Nchi ina kampuni 21 za kucheza kamari halafu uniambie tutakuwa na vijana jasiri na wapenda mabadiliko

kAzi ipo
 
Hahaha kamri ni MCHEZO? Kamari siyo mchezo huwezi kusema fulani ANACHEZA kamari. Ungekuwa ni MCHEZO ungekuwa chini ya wizara ya Utamaduni na Michezo.

Kamari ni kamari, siyo mchezo. Mbona hatuna ligi yake? Hatuna timu za kamari,Usituchanganye.
 
Mtu mweusi mahala popote ulimwenguni fikra zake zipo kwenye matumaini hewa (miujiza) na vitu vyepesi vyepesi tu ambavyo anaamini vinaweza kumsaidia kiuchumi. Hizi kampuni za kamari tunazionea bure tu. Ukizaliwa mtu mweusi jitahidi sana kutambua hilo na kuanza mchakato wa kuondokana na vinasaba hivyo mapema sana
 
Wewe unayebeti umefanya nini cha maana? Umeshinda hela ngapi?Umefanikiwa vipi tangu uanze kubeti? Betting ni kamari, ni dhambi.
Wewe usiyebet onyesha utajiri wako wa mabilioni Ili tuamini kama betting ni mbaya ukionyesha mabilioni Yako Mimi naacha betting Leo Leo ila kama huna hayo mabilioni fata maisha Yako hujaja na mtu duniani hapa
 
Kamari ni bomu kubwa katika TAIFA letu pia mtaji Kwa Wana siasa. Radio zote zimebadili madhumuni ya leseni zao ya kutoa habari na kuanza kutoa madhui ya betting.. kiongozi wao akiwa ni CLOUDS MEDIA,
 
Uingereza ina kampuni ngapi za kubet?..unataka mabadiliko gani?

Unalinganisha Prado na Bajaji....
Wenzetu Ulaya hufanya betting kama leisure wapate wasipate hawana cha kupoteza kwani huifanya kwa zile hela za ziada; Sisi vijana wetu masikini wanafikiri ni kazi ya kujiajiri, mwisho wa siku wanapoteza muda na hata kile kidogo walichokuwanacho .... matokeo yake wanakuwa hawana kitu na wamejikatia tamaa.....ni bomu tunatengeneza....
 
Ila kodi mnazitaka 🤣🤣🤣🤣
 
Ina shida kwa wachezaji kwani ina ushawishi sana na ni zaidi ya pombe nafikiri
Yaani huku kuna watu wanacheza mpaka hela za mikopo kwenye credit card zao
Wenye makampuni ndio wanafaidika sana na wanajilipa hela za kufuru
Pesa za kamari siku zote mwisho wake mmbaya!
Uliwahi kusikia stori huko ya yule mzenji aliyekuwa raia wa UK alishinda pesa nyingi sana kibongobongo alikuwa anamkaribia baresa lkn mwisho wa siku aliishiakuwa lofa
Angalia pia wale wanaoshinda ile lottery kubwa USA wengi wanaishiaa shimoni
Hizo pesa ni kama zina laanaa au

Labda ukizipata hutakiwi kuwa nanwenge kabisa

Ova
 
Kwa ufupi ni haram na haina faida yoyote kihivyo
Huyo mzenji nilimsikia na wengi zaidi
Kamari haina faida zaidi ya kuwa addicted tu na mwisho wake unakuwa kama mbwiya Unga tu
 
Watu walikaa wakafikiri njia Bora ya kuporana pesa bila kuumizana Wala kufikiana mwilini ni ipi 😂
 
Ni mwendo wa kucheza Kamari tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…