Wanaume mmekuwa very unafair kwenye hii thread..hivi kweli hakuna wanawake wanaopambana wenyewe bila nguvu ya wanaume? Au ndio ile notion ya mwanaume akipandishwa cheo ni kwa sababu ya uchapakazi ila mwanamke ni kwa sababu mwili wake? Ni watoto wangapi Tanzania hii kwa mfano tu waliolelewa na wazazi wa kike pekee mpaka wakaweza kujisimamia wenyewe. Humu JF kwenyewe mmejaa kibao. Leo mnakuja with such negative opinions. Acheni hizo. Hata kama wapo waliopitia njia hizo, hamuwezi kuja with such generalizations....