Nchi ambazo zinahangaika kujenga matundu ya choo hazipaswi kutoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri duniani

Nchi ambazo zinahangaika kujenga matundu ya choo hazipaswi kutoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri duniani

Endeleeni na huyu mama ikifika 2030 watanzania wote tutaongea kirumi wakati huo maza atakuwa na miaka 70 ni bibi
Mama anahusu nini? Ulisikia mama katowa hizo pesa?

Hapo inaongelewa Tanzania, siyo serikali ya Tanzania.
 
Ukweli ni kwamba utoaji unapaswa kutosababisha matatizo yasiyo ya lazima upande unaotoa. Maskini kutoa huku mwenyewe akifa njaa ni kosa.
Kwanza hapo ukute tunaambiwa Dola milioni moja kumbe zipo milioni 10, zingine Balozi kaambiwa vijana watakuja kuzichukua.
 
Waswahili wanasema msaada usizidi uwezo, mimi naona huo msaada wetu umetuzidi uwezo kabisa, niseme ndio tumeutoa huku tunalia kimoyo moyo.

Wewe ungependa itolewe kiasi gani ili msaada usizidi uwezo??
 
Heri yake kama ni sadaka. Lakini ni mlipa kodi muaminifu pia? Maana vinavyopatikana kwa njia haramu haviwezi kuwa sadaka. Au isije kuwa ni muuza madawa ya kulevya anayetakasa fedha zake!!
Hizo porojo zingine.

Wapi iliandikwa serikali ya Tanzania imetowa huo msaada?
 
Tumesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa Tanzania imetoa dola za Kimarekani milioni moja (zaidi ya bilioni 2 na milioni 200) kwa Uturuki iliyopatwa na janga la tetemeko la ardhi mwezi ulliopita.

Yapi Merkezi ni kampuni ya Kituruki inayojenga SGR kutoka Dar hadi Mwanza kwa zaidi ya trilioni 14 shilingi za kitanzania. Hii hi theluthi nzima ya bajeti ya Tanzania kwa mwaka!

Tanzania ni moja ya nchi maskini sana duniani na matatizo yetu bado ni yale ya siku za kale, kama kukosa maji safi na salama, watu kukosa chakula na kufa kwa njaa, wanafunzi kusomea chini ya miti na wananchi kushindwa kumudu kuwa na vyoo hata vile vya shimo!

Inashangaza sana kuona nchi kama yetu iliyo kwenye list nyekundu ya nchi maskini duniani ikitoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri za Ulaya kama Uturuki!

Kwa maoni yangu haya ni matumizi mabaya ya fedha za maskini....
Hivi ukichukua MKOPO benk, ukitokea msiba Jirani, ukichukua sehemu ya MKOPO kumpa pole Jirani aliyefiwa, bank inaweza kukusamehe rejesho la wiki hiyo ya msiba?

Anyway kusaidia wenye taabu Si vibaya.
 
Maskini naye anayo nafasi yake katika kutoa hususan katika majanga kama hayo, ama atoe kwa hali au mali, Sisi hatuna hali (rescue gears/ushauri) na tuachoweza kutoa ni mali (pesa), kumbuka Tz sio isolated country ni part ya dunia isitoshe leo ni kwa mwenzako kesho ni kwako.

Huo mchango ni sawa na mchango wa rambirambi, huwezi kusema maskini hatakiwi kutoa rambirambi kwenye msiba wa tajiri, rambirambi pia ni ishara ya maombolezo na kuonyesha huzuni juu ya msiba in short ni suala la humanity na sio suala la haves and have nots.
Atukatai angetoa ata Dola laki moja,nadhani ata Rais Erdogan atakuwa kashituka kwa nchi Masikini kama Tanzania kutoa Hela ndefu namna hiyo.
Ila hawa Wanasiasa wetu siyo wa kuwaamini, unaweza kuta tumetangaziwa Dola milioni moja kumbe zipo milioni 10 zingine Balozi kaambiwa vijana watakuja kuzichukua.
 
Mama anahusu nini? Ulisikia mama katowa hizo pesa?

Hapo inaongelewa Tanzania, siyo serikali ya Tanzania.
Kwamba mm nikitoa msaada Leo uturuki watasema Tanzania imetoa msaada sio?

Hivi umefunga Kweli au una kashata Kwa baibui unakula Kwa kificho?

Au kufunga kusema uongo Haiwezekani?
 
Mnajuwa nani aliyetowa hizo fedha au mnakurupuka tu?
Tupo vizuri,Mama anaupiga mwingi.
Screenshot_20230324_130110.jpg
 
Dola milioni moja msaada wa kibinafamu kwa taifa kubwa kama Tanzania ni pisa kiduchu! Kumbuka tuliuza dhabu tu yenye thamani dola bilioni 3 mwaka 2022
 
Wapi iliandikwa serikali imetowa sadaka?
Tujuze katoa nani?
Kama Lengo lilikuwa ni kutojulikana angeweza peleka kimya kimya. Na pesa ikapokelewa vizuri tu

Ila kama wanatangaza Tanzania imetoa msaada, maan yake ni serikali ya Jamhuri.
 
Tumesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa Tanzania imetoa dola za Kimarekani milioni moja (zaidi ya bilioni 2 na milioni 200) kwa Uturuki iliyopatwa na janga la tetemeko la ardhi mwezi ulliopita.

Yapi Merkezi ni kampuni ya Kituruki inayojenga SGR kutoka Dar hadi Mwanza kwa zaidi ya trilioni 14 shilingi za kitanzania. Hii hi theluthi nzima ya bajeti ya Tanzania kwa mwaka!

Tanzania ni moja ya nchi maskini sana duniani na matatizo yetu bado ni yale ya siku za kale, kama kukosa maji safi na salama, watu kukosa chakula na kufa kwa njaa, wanafunzi kusomea chini ya miti na wananchi kushindwa kumudu kuwa na vyoo hata vile vya shimo!

Inashangaza sana kuona nchi kama yetu iliyo kwenye list nyekundu ya nchi maskini duniani ikitoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri za Ulaya kama Uturuki!

Kwa maoni yangu haya ni matumizi mabaya ya fedha za maskini....
Tz muda wowote kuanzia sasa Tutauza umeme afrika kusini "sauti ya maza ilisikika"
 
Mada umeielewa lakini? Yaani unaomba kibaba cha unga kwa jirani, jioni unachangia Elfu tano kwa jirani mwingine ambaye kioo cha dirisha lake kimevunjwa na upepo.
Huyu anapenda ligi,hataki kukubali kuwa Mama katukosea Watanzania.Tuna hali ngumu hivi alafu anapeleka misaada kwa matajiri.Hiyo pesa si angeongezea ata Ruzuku ya Mbolea kwa Wakulima au angewapa TARURA warekebishe Barabara za vijijini.
 
Back
Top Bottom