Nchi inaelekea kuwa ngumu sana kwa Rais Samia kuanzia sasa na baada ya 2025

Hali hii itazuiaje wakulima kuvutiwa kulima mazao ya biashara kama kahawa, pamba nk ambayo bei yake inatawaliwa na bei ya soko la dunia?
Wakulima wasaidiwe kutafutiwa namna ya kufurahia kazi yao.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Pamoja na watetezi wote wa kile kinachoendelea tena kwa makusudi wakitumia mamlaka tuliyowakabidhi kwa jeuri, kiburi na fedhuli ndiye atakuwa rais wa kwanza tangu nchi hii iwe huru kuvuliwa kinga na kushitakiwa kama raia yeyote yule kwa makosa yasiyodhaminika.

1. Hasira ya Mungu haipimiki kwa viganja vya mikono
2. Jeuri ya viongozi wa umma kwa wananchi ina ukomo na vitendo visivyomithilika
3. Kujali pesa kwa ajili ya familia zao huku raia akibangaiza haikubaliki popote
4.Uporaji viwanja kwa wananchi sehemu mbalimbali za nchi kupitia matajiri, wawekezaji na watumishi wasio waaminifu haikubaliki popote

Anguko la uflme linakuja kama dhoruba na tufali bahari watashika nyasi zinazoelea lakini hazitawaokoa kamwe
 
Kazi ni kubwa kwa uwezo wake, busara ni kutoendelea baada ya 2025 aggregate ya matokeo ya kazi ameleta uharibifu mkubwa ndani ya muda mfupi, kuliko mazuri.

‘Bi Tozo’ must go kwa faida yake mwenyewe na watanzania; kudra za mwenyezi mungu ziwe mwisho 2025 voluntarily.
 
Acha yamshinde aende zake, maana kimsingi UONGOZI UMEMSHINDA; watanganyika hatufurahishwi na anayoyafanya na tunamuomba Mungu / Allah aingilie kati.
 
Huu upepo tu utapita na maisha yataendelea

Ova
Ndio wanavyojidanganya na kumdanganya huyo maza ndio maana yupo kimya anasikilizia.

Ila hili la bandari halitapoa.

Mtaani kuna watu wengi wamesoma na hawana ajira wapo mtaani wamepigika vibaya.

Wana hasira mno kuona namna wakubwa wanavyojipigia tu huku wao wakiteseka.

Zile zama za kudanganyana hazipo tena.
 
Wewe labda Tanzania umehamia jana, hizo kelele za watanzania mitandaoni isikupe pressure ni nguvu za soda tu..........hata kabla ya December tutakua tunedandia tukio jingine.
Sio kabla ya December inaweza kuwa kabla ya August ila madhara ni makubwa na watanzania wanaendelea kufunguka.
 
Sikubaliani na hitimisho hili, pamoja na kwamba kuna mambo ninayokubaliana nayo katika mada nzima.

Haihitaji kuwa mbabe kuleta ufanisi wa utendaji serikalini.
Miongozo ya uendeshaji serikali upo, na hauzungumzii mahli popote kutumia ubabe.

Nafahamu, kwa uwezo alionao Rais Samia hawezi kusimamia kazi hiyo bila kutumia ubabe, na hata kutumia ubabe kama unavyoeleza.
 
Mnakuja na mada za kutisha mtazamo mzima wa serikali ukweli ni kwamba muda wenu umekwisha.

Your time is up. Mbinu zenu za kudanganya akili ya umma na kupotosha mipango ya kiserikali hapo bandarini ndio imefika mwisho.

Tunaweza kupata trilioni 26 kwa kutegemea tu pato la hapo TPA, hizi trilioni 7 za sasa ni matokeo ya wizi wa mafisadi wanaodhaminiwa na viongozi wakuu wastaafu.

Hakuna ugumu wowote kwa Samia kwani anachotaka kufanya ni kuleta mapinduzi makubwa sana ya kiuchumi ambayo hayajawahi kutokea.

Lakini wote tunaelewa kwamba kizuri kina gharama zake. Hata huu uzi wako ni sehemu tu ya gharama za kupambana nazo ili huo uzuri kamili uweze kupatikana.
 
Muda wa Samia na CCM ndo unakwisha hivyo.
 
Hiyo ya mahindi naunga mkono asilimia 200, haiwezekani kilo ya sembe ninunue 2500 wakat mahindi yanalimwa nchini hata ww ungekuwa Kiongozi ungefanya kama alichoamua Samia.
Ona hili jinga! Bia unanunua 3000 inategenezwa wapi?
 
Wewe unajua wazi kuwa wananchi hawana wabunge. Wengi wanaoitwa wabunge, ni wabunge wa jengo la bunge Dodoma. Hawakuchaguliwa na wananchi, na wala hawajihangaishi na wananchi. Hawawezi kuacha posho ya vikao Dodoma, waende huko kwa wananchi ambako hakuna posho, huku wanajua kuwa hata wananchi hawawataki.

Ukweli ni kwamva siyo kwamba Serikali inanunua kwa bei ya sh. 25,000 kwa gunia bali hakuna taasisi yoyote ya Serikali ambayo ipo huko vijijini kununua mahindi.
 
Hali hii itazuiaje wakulima kuvutiwa kulima mazao ya biashara kama kahawa, pamba nk ambayo bei yake inatawaliwa na bei ya soko la dunia?
Wakulima wasaidiwe kutafutiwa namna ya kufurahia kazi yao.
Mungu ibariki Tanzania.
Huko Njombe, baada ya kadhia hii, kila mkulima anasema aheri kulima parachichi. Kama wakulima wengi wakiamua kukikimbia kilimo cha mahindi, janga lake litakuwa kubwa kuliko lile la bei kubwa lililokuwa limeikumba nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…