Nawezaje kurudishwa kazini baada ya kufukuzwa kazi?

Nawezaje kurudishwa kazini baada ya kufukuzwa kazi?

Erickford4

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2017
Posts
1,133
Reaction score
1,098
Habari zenu wakuu,

Mimi ni mwalimu idara ya sekondari katika mkoa wa Mara. Niliwahi kuugua ugonjwa wa tumbo kujaa na kuvimba ambao kule Mara ni maarufu kwa jina la passport size huwa inatokana na kulogwa.

Nilihangaika kutafuta uponyaji wake kwa njia ya hospitali hali ikawa sivyo hadi niliporudi kwa wenyeji wakanipeleka kwa mtaalam mmoja (kalumanzila) aliyekuwa anaishi nchi ya Kenya akanipa dawa kwenye kikombe, yeye kutibu kwake anatumia hiyo dawa yake tu kama alivyo yule babu wa Loliondo.

Nilipona lakini nilipewa masharti ya kutokula chapati kwani ilidaiwa kuwa nililogewa kupitia chapati.

Maisha yalisonga lakini nikajikuta nimekula chapati tena na kuja kuugua tena ule ugonjwa, nikapelekwa tena na tena kwa ajili ya dawa kwa kweli maisha yangu yalikuwa na mitihani kwa staili hiyo.

Nilitamani kuhama lakini nilipofika halmashauri kulikuwa na tangazo kuuubwa lililosema UHAMISHO UMESITISHWA. Baada ya muda tena niliugua safari hii nilichukia na morali ya kazi ilikatika nikaamua kwenda kwetu Tanga nikahangaika huko mpaka nikaweza kupona kabisa.

Tatizo likaja namna nilivyoondoka kwani mkuu wangu alikataa kunipa ruhusa nikaondoka kwa kulazimisha maana niliona kama wanafurahia kuugua kwangu.

Niliporudi nikakutana na barua ya kufukuzwa kazi na nilipofuatilia wakawa wakali kama mbogo sikukata tamaa nikaenda tena na tena hadi kufika mwaka huu wakaniambia ili niweze kurudi kazini natakiwa niandike barua ya kuomba kuajiriwa upya katika halmashauri nyingine tofauti na ile niliyokuwa nimeajiriwa mwanzo nikiambatanisha vitu vifuatavyo
  1. Nakala ya barua ya kufukuzwa kazini
  2. Nakala ya barua ya kuomba kuajiriwa upya iliyoandikwa kwenda katika halmashauri niliyokubaliwa kuwa nitapata nafasi (yaani hapa inatikiwa niombe kwanza nafasi nikubaliwe kwa maandishi ndio niandike tena barua hiyo nikiambatanisha hiyo nakala)
  3. barua za wadhamini watatu wanaonishuhudia kuwa mwenendo wangu ni wa kukubalika katika jamii, wadhamini hao watatu kila mmoja atoke katika mojawapo ya makundi yafuatayo:
    • Kiongozi wa kisiasa - Mbunge/Diwani
    • Kiongozi wa kiroho - Mchungaji, shehe, padri, askofu
    • kiongozi wa kiutawala - DAS, Afisa tarafa, DC
Baada ya hapo TSC atawasilisha maombi hayo kwa kamati ya TSC wilaya na kamati ya wilaya ikiridhia maombi hayo yatawasilishwa TSC makao makuu kwa hatua zaidi ya kuniombea kibali kwa katibu mkuu utumishi cha kuajiriwa upya kazini, baada ya hapo kama katibu mkuu akiridhia ndio niajiriwe upya.

Nimefuatilia huu mlolongo nikaona kama vile ni mgumu mno kufanikisha naomba kwenu wanabaraza kujuzwa kama ndio utaratibu au wameamua tu kuniwekea vikwazo ili nisifurahie mkate pamoja na familia yangu pia nilitaka usaidizi kwa aliye mjuzi namna rahisi ya kuweza kurudishwa kazini.

Natanguliza shukrani.
 
inaonesha wewe historia yako ni jeuri ndio mana waka ku fix kwa kukuloga kwa awamu hii usipojishusha utalimia meno au nasema uongo ndugu zanguuu
Kwa wenyeji wanafahamu kule ukila chakula hadharani ujue upo hatarini kupigwa kipapai.. mimi nilikuwa bachela nikawa napenda kunywa chai mgahawani ndio wakaniotea hukohuko.
 
Pole kaka.

Ila ungetushirikisha pale ulipo lazimisha kutoka eneo lako la kazi bila ruhusa tungekushauri yatakayo kutokea siku za usoni.

Any wai, sahau kupata tena ajira serikalini.
Shukria
 
Wanakudanganya tu. Unatakiwa upate kibali cha Katibu Mkuu kiongozi ndiye mwenye mamlaka ya kukurudisha kazini. Huyo DED anayetaka kukuajiri upya lazima aoneshe kuwa wewe ni wa muhimu katika hiyo nafasi na hakuna mbadala anayeimudu hiyo nafasi. Hapo utapata kuajiriwa tena baada ya kufukuzwa.

Njia ya pili ni kukata rufaa.
 
Wanakudanganya tu. Unatakiwa upate kibali cha Katibu Mkuu kiongozi ndiye mwenye mamlaka ya kukurudisha kazini. Huyo DED anayetaka kukuajiri upya lazima aoneshe kuwa wewe ni wa muhimu katika hiyo nafasi na hakuna mbadala anayeimudu hiyo nafasi. Hapo utapata kuajiriwa tena baada ya kufukuzwa.

Njia ya pili ni kukata rufaa
Wanakudanganya tu. Unatakiwa upate kibali cha Katibu Mkuu kiongozi ndiye mwenye mamlaka ya kukurudisha kazini. Huyo DED anayetaka kukuajiri upya lazima aoneshe kuwa wewe ni wa muhimu katika hiyo nafasi na hakuna mbadala anayeimudu hiyo nafasi. Hapo utapata kuajiriwa tena baada ya kufukuzwa.

Njia ya pili ni kukata rufaa
Huo utaratibu jinsi ya kupata kibali cha katibu mkuu napenda niufahamu mkuu
 
Ni PM nkushauri,ila usiondoke hapo kituoni.Je una nakala ya barua ya ruhusa?
Sawa nakuja mkuu hapana sina hiyo.. Tulikuwa na utaratubu wa kujaza fomu ya kuomba ruhusa ila najua mkuu wa shule ameiondoa ili nionekane nimeondoka tu
 
pole!

Usiondoke hio almashauri mpaka kieleweke
 
Kwanini unapenda kuamini Waganga? Hao hawawezi kukuponya kwa 100% ni usanii tu

Nenda kwa Katibu tawala Mkoa ukiwa na Mashahidi wa ugonjwa uliokuwa nao na wakutetee...basi.

Huyo Mkuu wako wa shule hakupendi kwasababu angeweza kukutetea, wala waalimu wenzio hawakupendi.
 
Back
Top Bottom