Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuwa bachela siyo kisingizio.Kwa wenyeji wanafahamu kule ukila chakula hadharani ujue upo hatarini kupigwa kipapai.. mimi nilikuwa bachela nikawa napenda kunywa chai mgahawani ndio wakaniotea hukohuko.
Fomu ya ruhusa zinajazwa mbili yako moja na nyingine ya Boss wako.Sawa nakuja mkuu hapana sina hiyo.. Tulikuwa na utaratubu wa kujaza fomu ya kuomba ruhusa ila najua mkuu wa shule ameiondoa ili nionekane nimeondoka tu
Hahaha kweli hii auNi kweli mkuu,Mimi ni mtu wa huko Mara wanaroga hatari Sana sana ukila hovyo... waliniroga kidogo niache msosi pamoja na maumivu makali niliapa nikienda nyumbani nakula ndani tena nafunga mlango.
Mgosi umezingua! Kama utaona maisha ni magumu, rudi tu kijijini tuje tulime ngogwe. Wenzako tunapambana kila siku dhidi ya hawa wadhulumati ili watupandishe madaraja yetu, wewe unakurupuka tu kuacha kazi huku ukiwa hujajiandaa!!Bado sijaenda huko maana maelekezo ya kwanza nilipewa hayo.. Taarifa za mganga zinaandikwa wapi mkuu?
Nipo nafanya mambo mengine ya biashara lakini tatizo maisha yamekuwa magumu na kumtegemea mtu katika ajira manyanyaso mengiKwani huwezi kufanya mambo mengine?
Watu kama nyie hawakosekani popote kwani kama ungepita kimya kimya ingekusumbua nini? Itakuwa umepimwa korona kwa kipimo kipya wewe si bure.Kuwa bachela siyo kisingizio.
Ina maana mabachela wote wa huko Mara wamelogwa???
Mbona ulipoambiwa usile chapati ukala tena??
Wewe una lako jambo ambalo unalijua mwenyewe.
Kuna rafiki yangu mmoja alifukuzwa kazi kwa kiburi chake mwenyewe na akafuatilia milolongo hiyo lakini hajarudishwa kazini tangu mwaka 2012.
Ushauri wangu
TAFUTA MASHAMBA ULIME, KAZI SERIKALINI SAHAU KABISAAA....
Nilichoulizia ni huo mlolongo niliopewa ili kurejea kazini kama ni sahihi na kama siyo nifanyeje ili niweze kurejea na sikumlaumu mtuNisichokipenda ni kusingizia mkuu was shule huku wewe mwenyewe umekiri kuwa ulilazimisha kuondoka baada ya kuona kuwa wanafurahia kuugua kwako.Kwa maana nyingine uliondoka bila kukamilisha taratibu za ruhusa.Sasa lawama kwa mkuu wa shule za nini?
Kawaida yenu wanaJF mtu akifungua uzi mnafukua makaburi kuanza kuchunguza nyuzi za nyuma... Kifupi suala la biashara nililifanya kama mbadala kwa sababu nilikatishwa moyo kuwa siwezi kurudi katika nafasi yangu nikatafuta pakujishikiza ili niweze kujikwamua na ugumu wa maisha... Kuhusu suala la Yesu nimefurahi kuwa niliwahi kukuhubiria na nimekuwa mmoja wa washauri wako waliokufanya ukaacha mambo ya wagangaMleta mada usinenee Mikoa ya Watu Uongo. Zama hizi Walimu weeeengi waliokacha kazi Serikalini na Kukimbilia Sekta Binafsi/Shule Binafsi Wamekosa kazi kutokana na kuyumba kwa SEKTA BINAFSI. Sasa ili waonewe huruma wamekuwa waigizaji wakubwa kuwa walikumbwa na Matatizo Makubwa. Post zako zooote toka 2017 na 2019 It seems ulikuwa Mwanza ukiwa Sekta Binafsi na ulikuwa hapa hapa JF unatangaza bidhaa za mwajiri wako huyo na mbaya zaidi tuliokuwa tukiomba Connection za Waganga Ulitunanga na kutwambia ni YESU PEKEE. Leo unakuja na ngonjera oooh Ulirogwa kwa CHAPATI HUKO MARA ukaenda kwa Mganga sijui Kenya! Acha kunena Uongo Mkuuu nakushauri uende kwa YESU ATAKURUDISHA KAZINI acha kusumbua members wenzako hapa JF. Over
Mbona kama vile wewe ndio mkuu wa shule aseeeSio kweli. Nimekaa huko miaka na miaka nakula hadharani hakuna kitu kama hicho.
Wewe sema una magonjwa yako ya kurithi usisingizie kurogwa, hakuna uchawi. Eti ulirogwa😂😂😂.
Wewe ndio unathamani eti? Hongera kwakuwa maisha yako yamenyookaKwa vile umesema ulilogwa nimejiaminisha hata hivyo hukuwa na faida yoyote ya kiualim kwa taifa. Hakuna msomi wa kujiaminisha amelogwa. Una vyeti tu. Unaweza kuendelea na maisha mengine yanayokufanana. Serkali imeshabahatika kuondoa takataka katika wizara yake.
Jamaaa mpuuzi sana anaanza kusingizia Oooh amelogwa sjui Rorya, oooh wachawi sana Mara. Utapeli pia unaanza hiv hivi ukiona Member analeta stori za kutunga hapa jamvini ujue anakoelekea ni kupiga watu pesa. Ameboa sana ujueKwa nini usiendelee na hiki kiwanda chenu? We unaonekana tu uliacha mwenyewe
AH Mavazi kiwanda cha kutengeneza mashati kinahitaji Mawakala wa Kuuza bidhaa zao
AH MAVAZI TANZANIA Ni kiwanda cha kutengeneza mashati nadhifu yaliyo dariziwa. Tunatangaza nafasi za ajira kwa wenye bidii ya kazi tu. Watu wenye ushawishi na wanaoweza kuuza bidhaa zetu kwa nafasi ya uwakala wa mauzo mnakaribishwa. MASHARTI: 1. Taja mkoa au mji uliopo 2. Eleza uwezo wa...www.jamiiforums.com
Ulifanyaje biashara wakati ulikua umerogwa tumbo limeshiba ndindiii kiasi kwamba ulishindwa kufundisha darasani? JF haipotezi ushahidi Mkuuu ndio maaana unaona hadi wadau wameanza kupandisha nyuzi zako za zamani hapa hapa kukupa fact jinsi unavyozingua.Kawaida yenu wanaJF mtu akifungua uzi mnafukua makaburi kuanza kuchunguza nyuzi za nyuma... Kifupi suala la biashara nililifanya kama mbadala kwa sababu nilikatishwa moyo kuwa siwezi kurudi katika nafasi yangu nikatafuta pakujishikiza ili niweze kujikwamua na ugumu wa maisha... Kuhusu suala la Yesu nimefurahi kuwa niliwahi kukuhubiria na nimekuwa mmoja wa washauri wako waliokufanya ukaacha mambo ya waganga
Wee ni muongo na mpuuzi tu,angalia post namba 16 ukimjibu BUMIJA.Maisha yamekuchapa unakuja na visingizio humu.Hata post zako za miaka ya nyuma zinaonyesha uliacha kazi mwenyewe.Nilichoulizia ni huo mlolongo niliopewa ili kurejea kazini kama ni sahihi na kama siyo nifanyeje ili niweze kurejea na sikumlaumu mtu