Nchi imepigwa nusu kaputi. Vikosi vya uokoaji vimefika eneo la tukio vikiwa mikono mitupu

Kuhusu elimu ya kujiokoa hii pasi na shaka ilitolewa kwani moja ya kanuni kabla ya kupaa lazima mpewe maelek3zo ya kujiokoa kwa dharura yoyote hadi majini
 
Sikitiko Kubwa Tanzania, Kama Viongozi Hawapo Vile
 
Binadamu bana! Nyie mnashangaa ya ndege ambayo ni bora imevutwa na Mitumbwi ya wavuvi. Rejea ajali ya kivuko cha ukara ambako wanajeshi walisitisha shughuli za uokozi mpaka kesho yake eti kisa giza limeingia

Nilibaki nimeduwaa na kujiuliza ni roho ngapi zimepotea kwa uzembe huo ambazo zingeweza kuokolewa
 
Nimejisikia vibaya sana kwa serikali kushindwa kuchukua hatua stahiki na muda muafaka ajari ilipotokea. Hapa kuna watu wanapaswa kuwajibishwa kuanzia ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa hadi wahusika wa mkoa ajari ilipotokea.
Hili si tukio la kwanza, tutajifunza baada ya miaka 100 ya uhuru?
 
Kuna kamjamaa kamoja kalikuwa kanapiga siasa kwa kusema watatumia vifaa vya tekinolojia ya hali ya juu kuokoa!
 
Kila ukipanda Ndege unaelezwa ikitokea Dharura kwenye maji ufanye nini.
Chini ya siti kuna lifejacket unalivaa ukilivaa unaelea hata kama hujui kuogelea.

Hao ziimamoto na uokozi leo jumapili wanakunywa bia zao, kwanini kuwabuguzi?
Mamako anaupiga mwingi
 
Kila ukipanda Ndege unaelezwa ikitokea Dharura kwenye maji ufanye nini.
Chini ya siti kuna lifevest unalivaa ukilivaa unaelea hata kama hujui kuogelea.

Hao ziimamoto na uokozi leo jumapili wanakunywa bia zao, kwanini kuwabuguzi?
Sio rahisi kama unavyofikiri lzm uwe vzr kisailojia na kimwili baada ya ajali ndio uweze kukumbuka hiyo life jacket, pia kwa ndege iliyotumbukia kwenye Maji life jacket itakusaidia ukiwa nje ya ndege ila kwa ndani itakufanya uelee juu ya ceiling ya ndege na ushindwe kuogelea kushuka chini kuipata milango ya kutokea during struggle unaishiwa nguvu wakati huo ndege inaendelea kujaa maji! Ripoti ya ajali ya ndege ya Ethiopia iliyokuwa imetekwa na vijana wa kiethiopia na kulazimisha iwapeleke Australia miaka ya 80's na kuangukia baharini kando ya visiwa vya Madagascar ilionyesha Kuna abiria walikufa wakiwa na life jacket kwa kuwa pulled up baada ya ndege kuzama majini na kushindwa kujiokoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…