Nchi ambazo zinahangaika kujenga matundu ya choo hazipaswi kutoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri duniani

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Tumesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa Tanzania imetoa dola za Kimarekani milioni moja (zaidi ya bilioni 2 na milioni 200) kwa Uturuki iliyopatwa na janga la tetemeko la ardhi mwezi ulliopita.

Yapi Merkezi ni kampuni ya Kituruki inayojenga SGR kutoka Dar hadi Mwanza kwa zaidi ya trilioni 14 shilingi za kitanzania. Hii hi theluthi nzima ya bajeti ya Tanzania kwa mwaka!

Tanzania ni moja ya nchi maskini sana duniani na matatizo yetu bado ni yale ya siku za kale, kama kukosa maji safi na salama, watu kukosa chakula na kufa kwa njaa, wanafunzi kusomea chini ya miti na wananchi kushindwa kumudu kuwa na vyoo hata vile vya shimo!

Inashangaza sana kuona nchi kama yetu iliyo kwenye list nyekundu ya nchi maskini duniani ikitoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri za Ulaya kama Uturuki!

Kwa maoni yangu haya ni matumizi mabaya ya fedha za maskini....
 
Andiko lako limenitoa machozi mkuu

FB_IMG_1575390806699.jpg
FB_IMG_1575390792397.jpg
 
Tumesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa Tanzania imetoa dola za Kimarekani milioni moja (zaidi ya bilioni 2 na milioni 200) kwa Uturuki iliyopatwa na janga la tetemeko la ardhi mwezi ulliopita.
Endeleeni na huyu mama ikifika 2030 watanzania wote tutaongea kirumi wakati huo maza atakuwa na miaka 70 ni bibi
 
Yep Merkezi ni kampuni ya Kituruki inayojenga SGR kutoka Dar hadi Mwanza kwa zaidi ya trilioni 14 shilingi za kitanzania. Hii hi theluthi nzima ya bajeti ya Tanzania kwa mwaka!

Tanzania ni moja ya nchi maskini sana duniani na matatizo yetu bado ni yale ya siku za kale, kama kukosa maji safi na salama, watu kukosa chakula na kufa kwa njaa, wanafunzi kusomea chini ya miti na wananchi kushindwa kumudu kuwa na vyoo hata vile vya shimo!

Inashangaza sana kuona nchi kama yetu iliyo kwenye list nyekundu ya nchi maskini duniani ikitoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri za Ulaya kama Uturuki!

Kwa maoni yangu haya ni matumizi mabaya ya fedha za maskini....
 
Cha ajabu majanga yetu wenyewe hatusaidiwi na serikali zaidi ya viongozi kupiga picha na wahanga.
 
Mi nashauri kama hela zipo basi nchi iwe inafanya kuziinua startup za ndani hata zenye risk kubwa. Maana zikifanikiwa tutakaofaidika na huduma hizo ni watanzania. Na aliyesaidiwa kodi za watanzania ni mtanzania.

Kumbe nchi ina hela sana sema tu wapi zinaelekezwa ndio tabu.

Mashirika ya nje tukishiriki kuwapa mawazo ya startup zetu yatafavour zile zenye faida kwa nchi zao zaidi
 
Endeleeni na huyu mama ikifika 2030 watanzania wote tutaongea kirumi wakati huo maza atakuwa na miaka 70 ni bibi
Halafu kwa nini iwe 2030?

Kwani mihula miwili kwa kila awamu ni lazima?

Na hata kama tumezoea mihula miwili kwani awamu ya tano mhula wake wa pili si ndio inaisha 2025!

Au watanzania wote tumenunua wazo la kwamba hii ni awamu ya sita wakati ni ya tano.

Huu utakuwa mfano wa big lie tekniki. Waambie watu kila siku kwamba hii ni awamu ya sita, ya sita, ya sita hadi wazoee (hata kama ni uongo) halafu watakubali hivyo utakuwa na 'haki' ya kudai muhula wako wa pili
 
Mimi naishukuru serikali maana ni kawaida. Kwanza hili janga linachukuliwa kwa wepesi, watu walio kufa ni wengi kupindukia.. ingalikuwa hali hii inaikumba marekani nadhani tungejua, maana wale watu elf tatu tunakumbuka siku zote.
Any way
Shida mi naiona ni nani aliye amua? Alishauriwa na nani? Kwanini hilo jambo lisipitishwe na bunge?
Pili, kwanini tuangalie uturuki tuu na tumuache Bashar al assad au mnamuogopa beberu?
 
Tumesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa Tanzania imetoa dola za Kimarekani milioni moja (zaidi ya bilioni 2 na milioni 200) kwa Uturuki iliyopatwa na janga la tetemeko la ardhi mwezi ulliopita.

Yapi Merkezi ni kampuni ya Kituruki inayojenga SGR kutoka Dar hadi Mwanza kwa zaidi ya trilioni 14 shilingi za kitanzania. Hii hi theluthi nzima ya bajeti ya Tanzania kwa mwaka!

Tanzania ni moja ya nchi maskini sana duniani na matatizo yetu bado ni yale ya siku za kale, kama kukosa maji safi na salama, watu kukosa chakula na kufa kwa njaa, wanafunzi kusomea chini ya miti na wananchi kushindwa kumudu kuwa na vyoo hata vile vya shimo!

Inashangaza sana kuona nchi kama yetu iliyo kwenye list nyekundu ya nchi maskini duniani ikitoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri za Ulaya kama Uturuki!

Kwa maoni yangu haya ni matumizi mabaya ya fedha za maskini....
Ni lazima ujiulize msaada huo umetolewa kwa minajili ipi?-- kwani msada huo umekwenda Uturuki kujenga madarasa au kuokoa maisha ya watu waliopatwa na msiba?, kumbuka; "kutoa ni moyo na wala sio utajiri" walisema wahenga.
 
Ni lazima ujiulize msaada huo umetolewa kwa minajili ipi??-- kwani msada huo umekwenda Uturuki kujenga madarasa au kuokoa maisha ya watu waliopatwa na msiba??, kumbuka; "kutoa ni moyo na wala sio utajiri" walisema wahenga.
Ukweli ni kwamba utoaji unapaswa kutosababisha matatizo yasiyo ya lazima upande unaotoa. Maskini kutoa huku mwenyewe akifa njaa ni kosa.
 
Ungetolewa sperm donor

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli ni kwamba utoaji unapaswa kutosababisha matatizo yasiyo ya lazima upande unaotoa. Maskini kutoa huku mwenyewe akifa njaa ni kosa.
Maskini naye anayo nafasi yake katika kutoa hususan katika majanga kama hayo, ama atoe kwa hali au mali, Sisi hatuna hali (rescue gears/ushauri) na tuachoweza kutoa ni mali (pesa), kumbuka Tz sio isolated country ni part ya dunia isitoshe leo ni kwa mwenzako kesho ni kwako.

Huo mchango ni sawa na mchango wa rambirambi, huwezi kusema maskini hatakiwi kutoa rambirambi kwenye msiba wa tajiri, rambirambi pia ni ishara ya maombolezo na kuonyesha huzuni juu ya msiba in short ni suala la humanity na sio suala la haves and have nots.
 
Back
Top Bottom