Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivyo vipimo mimi pia nimefanya mkuu na nilienda Muhimbili lakini ndo hivyo hawajatibu tatizo bado.Ndio nilipimwa tatizo nimesahau jina la vipimo na jina la dawa,but kipimo kimoja unawekewa waya miguuni mpaka kifuani na kingine Kama utrasound hivi
But wewe nakushauri nenda Hospital kubwa Sana
Vidonda vya tumbo mkuu mbona sijwahi kuhisi kama nina hilo tatizo lakini nitafanya vipimo kwa uhakika, maana hili tatizo la moyo kuvuta ni la tokea utotoni huko mkuu.Pole mkuu ACTUALLY
Unasumbuliwa na vidonda vya tumbo
Inaweza kuwa Una bacteria wa h-pylori
Au wingi wa ACID tumbon
Yote hayo yanakusababishia kitu kinaitwa HEARTBURN ndio ugonjwa wako mkubwa
Ndo mana ukitumia PARACHICHI au JUISI yake unaona ahueni au wakati mwingine kujihisi umepona
TiBA nzuri na ya uhakika badiri mtindo wako wa maisha hasa kula kwa wakati na pendelea zaidi kula vyakura vya jamii ya ALKARINE haswa PARACHICHI na BAMIA viwe havikosi katika milo yako ya kila siku
Mkuu pole kwa maradhi yako ya moyo kupiga nitafute kwa wakati wako ili nipate kukutibia amradhi yako.Habari za jion wana jf!
Nimekua nikitumia dawa za kupunguza mapigo ya moyo kwa muda wa miezi 6 sasa ,mwanzoni niliandikiwa dawa aina ya BISOPROLOL nikatumia kwa muda wa mwezi mmoja tu nikaacha then kutokana na side effects mbaya nikabadilishiwa dawa nikapewa NEBIVOLOL ambayo ndio natumia hadi sasa ila nameza nusu kidonge.
Sababu za kutumia dawa hizi ni kua, tokea nakua katika utoto wangu yani tokea nipo secondary( nikiwa na miaka 13-17) nilikua nikicheza mpira ila kuna muda moyo ulikua unavuta then unaachia yani kama unataka kusimama kudunda, ila kwa kipindi hicho sikuona shida yoyote ile nikawa naendelea na shughuli zangu kama kawaida, ila mwaka jana hali ikwa imechange (hapa nimefika miaka 24) nikawa napamua kwa shida, mikono na miguu inakua ya baridi, mapigo yanaenda mbio.
Halii hii ilinichanganya sana ila nikapata akili fasta nikaingia google na kuanza kutafuta shida ni nini, nilifanikiwa kugoogle matunda yanayoshusha mapigo ya moyo ambaya ni ndizi, machungwa , parachichi na nk. nilivyokua natumia haya matunda Hali yangu ilikua kawaida ila bado nikawa kama sijazuia shida ya kupumua kwa tabu.
Mwaka jana huo huo nikaona niende MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL nikafika nikafanya vipimo vingi sana ambavyo ni:
1.ECG ( Bordeline Abnormal ecg kipimo kikaandika sinus tachycardia ) hakukua na majibu mengine zaidi ya tachycardia
2.ECHO ( Hiki kilisoma normally essentially ECHO findings lakini TACHYCARDIA NOTED ambapo majibu yalikua ifuatavyo)
ECHO FINDINGS
NORMAL SIZED CARDIAC CHAMBERS,
LV-UNIFORM CONTRACTILITY,
NORMAL SYSTOLIC FUNCTION WITH LVEF 71%
NORMAL DIASTOLIC FUNCTION
ALL VALVES ARE NORMAL IN STRUCTURE AND FUNCTIONS
IVC-NORMAL, NO SHUNT/THROMBUS, NORMAL PERICARDIUM
3.Pia nilipima fasting glucose nikakutwa na 5.3mmol/l
4.Blood urea nitrogen (NIkakuta normal )
5.Serum creatinine ( nayo normal)
6.Full blood picture ( normal )
7.Serum cholesterol ( nayo normal)
8.X RAY chest pain ( nayo normal)
Kutokana na majibu hayo juu dokta akaniandikia dawa nilizotaja hapo juu nitumie ili nipunguze mapigo ya moyo lakini mwezi huu kwenye clinic ameniambia niziache hizi dawa, ila mimi kabla ya hapo nilijaribu kuziacha lakini nakua najisikia vibaya sana. kama kuna njia za kuacha hizi dawa niambieni wakuu wangu wa jf.
Lakini pia mbona kama sijatibu tatizo la moyo kuvuta maana huwa linanitokea na sijajua shida ni nini maana nimepima mpaka nimechoka wakuu, kama kuna mtu ameshawahi kupatwa na tatizo hili anisaidie wakuu, maana nimechoka na haya matatizoo mpaka dunia naiona chungu,
NAWASILISHA.
Je mkuu nawezaje kuacha kama kuna mbinu maana nimefatilia reviews nying sana za watu waliotaka kuacha hizi dawa ila naona wengine huwa wanaishia kufariki, icho ndio kinanitisha mkuu.
Sawaaa, afu awalipe au wajitoleeSio lazima aende physically anaweza cheki CVs zao kwenye platforms kama linkedin n.k na akawasiliana nao wakaorganize video conferencing au akattach na docs za matibabu akatatuliwa shida yake kwa bei nafuu na maisha yakaendelea!
Mtu kasoma udaktari, St Fransisi unategemea NiniBongo napo jau ila dokta amenisistiza niziache hizi dawa lakini hajanipa njia ya kuacha mkuu.
Hv kwa akili yako hafifu unadhani hakuna madaktari humu wakamshauriDah, Mkuu Yaani Unaongelea Mambo Ya kitaalamu deep sana Chimbuchibu huko ...Sisi JF members Ushatuacha..na Kutuchanganya..
Sasa Hapo sisi tukushauri nini.? Hivi kuna Mtu anajua Sinus na tachycardia ndo nini.?
Watu Watazunguuka wee Lkn Watakuja kwenye Ushauri huu ' Waone Wataalamu' .
Kuna Jamaa Anaitwa JANABI pale JAKAYA Muhimbili hayo Ndo Mambo Yake Hayo..Ushamtafuta?
Mbona hujamwambia kuhusu pombe na sigara?Huwezi kuacha dawa until umeanza method nyingine za kukusaidia.
1.Punguza matumizi ya chumvi au acha until urecover
2.Kama weight yako ni kubwa itabidi upunguze up to normal range ( body mass index)
3.Fanya mazoezi regular kwa wiki Mara tatu au nne kwa 45 min ...inaweza kuwa simple jogging ( sio magumu ya kukosa hewa)
4.zidisha matunda na mbogamboga kwa wingi .kula spiecies zote muhimu Kwa wingi Kama mdalasini, kitunguu swaumu ,FLAX SEED etc
5 .piga chini junk foods like chips and processing foods .
Zingatia hayo kwa makini
Nenda upande wa piliSawa mkuu, lakini me natafuta alternatively ya vidonge mkuu, nishavichoka na kama vinatibu mbona tatizo la moyo kuvuta haliishi bado lipo pale pale shida ni nini hapo?
aliacha na pia alikuwa haruhusiwi kazi ngumu. Kuna mda anabadilika mpaka jashoDuh ilikuaje mkuu au nae aliacha kutumia dawa ?
Kuna kitu sijaona majibu yake hapo kutokana na tatizo lako 1.BMI, 2.BP 3.Mapigo ya moyo na 4.Vipimo vya sukari ,pia muhimu kuacha vifutavyo kwa sasa,Chumvi,Pombe,Sigara, au kilevi chochote kile,Hasira ,vinyongo-kutosamehe watu,vitu vya mafuta,junk foods,vitu vya sukari nyingi kama soda na chocolate.Ukiweza kumudu hivyo kwa mwezi mzima nenda kacheki tena vipimo vyako.Hiyo Nebivolol unayotumia umesema ni nusu kidonge bado ni dose ndogo sana ingawa sijajua unatumia za miligram ngapi,kama ni za 5 mg,bado ni dose ndogo.Kwenye swala la kuacha pia huwezi kuziacha haraka ki hivyo utatakiwa kuziacha kidogo kidogo sana.Kama utaona vipimo vyako vyote viko normal na bado tatizo linaendelea mgeukie Mungu ufanyiwe maombi,wakati mwingine inaweza kuwa ni maroho yamekuvamia ndio yanayokutesa...
1.Kuhusu BMI, umri wangu ni 24years ,Height yangu in cm ni 175cm, uzito wangu ni 59Kg sasa hapo kucalculate bmi nimesahau kidogo ila nahisi nipo katika normal range.
BP ni 129/80mmhg
Mapigo nilivyopima kabla sijaanza kutumia dawa yalikua yanacheza 112-120 sometimes lakini tokea nianze dawa huwa yanaishia 74,76 80 and sometimes had 90( hapa nilipunguza dozi nilikua natumia robo kidoge cha nebivolol)
Kipimo cha sukari kilisoma 5.3mmol/l dokta aliniambia ipo normal tu
Situmii sigara wala pombe na kuhusu chumvu hapo kabla nilikua napendelea chumvi lakin sasa hapana, na chunk food nimeshaacha kabisa
NEBIVOLOL ninayotumia ni 5mg tablet ila mimi nakata nusu yake yani 2.5mg ndio natumia simezi kidonge kizima na natumia mara moja kwa siku tu.
Hivi nikirudia vipimo naweza kuta tatizo limeisha au ?
Basi acha stress Mkuu unaishi tu bila madawaHivyo vipimo mimi pia nimefanya mkuu na nilienda Muhimbili lakini ndo hivyo hawajatibu tatizo bado.