Nchi inapoongozwa na aliyeko nyumbani, na aliyeko ofisini hajui cha kufanya

Kama ni vision ya kuhonga mali za taifa kwa wakwe na shemeji zake, nakubaliana na wewe.
Wakwe gani ndugu yangu, nipo jirani kabisa na nyumbani kwao mama mkapa, wala hamna cha sana unachoweza kusema wamepata kutoka kwake.

Vipi kwa lile daraja la Busisi si lilikua linaenda kwa wakwe wa fulani.

Turudi kwenye mada bro.
 
Wakwe gani ndugu yangu, nipo jirani kabisa na nyumbani kwao mama mkapa, wala hamna cha sana unachoweza kusema wamepata kutoka kwake.
Good to know that you're one of them. Ile asasi ya fursa sawa kwa wote iliishia wapi?
 
Magamba Matatu

Kwa nilichokisoma kwako una mahaba na Team EL pamoja na team Magu

Kiufupi mabadiliko ya sasa umeyachukia naamini tutapata majibu muda si mrefu
 
Usifanye mzaha kwenye hoja za maslahi ya nchi
 
ulishajiuliza kwa nini Upinzani uko na Samia kwenye kila kitu? Uliona wapi Dunia hii Opposition parties wanakubaliana na Serikali kwa 100% ?
Mkuu upinzani gani unazungumzia? upinzani wa Cuba au Tanzania?
 
Kumbe ni mrithi duuu
 
Naomba utusaidie ni nani anayemuandalia Rais hotuba/cha kusema mbele ya Hadhara.

Nimekuwa nasikiliza Kila tukio kubwa la Rais, jambo ambalo anaongea linakuwa limehaririwa kabisa, ila nimepata wasiwasi wa dhahiri kuwa muhariri wa hizi hotuba za Rais anaziharibu makusudi kabisa ili kuharibu taswira ya Rais mbele ya watu wake.
 
nyie mlioteuliwa na magu ndiyo mnazingua, hamtaki mguswe, wala upigaji wenu uguswe

akishaelewa hili, na kifanya rishafo ndiyo utaelewa
Unajua upigaji au unafanya majaribio
 
watajua hawajui...wapo wapuuzi watakubishia ...kila mkoa,wilaya,kata/kijiji si wanaume wala wanawake wanasema hakuna rais hapo

na tulionya mapema sana huyu mama akienda na watu wa msoga itakula kwake hakuna watu wanaochukiwa na wananchi kama hao (msoga) sababu ni utawala wao ulijaa kila aina ya ufisadi na nchi kudidimia kweli kweli

kuna kikundi cha watu wachache ambacho kimo hata humu kazi yake ni kumpamba samia kwa uongo kuwa yupo kwenye njia sahihi...atakuja kushtuka too late sana
 
Mmi ni mgen JF ila mwamba huyu anaonekana ni GREAT THINKER.....pia yupo kweny system kila kinachoendelea anajua.


........shikamoo jf
 
Waache wafu wazike wafu wao...kifo cha CCM ndiyo ukombozi wa pili wa nchi hii......hata kama itaongozwa na hao waliopo CCM leo bado mabadiliko yatakuwa chanya kwa mstakabali wa taifa.

Ni bora kulumbana ndoa ikavunjika tukalazimika kumposa binti mwingine na kulipa mahari 2×2.
 
Mama alivyokuwa anapangua wateule wa Hayati Magufuli haraka haraka utadhani alikuwa na taarifa za kiintelinjesia kuwa Magufuli atafufuka tena hivyo jamaa wakamwambia apindue meza haraka ili jamaa akiamka akute mambo mapya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…