Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiongozwa kidemokrasia

demokrasia sio tatizo, tatizo kubwa la nchi za kiafrika ni sera mbovu za kiutawala, kiuchumi, kielimu na nk...

hata leo tukikubali kuwa na sera za kitaifa zisizofungamana na uccm katika kila nyanja maendeleo yatakuja haraka
 
Sikweli kuendesha nchi siyo kama familia tena wengine wanazikimbia familia
 
Natamani nikjweke ndani ili nione matokeo ya demokrasia.
 
demokrasia sio tatizo, tatizo kubwa la nchi za kiafrika ni sera mbovu za kiutawala, kiuchumi, kielimu na nk...

hata leo tukikubali kuwa na sera za kitaifa zisizofungamana na uccm katika kila nyanja maendeleo yatakuja haraka
Sera mbovu ambazo siyo shirikishi waonazitunga, hawana uelewa wa nini hatima ya hizo Sera
 
demokrasia sio tatizo, tatizo kubwa la nchi za kiafrika ni sera mbovu za kiutawala, kiuchumi, kielimu na nk...

hata leo tukikubali kuwa na sera za kitaifa zisizofungamana na uccm katika kila nyanja maendeleo yatakuja haraka
Sera mbovu, ambazo siyo shirikishi, waonazitunga hawana uelewa wa nini hatima ya hizo Sera
 
Mkuu Kama utaikataa demokrasia ebu tuweke wazi ni mfumo gani utatumika kuwapata viongozi wa nchi?

Nchi nyingi za Afrika hazina demokrasia lakini ndo nchi masikini za kutupwa kutwa viongozi kupanda ndege kwenda ulaya na Marekani kutembeza bakuri kwa mabeberu hili utalizingumzia vipi?

Ubovu wa sera chanzo ni demokrasia au aina ya viongozi tulio nao kutwa kuwaza uchaguzi sio kutatua shida za nchi kupitia sera bora
 
Wanasiasa wanatengeneza Sera kufanya sisa
 
Mbona Tanzania tulishindwa kuendelea tukiwa katika mfumo wa chama kimoja Kama Russia na China ?
 
Fanya kazi ,acha kupiga siasa.
 

Misri uliwahi kufika karibuni? Hilo rumba lilioko ni afadhali ya TZ mara 10

Hiyo Morocco ndiyo usitaje, vijana wanafika kuogelea kwenda Europa,
Ni hatari
 
Of course ukiwa upande mmoja wa shilingi lazima utaona mtiririko wangu kuwa very contradicting.

Upande mwingine wa shilingi ni kwamba wewe unaichukulia Tanzania kama independent state na inamaamuzi ya rasilimali zake A to Z kwa manufaa ya watu wake kitu ambacho si kweli, ni vita ya dunia kunyang’anyana rasilimali kwa namna yeyote ile ilimradi mwenye mabavu apate kwanza wanyonge waambulie masalia, wakati mwingine mpaka masalia (mfano makinikia) husombwa bure bure kabisa.

Wahenga husema kheri nusu shari kuliko shari kamili, sio kwamba kwa sasa hatupigwi ndani ya chama kimoja, trust me, kwa mfumo wa vyama vingi tayari nchi I nakuwa ime-entertain adui kuwa na access ya ndani kabisa mpaka chumbani ikibidi endapo kukawa na mbadilishano wa madaraka, let say leo Mbowe na Chadema nzima wakashika nchi, CCM wakiwa wapinzani, kwa kutumia ushawishi ambao bado watakuwa nao Jeshini, usalama wa taifa, polisi na kwenye idara mbalimbali zilizo nyeti, tutapigwa na wazungu kiulaini kuliko nguvu nyingi za ushawishi zinazotumika sasa. Pia ni rahisi kwa vikundi vya kiasi kuibuka, kuwa na nguvu kubwa na hata kufanya yasiyoelezeka.

Ulaya wao wamewekeza sana kwenye nguvu za kijeshi, ujasusi, ushawishi kwenye organizations kubwa walizoziasisi wao wenyewe hivyo kuwa na uhakika wa ulinzi na ndio maana ni ngumu kusikia vita vya waasi uingereza, Marekani, ufaransa, uswisi, Ujerumani, Italy na kwengineko. Pia kamwe mtoto wa baba mwizi wa mali za watu hawezi ishi maisha ya mtoto wa machinga, lazima kuwepo na tofauti kubwa na pia aggressiveness lazima iwe tofauti na ndio maana waafrica popote duniania tunamalizana wenyewe kwa wenyewe maana tumetengenezewa mazingira magumu ya survival.

Sisi bado wachanga sana kimifumo ya uongozi wa kimagharibi, Ghana kwa mfano, ndio nchi ambayo inasifika sana Africa kwa demokrasia, sidhani kama inaweza kuisogelea South Africa katika Maendeleo ya kiuchumi nchi ambayo imekwenda kidikteta mpaka miaka ya tisini.
 
Inaweza. Kabisa.
 
Ndugu yangu Katiba na sheria tulizojiwekea wenyewe ni muhimu zikafuatwa na katiba ndio mkataba wetu kati ya watawala na watawaliwa ndio the mother law of all laws, sasa ni muhimu kuifuata kwa kujali rule of law, kujali haki za binadamu.

Mfaransa, Mmarekani na Muingereza hawana uhusiano na watu kutokuheshimu katiba, tukirudi kwa mtoa mada yeye uelekeo wake ni katika kuhimiza udikteta sasa madikteta huwa hawana macho ya kuona mbele na ndio maana mwisho wao huwa ni mbaya. Sisi kama Tanzania tunashukuru kwamba viongozi wetu wamekuwa wakiheshimu rule of law na kuheshimu katiba.

Kama ni accumulation of wealth ni vyema tukajipanga katika economic espionage, tufufue viwanda na ikiwezekana tuwe na watu wetu ambao wanaweza kwenda kwa washindani wetu na kutupatia taarifa muhimu na ikibidi kufanya mambo ambayo yatatusaidia kama nchi kupenya katika masoko ya washindani, tukianza na ukanda wetu yaani nchi jirani na watu wao kila kitu watakachotumia (Bidhaa,madawa,huduma za kifedha,elimu,usafiri wa anga,ardhini na kwenye maji, nishati ya umeme etc) kiwe kimepita kwenye mikono yetu na kutuachia madollar.

Tuna ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo tulime tuprocess tuilishe dunia tupate madollar sio kukaa hapa na kuhubiri viongozi wawe madikteta.

#Mama 2025.
 
Ukisikia mtu kuwa mjinga, hii ndiyo maana halisi.

Huyu haelewi hata maana ya maendeleo. Hajui kuwa demokrasia ni sehemu ya maendeleo. Hajui kuwa hata katika kanda hii ya Afrika, nchi yenye maendeleo mazuri ya kiuchumi ni Botswana, na Botswana ni kati ya nchi zinazoongoza kwa maendeleo ya demokrasia.

Huyu mjinga hajui kuwa North Korea ilikuwa kwenye hali bora zaidi kuliko South Korea miaka ya 40, lakini udikteta wa North Korea umeifanya hicho hiyo kutopea kwenye umaskini wa kiuchumi ukilinganisha na South Korea yenye demokrasia.

China ilikuwa sawa na Japan, miaka 60, lakini leo Japan ni tajiri maradufu ya China yenye udikteta, tena hali ya China imekuwa afadhali sasa baada ya kuondokana na udikteta ule uliotopea. Leo Japan ni nchi ya 19 katika human development, China ni nchi ya 86, ikizidiwa na hata ya baadhi ya nchi za kiafrika.

Pia linganisha maendeleo ya Hong Kong yenye demokrasia tele na China yenye udikteta. Leo hii Hong Kong na Netherlands ndizo zinazoongoza kuwekeza nchni China.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…