Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Hivi hatuwezi kukupiga fine! Kwa nini hukuielekeza kwangu hiyo ofa mkuu? Japo siyo mshabiki wa mpira, lakini ningepewa hiyo ofa nisingeisusa. Ningeenda kama shabiki lakini ningeishia kujisomea zangu kakitabu kazuri huku mpira ukiendelea. Kwani kuna mtu angeniuliza kwa nini siufuatilii mpira unaendelea uwanjani?Natamani ningekuwa mpenzi wa mpira, nilipewa ticket nikaikataa kwenda kuangalia mechi Walahi
👏👏👏🙏Sio vibaya kuwa na ndoto za kuiona Dunia
Binafsi nimejaza passports Tatu na ya nne inaenda page ya 12
Nimetembelea nchi nyingi sana mpaka sina tena ile shauku ya kutamani bali ni kukata ticket tu na kwenda ninapoamua kwenda
Kuna jamaa kaniomba nikamtembelee Toronto
Niagara falls ndio lengo
Muda ukiruhusu, nitapenda kukaa Nigeria kwa muda kama mwezi mmoja hivi. Nataka nijue siri ya wao kutapakaa dunia nzima kwa wingi.
Wakenya ni wajasiri, lakini nafikiri Wanigeria wametia fora.
🙏🙏🙏Jibu unalo, Nigeria ni nchi inayotoshana na Tanzania kwa ukubwa ilhali hiyo Nigeria ina watu milioni 218 huku Tanzania ikiwa na idadi ya watu milioni 67, yaani wingi wa Wanijeria ni mara nne ya Watanzania, hivyo usishangae kwanini wametapakaa.
Nikifika South Korea, nitajitahidi niunganishe hadi North Korea.South Korea na China.
Mimi nina rafiki yangu huko aliniambia nimtumie nauli aje BongoAisee mm Namibia ndo nchi naham sana nikaitembelee nchi kubwaaa harafu watu kiduchu.Nimetokea kuipenda tu ile nchu japo sehem kubwa ni jangwa ila ni nchi poa sana maana hua naangalia sana youtube.Mungu ani bless nikatimize ndoto zangu.
Dar, Mwanza na Arusha! Hiyo nayo pia ni hatua.Dar, mwanza na arusha
Afu kwa nini umeifanya USA ya pili kutoka mwisho?
🤣🤣Fujo zingine, du😂😂😂
Mkeo ana hekaheka 🤣🤣🤣Tulia basi dada
Sina mke jf tuheshimiane, tafadhali😂Mkeo ana hekaheka 🤣🤣🤣
Hivi zile talaka ulitoa zote tatu?
Au moja talaka rejea?
Km moja bora uchane kuna tajiri uko anamnyapia atambeba mazima umkose 🤣
Kila la kheri mkuu!Aisee mm Namibia ndo nchi naham sana nikaitembelee nchi kubwaaa harafu watu kiduchu.Nimetokea kuipenda tu ile nchu japo sehem kubwa ni jangwa ila ni nchi poa sana maana hua naangalia sana youtube.Mungu ani bless nikatimize ndoto zangu.
Penye nia pana njia.London Uingereza, I wish siku moja nipate nafasi ya kuangalia live game ya Arsenal pale Emirates Stadium
Binafsi napendelea kusagiri Nchi za Africa Kwa Sasa badala ya Ulaya.Umepanga kutembelea nchi ngapi katika kipindi cha miaka 5 ijayo?
Binafsi, ninapenda sana kusafiri, lakini kwa sababu ya kiwango cha kipato, bado sijazimaliza hata nchi za Afrika Mashariki.
Mpaka sasa, nchi nilizokwishatia miguu yangu ni Kenya, Uganda na Burundi.
Ikimpendeza Mungu, mwishoni mwa mwaka huu nitaenda Rwanda na South Africa.
Kwa sababu safari ya South Africa itakuwa kwa basi, nitaweza kupitia nchi kadhaa, labda Zambia, Zimbabwe, n.k. Bado sijaamua route, lakini huenda nikaenda kwa basi nikarudi kwa ndege, au vinginevyo.
Kwa hiyo, nimeziengua Rwanda na S. A kwenye nchi za kuzitembelea katika miaka mitano ijayo. Ninahesabu nimeshazitembelea.
Hizi ndizo nchi nitakazozitembelea katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2024:
1. Misri
2. Nigeria
3. Dubai - ( UAE)
4. Israel
5. Ugiriki
6. Uturuki
7. China
8. Uingereza
9. Marekani
10. Canada.
Natamani kwamba ifikapo Disemba 2028, niwe nimeshazitembelea nchi zote hizo hapo juu, na zaidi, ikiwezekana.
Wewe umepanga kutembelea nchi zipi?