Nchi ambazo zinahangaika kujenga matundu ya choo hazipaswi kutoa msaada wa fedha kwa nchi matajiri duniani

Hiyo pesa ifuatiliwe,ukute tunaambiwa Dola milioni moja kumbe zipo milioni 10 zingine Balozi kaambiwa vijana watakuja kuzichukua.
 
Na mimi nilishangaa wanajamvi wakanikemea

 
Weka clear maoni yako, Tanzania ni nchi yenye wsnachi wske na yenye serikali yake, hizo pesa "ulizosikia" hukusikia katowa nani?

Wacheni fitna za rejareja.
 
Kutoa ni moyo si utajiri. Malawi pia tumewapa 1M USD na misaada mingine.

 
Walipaswa kununu madawati 4000 na sio ticket 4000!
 
La hasha!

Tanzania ni watu wakarimu Africa nzima ni sisi ndo tuna historia hiyo!

Ukarimu haumaanishi UTAJIRI!

A GIVING creates an Energy which causes a lot of inward flows..either by knowing or unknowingly!

Siyo Lazima tuone majawabu yake sasa hivi...ila huo ni utamaduni Mzuri na hiyo ndiyo Tanzania!

Wewe unaposikia Wenzetu wanapatwa na Majanga Mazito kila uchwao wadhani Mungu hatuoni??

Mi kwa kweli naipongeza Serikali kwenye hatua hiyo!!
 
Aiseeeeee !!!
 
Kutoa si wajibu wa tajiri tuu, hata maskini anapaswa kutoa.

Ni Tabia ya Maskini kudhani kuwa yeye anapaswa kupewa tuu.

Uturuki wamepatwa Janga baya sana. Wanahitaji msaada. Hatuwezi kwenda na maneno tuu bila chochote.

Hizo fedha hata zingebaki hapa nyumbani, zisingetatua matatizo yote tuliyonayo.

Naunga mkono kilichofanyika, Kwanza Nchi yetu inapata heshima, kwamba Licha ya Umaskini wetu lakini bado tunaweza saidia kwa kidogo tulichonacho.
 
Fazili upo sahihi kbs ✔️!! But nakuja tofaut kidogo juu ya hili... B 2 na point ni pesa nying lkn kwann tusipigie kelele mabilioni mengi zaid ya hizi mbili? At least bora zipo wazi zimeenda kama msaada. Je haya mabilioni ya kifisadi ambayo CAG ameelezea sana, kwann wahusika hwachukuliwi hatua? Basi pesa zote zirudishwe lkn hakuna. Hapa ndipo pa kukazia zaid!!
 


Hiyo Dola laki moja unayoisema kwa mtu mwingine bado ni ela ndefu sana na kwa mwingine ni ela ndogo sana halikadhalika hiyo dola milioni moja ni hivyo hivyo kwa mwingine ni ela ya kawaida na kwa wengine kama wewe ni ela ndefu, Sasa nadhani mada ilistahili iwe; NI KIGEZO GANI KINACHOFUATWA KATIKA KUTOA KIASI CHA PESA ZA RAMBIRAMBI KATIKA MAJANGA??, hapo nadhani hiyo ndio ingekuwa mada inayofaa kwani hatubishani juu ya utoaji wa rambirambi bali tunabishana juu ya kiwango cha rambirambi.
 
Hii nchi ni tajiri😂😂😂 afu Kuna watu wanalia magu kununua ndege
 
Acheni kunung'unika. Ilichofanya Tanzania ni kumsaidia rafiki aliyepata janga na wala siyo msaada. Kumsaidia jamaa yako aliyepeta janga haihitaji hadi uwe tajiri.

Ingelikuwa Tanzania inaweka bajeti ya misaada kwenye bajeti yake ya kitaifa ili kusaidia nchi nyingine ilihali tunajua nchi yetu haijitoshelezi kwa mahitaji yake hapo tungesema kuna tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…