Nawezaje kurudishwa kazini baada ya kufukuzwa kazi?

Nawezaje kurudishwa kazini baada ya kufukuzwa kazi?

Hilo ni kosa la utoro kazini na bilashaka Tume ya utumishi wa walimu (T.S.c) walichukua hatua zifuatazo
1.Kukupa notisi ya kueleza kosa lako
2.kukuhitaji kujieleza ndani ya siku 14 Kwa maandishi
3.Kama ulikataa kosa kuundiwa kamati na kukuhojiwa ana Kwa ana
Makosa ya utoro wa kuanzia siku tano na kuendlea ni miongoni mwa makosa makubwa na adhabu yako ndo kma hiyo(kufukuzwa kazi,onyo au kushushwa cheo)



Hatua mpaka Tsc wanachukua uamuzi wa kufukuza kazi inamaana umeshindwa kuwashawishi Kwa maana wewe unakosa lakini kujifanya huna kosa na kujua Sana Sheria, ninvyo jua Mimi TSC ni chombo cha kumtetea mwalimu lakn inategemea unavyo jieleza nidhamu yako na vitu vingne mfano rekodi yako ya matukio yako ya nyuma n.k

Baada ya kufukuzwa kazi utakaa mwaka mmoja na Kama utahitaji kurudi kazini utawafuata TSC watkupa muongozo wa kurudi kazini lakini watahitaji wajiridhishe Kama tabia na mwenendo wako umebadilika njia ya kujua ni kupitisha barua kuanzia serikali za mitaa na sehemu unazofanyia ibada.

Panachangamoto kubwa Kwa watumishi baadhi kutokujua Sheria za kazi au wakt mwingne hata kanuni ndogo ndogo au muongozo inayotolewa na wizara husika japo zipo na zmeandikwa tena Kwa lugha rahisi.

Ushauri wangu teyari umeshatumikia adhabu ya mwaka mmoja fuata hizo taratibu uweze kurudishwa kazini hakuna shortcut zaidi ya barua kutoka tsc ya kurudishwa kazini kwasababu wao ndo chombo kinachosimamia mienendo ya walimu na vitu vingne
Asante mkuu kwa ushauri mzuri wa kujenga. Nitafatilia hatua zote kama nilivyo ambiwa na kuleta mrejesho.. Kuna walionishauri niende CWT nikalalamike je nitapata usaidizi?
 
Mtoa Post umefikia wapi na shauri lako la kurudishwa kazini ktk Utumishi?
 
Back
Top Bottom