Kwani Mbatia ashakaa miaka mingapi kwenye kiti? na je kwa muda wote aliokaa kwenye kiti unajua ashafanya mambo mangapi ya kukihujumu chama na wakamvumilia? Fikiria mtu ashakaa kwenye kiti kwa zaidi ya miaka 10 afu hapo hapo ulitegemea wangeendelea kumvumilia. Kwa ccm hauwezi kupitisha ukomo wa miaka iliyoainishwa kwenye katiba yao. Lakini pia hakuna mwenyekiti ambae anaweza kukihujumu chama chao ili kumpa nafasi adui (wapinzani) aje akiangushe chama. Lakini kwa viongozi wa upinzani kuhujumu vyama vyao kwa sababu ya masilahi yao hilo ni kawaida, ndo maana hawa wamethubutu kuchukua hatua ila upande wa pili mtu kapokea mshiko akamuingiza waliemwita fisadi agombee kupitia chama chake huku akiwaacha wale waliopigania chama kwa jasho na damu wakimpigia deki mgombea wa mchongo alielengeshwa mahususi na ccm (hiyo ni hujuma kubwa kwa chama)