Nchi ambazo zinahangaika kujenga matundu ya choo hazipaswi kutoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri duniani

Tanzania kuna hela wewe,ukitaka kuamini piga hesabu miradi yoote mikubwa na midogo aliyoifanya MAGU ndo utajua uturuki ni maskini kuliko sisi.
 
Mnajuwa nani aliyetowa hizo fedha au mnakurupuka tu?
 
Waswahili wanasema msaada usizidi uwezo, mimi naona huo msaada wetu umetuzidi uwezo kabisa, niseme ndio tumeutoa huku tunalia kimoyo moyo.
 
Ngoja lema akusikie
 
Tumeiga from South Africa na Egypt..
tuna pesa asee
Hao wenzetu Uchumi wao mkubwa na nchi zao zimejitosheleza kimiuondombinu.Juzi tu nimesikia Japan imelipa Jiji la Mbeya milioni 187 kujenga matundu ya vyoo!
 
Hao Uturuki wenyewe siku chache baada ya tetemeko la ardhi wakaendelea na mashindano waliyoandaa kwa gharama kubwa ya EU indoor championship na stadium ilikuwa inajaza washangiliaji kama upande mwingine wa nchi yao akujatokea majanga.

Wewe kiherehere wananchi wako ata hela za kugomboa miili ya ndugu zao hospitali wakailaze kwenye nyumba zao za milele hawana; halafu unataka kusaidia nchi tajiri.
 
Tena mnapaswa mshukuru aliyetowa hi yo sadaka kataka ifahamike ni Tanzania, hakutaka hata jina lake lijulikane.
Heri yake kama ni sadaka. Lakini ni mlipa kodi muaminifu pia? Maana vinavyopatikana kwa njia haramu haviwezi kuwa sadaka. Au isije kuwa ni muuza madawa ya kulevya anayetakasa fedha zake!!
 
Tena mnapaswa mshukuru aliyetowa hi yo sadaka kataka ifahamike ni Tanzania, hakutaka hata jina lake lijulikane.
Sadaka ya nini, Serikali hutoa sadaka?
Huwezi tenganisha Tanzania na serikali ya Tanzania.
Tunapaswa kushkuru kwa lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…