mnakera kuhesabu kila mafanikio ya mwanamke yanatokana na ngono, na si vinginevyo. Labda ili twende sawa, nendeni mkaiendeleze theory hii kwa watoto wenu wa kike ili wasije wakafeli mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom