Nawezaje kurudishwa kazini baada ya kufukuzwa kazi?

Pole sana mkuu mimi siwezi kuhukumu mwenye makosa ni nani kati yako wewe na mkuu wa shule kwasababu sijasikiliza upande wa pili ambao ni mkuu wa shule.

Ila kama ulifanya kuondoka kazi kwa jeuri yako pole sana na inawezekana vipi mkuu wa shule anaona tumbo lako limejaa afu yeye akufukuze kazi?

Any way mimi ni mwakilishi wa wahitimu wasio na ajira naomba nikukaribishe mtaani, karbu sana.
 
Case closed katika wachangiaji wote wewe ndiye uliyeoffer solution kwa tatizo linalomkabili.
Usipozingatia hapa utakuwa mtu mjeuri jeuri tu.
 
Ulilishwa dawa na wajita ile ya kuvimbisha tumbo.

Duh, pole sana mkuu
 
Kwani wewe ni jinsia gani. Kama ni mwanamke na hujawai mpa boss sukari basi mpelekee atakurudisha ila kama ulikuwa unampa bac jua kapata sukari tamu zaidi kaamua nafasi yako kuweka mwingine.

Kwa part ya mwanaume binafsi huwa sirecommend mwanaume kufanya kazi za kuajiriwa. Hivi uloshajiuliza, siku ukifa wanao unawaachia nini. Mwanaumeunatakiwa utengeneze business empire ambayo hata watoto wako wataridhi. Tijaribu kuiga hawa wahindi na waarabu.
 
Hujamuahidi demu kumuowa alaf ukamtema kweli? Maana huko Kanda ya ziwa kula demu ila usifanye kosa la kumuahidi kumuowa alaf umuache haki ya nani unalogwa Kuna mmoja nywele hazioti na asimamishi
 
Zile mbinu ulizotumia kumteka dada wa kazi nenda kazitumie kumteka boss
 
kuwa makini usije ukatumia akiba yako kuhonga ili urudi kazini maana huenda ukabaki mtupu huna hata 100 na kazini usirudi, kama unao mtaji kidogo bora uanzishe biashara na nguvu zako uziweke huko pengine rizk yako iliyokua serekalini imeisha fanya biashara nyingine na Mungu atakusaidia mkuu
 
Pole sana..ila bro mbishi...umeambiwa usile chapati ukarudia...
 
Ni PM nkushauri, ila usiondoke hapo kituoni. Je una nakala ya barua ya ruhusa?
Alilazimisha kuondoka inaonekana huyu hakuruhusiwa, pia inaonekana wakuu wake aliwaambia hapaswi kula chapati, na akawa anakula!
Lazima walimjaji kuona anafanya makusudi apate ruhusa.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Pole sana mkuu.

Mimi nakushauri kuwa utangaze mgogoro kwa kuwasilisha malalamiko yako kwa tume ya usuluhishi wa migogoro makazini (Commission for Mediation and abitration-CMA). Wa contact kwanza hawa jamaa uwaelezee issue yako namna ilivyokaa, then wao watakupa ushauri wa nini cha kufanya hatua kwa hatua, na ni namna gani ya kujaza fomu zao za kutangaza mgogoro na kuanzia hapo muajiri wako ataitwa na shauri litaanza kusikilizwa.

Hawa huwa ni watu useful sana kwa waajiriwa, sema wabongo wengi bado hatujawajua na hatujajua kazi zao.

Hatua ya kwanza, cheki na muwakilishi wa ofisi ya CMA hapo Musoma, contacts zake hizi hapa;
CMA MUSOMA, MARA

Mukendo Street, Near Post Office, P.o.Box 260, Musoma. In charge Honourable Haruna Soleka Mobile No: 0759272218.


Pia kwa maelezo zaidi unaweza ingia kwenye website yao Home | Commission for Mediation and Arbitration kuna maelezo mbalimbali huko wametoa kuhusu namna ya kufungua malalamiko ya kuachishwa kazi isivyo halali, etc.
Ila, cha muhimu zaidi wasiliana na hao jamaa wa CMA wa Musoma, utapata mwanga na watakufungua macho sana.
Erickford4
 
Kwa wenyeji wanafahamu kule ukila chakula hadharani ujue upo hatarini kupigwa kipapai.. mimi nilikuwa bachela nikawa napenda kunywa chai mgahawani ndio wakaniotea hukohuko.
Pole sana mkuu,najaribu kulibeba tatizo lako lakini nashindwa,Mungu akupiganie.

Najaribu kuwaza kwa sauti sasa kinachowufanya wakupige kipapai ni nini??

Au kuna vitu unawakera?
 
Unamhubiri yesu huku unaenda kwa mganga crazyyyyy!!!

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Brother usichanganye mambo huyo mgogoro ushafunguliwa na muajiri wake ambae ni halmashauri yake husika(mkurugenzi)

Mkurugenzi alimpeleka Tsc ambao wao ndo watatuzi wa mgogoro baina ya walimu na muajiri ( kumbuka mkurugenzi Hana mamlaka kisheria kumfukuza mwalimu kazi au kutoa adhabu yoyote) chombo chenye mamlaka ya kutoa adhabu au kutatua mgogoro Kwa walimu ni tume ya utumishi wa walimu (TSC) ambapo katibu wake ni presidential appointee kuna ngazi ya Kwanza ya wilaya harafu kuna Tsc taifa
Zamani kulikuwa na tsc wilaya ,taifa na mkoa lakini tsc mkoa
Iliondolewa baada ya kubadilishwa toka tsd kwenda tsd

Uamuzi ukitolewa na TSC wilaya Kama usipo ridhia maamuzi utakata rufaa ndani ya siku 40 kwenda ngazi ya Tsc taifa.

Kwakifupi Sana maana katika hili kuna mengi ya kuelekeza lakini ngoja nimshauri tena

Hakuna chombo kinaweza kutengua uamuzi wa TSc kwasababu hawa ni chombo huru na kinafanya uamuzi pasipo kupendelea au kuonelea

Pili baada ya adhabu kutolewa ulipewa nafasi ya kukata rufaa ulikata?

Tatu uamuzi ulikuwa umefukuzwa KAZI lakni baada ya mwaka mmoja umepewa taratibu za kurudi kazini
Sasa hapo shida ipo wapi?

Hebu fuata hizo taratibu uone Kama hutorudi kazini
 
Ahsante kwa mchango wako. Mimi sijui chochote kuhusu haya mambo, nimejaribu tu kumuelekeza jamaa sehemu ambayo anaweza kupata muongozo sahihi. Ndio maana nikamwambia acheki na hao watu wa CMA, kama maelezo yako uliyoyatoa yako sawa ina maana jamaa wa CMA atamwambia hivyo hivyo pia. Ni muhimu apate ushauri wa kitaalamu kutoka kwa huyo mwakilishi wa CMA huko Musoma, ndio maana nimecopy na ku paste details za huyo mwakilishi kutoka website ya CMA ili awasiliane nae. Maana wao watakua na weledi zaidi na uzoefu wa kudeal na hayo mambo.
ngurutu
 
Tupo pamoja brother lengo kujenga
 
Usiache nkakutukana nikafungiwa.. kwa hiyo huyo biashara niliifanya mwaka 2017? We ukiugua unalala tu ndani ndio matatizo ya watoto kujaa jf umezoea kulishwa na baba au kwa shemeji umiza kichwa kuwaza sio makalio
 
Jamaaa mpuuzi sana anaanza kusingizia Oooh amelogwa sjui Rorya, oooh wachawi sana Mara. Utapeli pia unaanza hiv hivi ukiona Member analeta stori za kutunga hapa jamvini ujue anakoelekea ni kupiga watu pesa. Ameboa sana ujue
Uzuri wake nyuzi zangu za nyuma nilijielezea matatizo niliyopataga hadi kupelekea kuacha kazi na kuachana na mwanamke wangu ambaye nilizaa naye mtoto mmoja.. Usipende kukurupuka.. Nimekuomba wapi hela?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…