Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Wakati nasoma uzi wako, akilini mwangu nilikuwa nafikiria swali lako uliouliza.
"watoto wetu wataikuta Tanzania ya namna gani? "
Kama na wewe umeliona hili, sina shaka kabisa kwamba tunapoelekea sio pazuri kabisa.
 
Huu uzi umenigusa mkuu kasanga70 kwanza hongera umelima eka 20 umepata maguni 200 kuonyesha ulivyozingatia hatua zote za kilimo bora. Mwenzako nimelima mara ya kwako nimeambulia 180. Kanitangaze alifanya yake...mvua ikanikimbia na sasa bei imetutoroka...Serikali imesema itanunua bado sijajua bei yao. Mkuu ukisikia bei popote unishtue
 
umeniliza upya nimemkumbuka JPM alivyokuwa anapambana kuifikisha Tanzania kwenye nchi ya asali na maziwa.

uongozi sio kitu rahisi.

tusiache kuliombea Taifa letu.
 
ndugu hebu nitajie nchi ambayo imeweza kutatua hayo uliyosema na wako paradiso ndogo nchi gani
 
We hujielewi huku dar wanauziwa unga sembe bei huu. Safirishwa mahindi Dar uuze bei nzuri acha ujinga
Wewe ndio hujielewi kabisa yaani na sio kosa lako ngoja nikutoe tongotongo
Sokoni dar kg moja ya mahindi inanunuliwa kwa wastani wa tsh 400 Hadi 460 Sasa twende kimahesabau
Gunia moja Lina wastani was kg 110 sawa? Sasa chukua 110 × 460 = 56000/=
Hapo toa matumizi yafuatayo

Usafiri kutoka namtumbo, mpwapwa mbeya n.k mfano gunia moja kulisafirisha iwe Tsh 10000 kwa gunia
Pakia shusha iwe 2000
Ushuru 1500 kwa gunia
Kiroba 1000 jumla ndogo 14500/=

Kwa hiyo 56000- 14500 = 41500[emoji848][emoji848][emoji848]

Kwa hiyo gunia utakua umeliuza tsh 41500 [emoji848][emoji848] ambayo ni sawa na wastan wa 6500 -7000 kwa debe moja

Heka moja tuseme umevuna gunia 10[emoji23][emoji23]

Kwa hiyo 10 × 41500= 415000 sio??
Je hiyo heka moja mpaka unavuna hayo mahindi unafikiria hiyo 425K inatosha???
 
Piga hesabu ya bulk transport. Sasa gunia 10 unapeleka wapi? Wanachofanya watu ni wanajikusanya wanasafirisha in bulk kwa kulipia usafiri mmoja uliojaa mahindi tu.
 
Tabia za nchi maskini sana duniani kama Tanzania ni kufikiri kuwa chanzo kikuu cha mapato ya serikali ni wananchi. Ila ikumbukwe kuwa asilimia kubwa ya watanzania ni maskini, hivyo kufanya hivyo ni kuendeleza umaskini. Nchi maskini hutegemea zaidi mapato kutoka kweye sekta ya huduma (service) wakati serikali za nchi tajiri wanapata hadi 90% ya mapato yake kutoka sekta ya viwanda na si huduma.
Tunahitaji akili kubwa kubadili mwelekeo la sivyo tutabaki na serikali maskini, nchi maskini na wananchi maskini. Mwisho wa siku tutagemea misaada, mikopo hadi kuuza nchi. TAFAKARI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…