Nchi kumi za kutembelea katika kipindi cha miaka mitano

Nchi kumi za kutembelea katika kipindi cha miaka mitano

Umepanga kutembelea nchi ngapi katika kipindi cha miaka 5 ijayo?

Binafsi, ninapenda sana kusafiri, lakini kwa sababu ya kiwango cha kipato, bado sijazimaliza hata nchi za Afrika Mashariki.

Mpaka sasa, nchi nilizokwishatia miguu yangu ni Kenya, Uganda na Burundi.

Ikimpendeza Mungu, mwishoni mwa mwaka huu nitaenda Rwanda na South Africa.

Kwa sababu safari ya South Africa itakuwa kwa basi, nitaweza kupitia nchi kadhaa, labda Zambia, Zimbabwe, n.k. Bado sijaamua route, lakini huenda nikaenda kwa basi nikarudi kwa ndege, au vinginevyo.

Kwa hiyo, nimeziengua Rwanda na S. A kwenye nchi za kuzitembelea katika miaka mitano ijayo. Ninahesabu nimeshazitembelea.

Hizi ndizo nchi nitakazozitembelea katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2024:
1. Misri

2. Nigeria

3. Dubai - ( UAE)

4. Israel

5. Ugiriki

6. Uturuki

7. China

8. Uingereza

9. Marekani

10. Canada.

Natamani kwamba ifikapo Disemba 2028, niwe nimeshazitembelea nchi zote hizo hapo juu, na zaidi, ikiwezekana.

Wewe umepanga kutembelea nchi zipi?
"Pumbavu mkubwa wewe, jioni ya leo ninakuja kuchukua hela yako"
 
Kabla ya kwenda nje ya Tanzania natamani nimalize kuizinguka Tanzania yote Kwa gari binafsi.
Napenda kusafiri safari ndefu kuliko kitu kingine chochote duniani huwa moyo wangu unapata Amani sana
Nina wazo kama lako ila Kwa kutumia kibao Cha mbuzi , maybe baadae Nita upgrade na kutoka nnje ya bongo

images - 2023-09-26T162258.806.jpeg
 
Back
Top Bottom