Nchi kumi za kutembelea katika kipindi cha miaka mitano

Aisee mm Namibia ndo nchi naham sana nikaitembelee nchi kubwaaa harafu watu kiduchu.Nimetokea kuipenda tu ile nchu japo sehem kubwa ni jangwa ila ni nchi poa sana maana hua naangalia sana youtube.Mungu ani bless nikatimize ndoto zangu.
Yes mkuu Namibia ipo super, Windhoek jiji dogo ila lipo safi sana, wajerumani waliijenga vema,tembelea pia Katutura township, walvis bay(bandari hii ni mshindani wetu,Dar Port),katima mulilo, Rundu, etc etc ,na nchi ipo peace ya kweli SIO YA LAZIMA
 
Hapo labda DUBAI, uturuki na china(macau) huko tutaenda sote
ila haswa haswa nina mpango wa kwenda Brazil, hapa unisamehe sintokwenda na wewe..
Hata mimi sitaki safari yoyote ya kwenda na wewe🤣🤣🤣
 
Wiki mbili za mwanzo za mwaka ujao 2024 nimepanga kuchukua likizo fupi itakayoniwezesha kutembelea nchi jirani tatu.
Nitaanza na Bujumbura Burundi, nivuke DRC- Bukavu na Goma, Kisha nirudi kupitia Kigali Rwanda.
Mwaka 2025 nimepanga kutembelea Namibia na Zimbabwe. Inshallah!.
 
Kabla ya kwenda nje ya Tanzania natamani nimalize kuizinguka Tanzania yote Kwa gari binafsi.
Napenda kusafiri safari ndefu kuliko kitu kingine chochote duniani huwa moyo wangu unapata Amani sana
Upo kama mimi, napenda kusafiri sana kuijua nchi yangu kwanza halafu huko kwingine nitaenda tu
 
Hata mimi sitaki safari yoyote ya kwenda na wewe🤣🤣🤣
Ewaa, AFAZALI...
😂😂

kanuni za kutembea, bar, club au kusafiri kwenda kula burudani huendi na mchumba, usije kosa mambo mazuri huko buree😂🤣
 
Kuna nini cha kwenda kutalii Nigeria?

Kwenye hiyo list naondoa Nigeria na Canada naweka Madagascar na Brazil
Muda ukiruhusu, nitapenda kukaa Nigeria kwa muda kama mwezi mmoja hivi. Nataka nijue siri ya wao kutapakaa dunia nzima kwa wingi.

Wakenya ni wajasiri, lakini nafikiri Wanigeria wametia fora.
 
Wewe umetisha sanaaa!! Kama umebakiza mikoa miwili Tanzania umejitahidi Sana na Una haki ya kusafiri nje ya nchi..
Mimi bado mikoa mingi Sana sijafika hasa nyanda za juu kusini iringa,mbeya na songea Ila Kwa mikoa ya kusini naijua vichochoro vyote
 
We umetembelea ipi kati ya hizo? Au Copy and paste? Oga
 
Wewe umetisha sanaaa!! Kama umebakiza mikoa miwili Tanzania umejitahidi Sana na Una haki ya kusafiri nje ya nchi..
Mimi bado mikoa mingi Sana sijafika hasa nyanda za juu kusini iringa,mbeya na songea Ila Kwa mikoa ya kusini naijua vichochoro vyote
Ni hatua! Kama ingelikuwa ni darasa, nina uhakika umeshavuka level ya kalamu ya mkaa na sasa unatumia ya wino.
 
Wewe umetisha sanaaa!! Kama umebakiza mikoa miwili Tanzania umejitahidi Sana na Una haki ya kusafiri nje ya nchi..
Mimi bado mikoa mingi Sana sijafika hasa nyanda za juu kusini iringa,mbeya na songea Ila Kwa mikoa ya kusini naijua vichochoro vyote
Siyo Tanzania mkuu, bali upande wa bara pekee. Pemba bado sijatia mguu kiongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…