Nchi kumi za kutembelea katika kipindi cha miaka mitano

Nchi kumi za kutembelea katika kipindi cha miaka mitano

Sio vibaya kuwa na ndoto za kuiona Dunia
Binafsi nimejaza passports Tatu na ya nne inaenda page ya 12

Nimetembelea nchi nyingi sana mpaka sina tena ile shauku ya kutamani bali ni kukata ticket tu na kwenda ninapoamua kwenda
Kuna jamaa kaniomba nikamtembelee Toronto
Niagara falls ndio lengo
 
Natamani ningekuwa mpenzi wa mpira, nilipewa ticket nikaikataa kwenda kuangalia mechi Walahi
Hivi hatuwezi kukupiga fine! Kwa nini hukuielekeza kwangu hiyo ofa mkuu? Japo siyo mshabiki wa mpira, lakini ningepewa hiyo ofa nisingeisusa. Ningeenda kama shabiki lakini ningeishia kujisomea zangu kakitabu kazuri huku mpira ukiendelea. Kwani kuna mtu angeniuliza kwa nini siufuatilii mpira unaendelea uwanjani?

Siku nyingine ukipewa uniuzie, japo nitakupa jela ya "soda" tu😂
 
Sio vibaya kuwa na ndoto za kuiona Dunia
Binafsi nimejaza passports Tatu na ya nne inaenda page ya 12

Nimetembelea nchi nyingi sana mpaka sina tena ile shauku ya kutamani bali ni kukata ticket tu na kwenda ninapoamua kwenda
Kuna jamaa kaniomba nikamtembelee Toronto
Niagara falls ndio lengo
👏👏👏🙏
 
Muda ukiruhusu, nitapenda kukaa Nigeria kwa muda kama mwezi mmoja hivi. Nataka nijue siri ya wao kutapakaa dunia nzima kwa wingi.

Wakenya ni wajasiri, lakini nafikiri Wanigeria wametia fora.

Jibu unalo, Nigeria ni nchi inayotoshana na Tanzania kwa ukubwa ilhali hiyo Nigeria ina watu milioni 218 huku Tanzania ikiwa na idadi ya watu milioni 67, yaani wingi wa Wanijeria ni mara nne ya Watanzania, hivyo usishangae kwanini wametapakaa.
 
🙏🙏🙏
 
Aisee mm Namibia ndo nchi naham sana nikaitembelee nchi kubwaaa harafu watu kiduchu.Nimetokea kuipenda tu ile nchu japo sehem kubwa ni jangwa ila ni nchi poa sana maana hua naangalia sana youtube.Mungu ani bless nikatimize ndoto zangu.
Mimi nina rafiki yangu huko aliniambia nimtumie nauli aje Bongo
 
Dar, mwanza na arusha

Afu kwa nini umeifanya USA ya pili kutoka mwisho?
Dar, Mwanza na Arusha! Hiyo nayo pia ni hatua.

Safari moja ni chanzo cha safari nyingine.

Nimeiweka USA na Canada mwishoni kwa makusudi.

Nimeelezwa na wazoefu kuwa ni changamoto kupata viza, lakini passport ikiwa na "muhuri" mingi inaweza ikawa rahisi kukubalika.

Nimejaribu kufikiri kuwa wakiona kuwa nimeshafika DUBAI, CHINA, UGIRIKI, UTURUKI, ISRAELI na UINGEREZA, ni rahisi kunikubalia kuitembelea nchi yao.
 
Ulaya
1. Netherlands (huku napenda zile water canals zake)
2. Spain (mitaa ya miji mikongwe ya f , Sevilla)
3. Portugal (sababu kama ya Spain)
4. North Europe (nchi yeyote isiyo na sunset)

Asia
1. Japan (huku nataka kwenda shangaa magorofa tu)
2. Nepal (kuna mshikaji wangu chuo alikuwa ni Mnepal, jamaa wana roho nzuri kama wabongo)

Afrika
1. Angola (nasikia kuna ngozi nzuri sana huku 😁😁😁)
2. Cape Verde (sababu kama ya Angola)

Amerika ya Kusini
1. Peru (kuna mchuchu mmoja naye tuliskomga naye chuo alikuwa anatokea huku, alikuwa na roho nzuri hii ikanifanya niamini watu wa huku wako poa)
2. Chile

Amerika ya Kaskazini.
1. Hawaii
2. Nova Scotia
 
Tulia basi dada
Mkeo ana hekaheka 🤣🤣🤣
Hivi zile talaka ulitoa zote tatu?
Au moja talaka rejea?

Km moja bora uchane kuna tajiri uko anamnyapia atambeba mazima umkose 🤣
 
Mkeo ana hekaheka 🤣🤣🤣
Hivi zile talaka ulitoa zote tatu?
Au moja talaka rejea?

Km moja bora uchane kuna tajiri uko anamnyapia atambeba mazima umkose 🤣
Sina mke jf tuheshimiane, tafadhali😂
 
Aisee mm Namibia ndo nchi naham sana nikaitembelee nchi kubwaaa harafu watu kiduchu.Nimetokea kuipenda tu ile nchu japo sehem kubwa ni jangwa ila ni nchi poa sana maana hua naangalia sana youtube.Mungu ani bless nikatimize ndoto zangu.
Kila la kheri mkuu!
 
Sera yangu ni kuzimiza nchi zote jirani na Tanzania Kisha nitaenda hizi nchi ;

Djbout
Ethiopia
Estonia

Huko nitaacha watoto
 
Umepanga kutembelea nchi ngapi katika kipindi cha miaka 5 ijayo?

Binafsi, ninapenda sana kusafiri, lakini kwa sababu ya kiwango cha kipato, bado sijazimaliza hata nchi za Afrika Mashariki.

Mpaka sasa, nchi nilizokwishatia miguu yangu ni Kenya, Uganda na Burundi.

Ikimpendeza Mungu, mwishoni mwa mwaka huu nitaenda Rwanda na South Africa.

Kwa sababu safari ya South Africa itakuwa kwa basi, nitaweza kupitia nchi kadhaa, labda Zambia, Zimbabwe, n.k. Bado sijaamua route, lakini huenda nikaenda kwa basi nikarudi kwa ndege, au vinginevyo.

Kwa hiyo, nimeziengua Rwanda na S. A kwenye nchi za kuzitembelea katika miaka mitano ijayo. Ninahesabu nimeshazitembelea.

Hizi ndizo nchi nitakazozitembelea katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2024:
1. Misri

2. Nigeria

3. Dubai - ( UAE)

4. Israel

5. Ugiriki

6. Uturuki

7. China

8. Uingereza

9. Marekani

10. Canada.

Natamani kwamba ifikapo Disemba 2028, niwe nimeshazitembelea nchi zote hizo hapo juu, na zaidi, ikiwezekana.

Wewe umepanga kutembelea nchi zipi?
Binafsi napendelea kusagiri Nchi za Africa Kwa Sasa badala ya Ulaya.

Nimefika Nchi zote za Kenya,Uganda,Malawi na Zambia.

By 2028 nafikiria niwe nimefika Botswana,Angola,Ivory Coast,Ethiopia,Senegal,Egypt na Ghana.
 
Back
Top Bottom