Nawezaje kuacha kutumia dawa za kupunguza mapigo ya moyo

Habari za jion wana jf!
Nimekua nikitumia dawa za kupunguza mapigo ya moyo kwa muda wa miezi 6 sasa ,mwanzoni niliandikiwa dawa aina ya BISOPROLOL nikatumia kwa muda wa mwezi mmoja tu nikaacha then kutokana na side effects mbaya nikabadilishiwa dawa nikapewa NEBIVOLOL ambayo ndio natumia hadi sasa ila nameza nusu kidonge.

Sababu za kutumia dawa hizi ni kua, tokea nakua katika utoto wangu yani tokea nipo secondary( nikiwa na miaka 13-17) nilikua nikicheza mpira ila kuna muda moyo ulikua unavuta then unaachia yani kama unataka kusimama kudunda, ila kwa kipindi hicho sikuona shida yoyote ile nikawa naendelea na shughuli zangu kama kawaida, ila mwaka jana hali ikwa imechange (hapa nimefika miaka 24) nikawa napamua kwa shida, mikono na miguu inakua ya baridi, mapigo yanaenda mbio.

Halii hii ilinichanganya sana ila nikapata akili fasta nikaingia google na kuanza kutafuta shida ni nini, nilifanikiwa kugoogle matunda yanayoshusha mapigo ya moyo ambaya ni ndizi, machungwa , parachichi na nk. nilivyokua natumia haya matunda Hali yangu ilikua kawaida ila bado nikawa kama sijazuia shida ya kupumua kwa tabu.

Mwaka jana huo huo nikaona niende MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL nikafika nikafanya vipimo vingi sana ambavyo ni:
1.ECG ( Bordeline Abnormal ecg kipimo kikaandika sinus tachycardia ) hakukua na majibu mengine zaidi ya tachycardia
2.ECHO ( Hiki kilisoma normally essentially ECHO findings lakini TACHYCARDIA NOTED ambapo majibu yalikua ifuatavyo)
ECHO FINDINGS
NORMAL SIZED CARDIAC CHAMBERS,
LV-UNIFORM CONTRACTILITY,
NORMAL SYSTOLIC FUNCTION WITH LVEF 71%
NORMAL DIASTOLIC FUNCTION
ALL VALVES ARE NORMAL IN STRUCTURE AND FUNCTIONS
IVC-NORMAL, NO SHUNT/THROMBUS, NORMAL PERICARDIUM

3.Pia nilipima fasting glucose nikakutwa na 5.3mmol/l
4.Blood urea nitrogen (NIkakuta normal )
5.Serum creatinine ( nayo normal)
6.Full blood picture ( normal )
7.Serum cholesterol ( nayo normal)
8.X RAY chest pain ( nayo normal)

Kutokana na majibu hayo juu dokta akaniandikia dawa nilizotaja hapo juu nitumie ili nipunguze mapigo ya moyo lakini mwezi huu kwenye clinic ameniambia niziache hizi dawa, ila mimi kabla ya hapo nilijaribu kuziacha lakini nakua najisikia vibaya sana. kama kuna njia za kuacha hizi dawa niambieni wakuu wangu wa jf.

Lakini pia mbona kama sijatibu tatizo la moyo kuvuta maana huwa linanitokea na sijajua shida ni nini maana nimepima mpaka nimechoka wakuu, kama kuna mtu ameshawahi kupatwa na tatizo hili anisaidie wakuu, maana nimechoka na haya matatizoo mpaka dunia naiona chungu,

NAWASILISHA.
Umejitahidi kuelezea vizuri ila
1.unajuaje kama hapo unapovuta source yake ni moyo
Unapata maumivu upande wa kushoto wa kifua? Na je kifuani pekee au na sehemu zingine za mwili mf bega na mkono
Isije kuwa unachanganya maumivu ya kiungulia(heart burn) na maumivu yanayotokana na kupungua kwa oksijeni kwenye misuli ya moyo(angina)

2.kwa vipimo ulivyofanya ECG imesema abnormal ECG
Haijatoa detail za kila phase ya mzunguko wa umeme kwenye moyo wako
Hii taarifa ni muhimu ukizingatia ndo kipimo ambacho kimeonesha tatizo ni nini

Ushauri
Bado swala lako linahitaji kufanyia more evaluation kwasababu visababishi vya tachycardia(mapigo ya moyo kwenda kasi tofauti na kawaida) ni vingi ikiwemo

Matatizo kwenye tezi muhimu za mwili
Mf thyroid,adrenaline
Stress&anxiety

Jitahidi uonane na mtaalamu wa maswala ya moyo(cardiologist) kama tayari ushamuona mtaalam wa magonjwa ya ndani (physician)
 
Ukiziacha Hali inarudi kama awali au side effects za hizo dawa ndiyo unasema ni ngumu kuziacha?

Pole
 
Nikiziacha pumzi huwa inabana yani napumua kwa shida na pia mapigo ya moyo yanakua juu zaidi mkuu.
 
Huwezi kuacha dawa until umeanza method nyingine za kukusaidia.
1.Punguza matumizi ya chumvi au acha until urecover
2.Kama weight yako ni kubwa itabidi upunguze up to normal range ( body mass index)
3.Fanya mazoezi regular kwa wiki Mara tatu au nne kwa 45 min ...inaweza kuwa simple jogging ( sio magumu ya kukosa hewa)
4.zidisha matunda na mbogamboga kwa wingi .kula spiecies zote muhimu Kwa wingi Kama mdalasini, kitunguu swaumu ,FLAX SEED etc
5 .piga chini junk foods like chips and processing foods .
Zingatia hayo kwa makini
This is the broad spectrum naturopathy,peoples use it as a solution to every problem.

Camooon men.
 
Umejitahidi kuelezea vizuri ila
1.unajuaje kama hapo unapovuta source yake ni moyo
Unapata maumivu upande wa kushoto wa kifua? Na je kifuani pekee au na sehemu zingine za mwili mf bega na mkono
Isije kuwa unachanganya maumivu ya kiungulia(heart burn) na maumivu yanayotokana na kupungua kwa oksijeni kwenye misuli ya moyo(angina)

2.kwa vipimo ulivyofanya ECG imesema abnormal ECG
Haijatoa detail za kila phase ya mzunguko wa umeme kwenye moyo wako
Hii taarifa ni muhimu ukizingatia ndo kipimo ambacho kimeonesha tatizo ni nini

Ushauri
Bado swala lako linahitaji kufanyia more evaluation kwasababu visababishi vya tachycardia(mapigo ya moyo kwenda kasi tofauti na kawaida) ni vingi ikiwemo

Matatizo kwenye tezi muhimu za mwili
Mf thyroid,adrenaline
Stress&anxiety

Jitahidi uonane na mtaalamu wa maswala ya moyo(cardiologist) kama tayari ushamuona mtaalam wa magonjwa ya ndani (physician)
1. Sijajua source ni nin mkuu, ila moyo huwa unavuta upande wa kushoto. Kuhusu maumivu ya kifua sijawahi kuyapata kabisa wala kuhisi kama kifua kinauma na wala sijawahi kupata maumivu kwenye bega wala mkono mkuu.

2.Kwenye kipimo cha ECG kilisoma bordeline abnormal ECG pia kiliandika sinus tachycardia, pia kulikua na magraph yanoenyesha mzunguko wa moyo ila yamefuta hayawezi kusomeka tena mkuu. pia nmepanga kurudia vipimo mwezi ujao.

3. Kweli mkuu maana dokta alitaka kuniandikia kipimo ya hormone ilaa nitapima huo mwezi ujao maana inaweza kuwa sababu pia.
4.Huyo dokta pia ni cardiologist mkuu ndio anaenitibu
5.Pia kuhusu magonjwa ya chronic hatuna historia nayo kwetu sasa najiuliza shida ni nini mkuu ?
 
Nenda supermarket tafuta hizi nuts zinaitwa almonds uwe unakula,halafu uone mrejesho wake…100g ni kama 4000 hivi
 
Daktari kakuambia tatiizo ni nini ?

Yaani kakupa diagnosis ya kuwa una tatizo gani kitaalamu ?
 
Nikiziacha pumzi huwa inabana yani napumua kwa shida na pia mapigo ya moyo yanakua juu zaidi mkuu.
Yanakuwa juu ata Kama ume relax? Je ukiwa na stress yanaendaje? Kwenye ku sex inakupa shida? Unakoka?
 
Nenda supermarket tafuta hizi nuts zinaitwa almonds uwe unakula,halafu uone mrejesho wake…100g ni kama 4000 hivi
Ahsante kwa ushauri mkuu nitafanya hivyo pia.
 
Daktari kakuambia tatiizo ni nini ?

Yaani kakupa diagnosis ya kuwa una tatizo gani kitaalamu ?
Aliniambia hii hali ya sinus tachycardia huwa inatokeaga sometimes kutokana labda na stress au hormones kwahyo aliniambia itapotea yenyewe tu nisiwe na shida, lakini pia aliniambia nifanye kipimo cha hormone

Lakini pia nikimuuliza mbona tatizo la moyo kuvuta alipotei , anasema litaisha tu anakua hana majibu ya moja kwa moja
 
Daktari kakuambia tatiizo ni nini ?

Yaani kakupa diagnosis ya kuwa una tatizo gani kitaalamu ?
Aliniambia hii hali ya sinus tachycardia huwa inatokeaga sometimes kutokana labda na stress au hormones kwahyo aliniambia itapotea yenyewe tu nisiwe na shida, lakini pia aliniambia nifanye kipimo cha hormone

Lakini pia nikimuuliza mbona tatizo la moyo kuvuta alipotei , anasema litaisha tu anakua hana majibu ya moja kwa moja
 
Yanakuwa juu ata Kama ume relax? Je ukiwa na stress yanaendaje? Kwenye ku sex inakupa shida? Unakoka?
Ndio mkuu ila natajaribu kuandaaa mikakati kua nitengezene dozi ya ndizi na machungwa tu
 
Aliniambia hii hali ya sinus tachycardia huwa inatokeaga sometimes kutokana labda na stress au hormones kwahyo aliniambia itapotea yenyewe tu nisiwe na shida, lakini pia aliniambia nifanye kipimo cha hormone

Lakini pia nikimuuliza mbona tatizo la moyo kuvuta alipotei , anasema litaisha tu anakua hana majibu ya moja kwa moja
Usikubali kutumia dawa ambazo daktari hana uhakika na ugonjwa.

Atakupotezea pesa zako bure tu,kuna conditions zinatokea na madaktari wanakuwa hawana kwenye rejea zao,ni new cases kwao hapo watakuwa wanabeti na mwili wako.

Tatizo kama hilo inatakiwa mtu akae chini,atulie,aumize kichwa kwa lengo la kukusaidia na nia njema aangalie anafanyaje.

Kila la hwri Mungu akujaalie
 
Kweli mkuu sijui kwa nini dokta aliniandikia nitumie dawa kwa muda wote huu, maana kadri unavyozid kutumia ndivyo ugumu wa kuacha unaongezeka daah.
 
ww unasumbuliwa na anxiety na panic disorder kwa miaka 24. we bado mdogo Sana ...hivyo vitu huwa vinaishaga vyenyewe kinachokusumbua ni hile hisia kuwa huna ugonjwa mkubwa....so relax hiyo hali itaisha yenyewe...
 
Habari za jion wana jf!
Nimekua nikitumia dawa za kupunguza mapigo ya moyo kwa muda wa miezi 6 sasa ,mwanzoni niliandikiwa dawa aina ya BISOPROLOL nikatumia kwa muda wa mwezi mmoja tu nikaacha then kutokana na side effects mbaya nikabadilishiwa dawa nikapewa NEBIVOLOL ambayo ndio natumia hadi sasa ila nameza nusu kidonge.

Sababu za kutumia dawa hizi ni kua, tokea nakua katika utoto wangu yani tokea nipo secondary( nikiwa na miaka 13-17) nilikua nikicheza mpira ila kuna muda moyo ulikua unavuta then unaachia yani kama unataka kusimama kudunda, ila kwa kipindi hicho sikuona shida yoyote ile nikawa naendelea na shughuli zangu kama kawaida, ila mwaka jana hali ikwa imechange (hapa nimefika miaka 24) nikawa napamua kwa shida, mikono na miguu inakua ya baridi, mapigo yanaenda mbio.

Halii hii ilinichanganya sana ila nikapata akili fasta nikaingia google na kuanza kutafuta shida ni nini, nilifanikiwa kugoogle matunda yanayoshusha mapigo ya moyo ambaya ni ndizi, machungwa , parachichi na nk. nilivyokua natumia haya matunda Hali yangu ilikua kawaida ila bado nikawa kama sijazuia shida ya kupumua kwa tabu.

Mwaka jana huo huo nikaona niende MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL nikafika nikafanya vipimo vingi sana ambavyo ni:
1.ECG ( Bordeline Abnormal ecg kipimo kikaandika sinus tachycardia ) hakukua na majibu mengine zaidi ya tachycardia
2.ECHO ( Hiki kilisoma normally essentially ECHO findings lakini TACHYCARDIA NOTED ambapo majibu yalikua ifuatavyo)
ECHO FINDINGS
NORMAL SIZED CARDIAC CHAMBERS,
LV-UNIFORM CONTRACTILITY,
NORMAL SYSTOLIC FUNCTION WITH LVEF 71%
NORMAL DIASTOLIC FUNCTION
ALL VALVES ARE NORMAL IN STRUCTURE AND FUNCTIONS
IVC-NORMAL, NO SHUNT/THROMBUS, NORMAL PERICARDIUM

3.Pia nilipima fasting glucose nikakutwa na 5.3mmol/l
4.Blood urea nitrogen (NIkakuta normal )
5.Serum creatinine ( nayo normal)
6.Full blood picture ( normal )
7.Serum cholesterol ( nayo normal)
8.X RAY chest pain ( nayo normal)

Kutokana na majibu hayo juu dokta akaniandikia dawa nilizotaja hapo juu nitumie ili nipunguze mapigo ya moyo lakini mwezi huu kwenye clinic ameniambia niziache hizi dawa, ila mimi kabla ya hapo nilijaribu kuziacha lakini nakua najisikia vibaya sana. kama kuna njia za kuacha hizi dawa niambieni wakuu wangu wa jf.

Lakini pia mbona kama sijatibu tatizo la moyo kuvuta maana huwa linanitokea na sijajua shida ni nini maana nimepima mpaka nimechoka wakuu, kama kuna mtu ameshawahi kupatwa na tatizo hili anisaidie wakuu, maana nimechoka na haya matatizoo mpaka dunia naiona chungu,

NAWASILISHA.
Pole sana. Mtafute daktar Ben wa Jakaya kikwete heart institute atakusaidia maana baba yangu mzazi alikua na tatizo kama lako na madawa uliyoandika nimemnunukia sana. Lakini kuna dawa alipewa siikumbuki na toka hapo aliacha kabisa kutumia na wala shida haitokei tena.

0719794789.dkt Ben Soy
 
Back
Top Bottom