Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiongozwa kidemokrasia

Mapinduzi ya viwanda, ambayo ndiyo yameziletea nchi nyingi hizo maendeleo yalitokea kipindi zinaongozwa kifalme. Ni bora tuseme ufalme ndiyo umeziletea nchi hizo maendeleo. Kuhusianisha maendeleo ya nchi hizo na demokrasia ni kupotosha. Na hapa siyo nilete mifano ya nchi zilizoendelea kwa udikteta, nilete mifano ya nchi zilizoendelea bila demokrasia, hizo ni nyingi sana kiasi kwamba ni kama vile unahitaji kutokuwa na semokrasia ili kuendelea.
 
 

Attachments

  • VID-20211001-WA0001.mp4
    2.2 MB
South Korea kwani haiheshimu Demokrasia? Miaka ya 60 kiuchumi hawa walikuwa sawa kabisa na Tanzania zikiwemo Singapore, Indonesia na Malaysia na wao hawana utajiri mkubwa kama Tanzania wa Rasilimali lakini angalia walivyotuacha mbali kimaendeleo.
South Korea imeacha kuongozwa na wanajeshi kama mwaka wa tisini hivi. Ukuaji wote wa maana wa uchumi, makampuni yote ya maana ya South Korea yalizaliwa wakati huo.
 
Mapinduzi ya viwanda bila kuwa na Serikali za Kidemokrasia ili kuhakikisha uhuru na haki ya raia, vyama vya siasa, vyombo vya habari na pia Wafanyakazi kutendewa haki unadhani kungekuwa na maendeleo? Serikali iliyo madarakani ikivurunda Wananchi wanaipiga kibuti na kuweka Serikali mpya na wao wakivurunda Wananchi wanaiondoa madarakani. ACHA DHARAU ZAKO DHIDI YA DEMOKRASIA.

 
South Korea kuna chaguzi huru na haki na Bunge lao kama halina imani na Kiongozi wa nchi wanampigia kura ya kutokuwa na imani naye hivyo kunakuwa na uchaguzi mpya wakati kuna mtu anakaimu.

South Korea imeacha kuongozwa na wanajeshi kama mwaka wa tisini hivi. Ukuaji wote wa maana wa uchumi, makampuni yote ya maana ya South Korea yalizaliwa wakati huo.
 
On May 10, 1948, the first general election was held in a democratic manner in South Korea under the UN’s supervision to elect the 198 members of the National Assembly. In July of the same year, the Constitution was enacted and Rhee Syngman and Yi Si-yeong, two independence fighters deeply respected by Koreans, were elected as the country’s first President and Vice President, respectively. On August 15, 1948, the Republic of Korea (ROK) was formally established as a liberal democracy, which inherited the legitimacy of the PGK. The UN recognized the government of the ROK as the only legitimate government on the Korean Peninsula.


South Korea imeacha kuongozwa na wanajeshi kama mwaka wa tisini hivi. Ukuaji wote wa maana wa uchumi, makampuni yote ya maana ya South Korea yalizaliwa wakati huo.
 
Vipi kuhusu nchi yenye uchumi wa kati ?
 
Kuna mambo mengi sana yanayo husishwa na demokrasia ila vitu muhimu kuliko vyote ni uwepo wa uchaguzi kila baada ya muda flani, uhuru wa vyombo vya habari na uhusishaji wa wananchi katika uendeshaji wa nchi yao. Sababu hizo zina sababisha kuwepo kwa aina mbili za demokrasia

1. Liberal democracy: Demokrasia ambayo kweli inazingatia kuwepo kwa uchaguzi, uhuru wa vyombo vya habari na uhusishaji wa wananchi katika maamuzi ya serikali
2. Illiberal democracy: Aina hii ya demokrasia inaruhusu uwepo wa chaguzi mbali mbali ila vyombo vya habari vinaweza visiwe na uhuru wa kutosha na wananchi mara nyingi hawaruhusiwi kushiriki kwa njia moja au nyingine katika uendeshaji wa nchi yao haswa kwa kutoa maoni. Kwa bahati mbaya au nzuri, Tanzania ni mfano wa nchi iliyo adopt aina hii ya demokrasia ambayo haina tofauti sana na udikteta.

Ili demokrasia ya ukweli (Liberal democracy) iweze kuzaa matunda haswa katika nchi zinazo endelea, lazima wananchi wawe na uelewa mkubwa wa mambo ya kiserikali ili kuwa wezesha wao kufanya maamuzi sahihi katika kila chaguzi au kutoa maelekezo sahihi katika kila kura ya maoni. Sababu ya umma kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mambo mengi ya serikali ni sababu kubwa inayoweza kusababisha mfumo huu kutokuwa na manufaa. Sababu zingine ni pamoja na urasimu katika kufanya maamuzi ambayo yana onekana kuwa sahihi na vyombo vya habari kutumiwa vibaya na kusababisha maafa makubwa kama vile mapinduzi au hata vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tofauti na illeberal democracy iliyopo Tanzania, kitu ambacho mtoa mada anajaribu kuelezea kinaitwa "Benovelant dictatorship". Mfumo huu unahusisha serikali kuhakikisha kwamba maamuzi yote yanafanywa baada ya uchunguzi wa kina mpaka kufikia hatua ambayo wana uhakika kwamba kila kitu ni sahihi. Mtu mmoja au wachache sana ndio wanao husika katika uendeshaji wa nchi na kutoa maamuzi sahihi kila wakati. Hii ni kama kuwa na "A very good dictator".
 
Bongo hakuna demokrasi ni wizi wa kura na ufisadi kwa kwenda mbele na kilichopo ni umaskini uliokithiri tuu, bongo kungekuwa na maendeleo ningekuelewa, inaonekana watu mlivyopigika mmeanza kuamini njaa zenu zinatokana na demokrasi
 
Nadhani ungetoa mifano ya nchi zilizoendelea kipindi zikiwa na Demokrasia hiyo unayoisema ingekuwa unaeleweka vinginevyo unaongea porojo tu.

Nakubaliana nawe kuwa Demokrasia ni muhimu sana kwenye Maendeleo (hii Demokrasia ya kileberali), lakini ili hii Demokrasia ifanye kazi ni lazima wananchi wawe na elimu ya kutosha na uwezo mkubwa wa kifedha—yote yanahitaji Maendeleo makubwa ya kiuchumi ya nchi ambapo middle class itakuwa kubwa na yenye kuweza kufanya maamuzi bila kupewa vipande vya kanga na t-shirt. Hivyo INAANZA MAENDELEO YA KIUCHUMI KISHA INAFUATA DEMOKRASIA YA KILIBERALI.

Nakupa mfano, ambao umeupotosha sana wa Korea Kusini. General Park alipoingia Madarakani miaka ya 1960 alifuta Demokrasia hii tunayoijua na chaguzi zilifanyika kiini macho tu, ndani ya muda wake mwaka 1973 aliinzisha sera iliyoitwa Heavy and Chemical Industrialization (HCI) programme. Kwenye program hi ili ifanikiwe alifanya haya—alilinda viwanda vya ndani vichanga (kwa kushirikiana na sekta binafsi), alivipa ruzuku, aliweka tarrifs kubwa kwa bidhaa za nje shindani na bidhaa za ndani, sheria ya hakimiliki aliipuza ili kuchochea wizi wa bidhaa za nje na uigaji ambao ulikuza ubunifu na kuendeleza teknolojia kwa kasi kubwa, kilikuwa ni kipindi chenye upinzani mkubwa kutoka mataifa na makampuni shindani ya nje na yaliyojaribu kuhujumu jitihada hizi na pia kelele za raia ndani na wanasiasa ndani zilikuwa nyingi ndio akaminya vyama shindani, akaminya vyombo vya habari. Hatimaye kufikia mwaka 1981, lengo lake la kufikia pato la raia la dola 1,000 likafikiwa. Hii ilizaa middle class kubwa na automatically demand ya haki za kiraia na kisiasa ikawa kubwa na sustainable. So kwa mfano wa Korea kusini, ni Maendeleo ya kiuchumi ndio yanazaa liberal democracy na sio kinyume chake.

Imetokea hili kwa Singapore, Taiwan, Vietnam, China n.k.

Tatizo la Afrika, madikteta wote waliwekwa aidha na Marekani kuiba kama kina Mobutu, au Wasoviet kama kina Dos Santos ambao walikuwa na sera mbovu za uchumi na hawakua na malengo yoyote ya kiuchumi kwa nchi zao, tofauti na watu kama kina General Park.
 
South Africa Demokrasia yao ni ya kutengeneza machoni tu, ila kiuhalisia wanaoitawala bado ni makaburu na ndio maana imepiga hatua hivyo. Weusi wamepewa siasa, wazungu wakabaki na uchumi na hapo ni baada ya wazungu kutengeneza mifumo ya namna ya kuiongoza nchi. Mtu mweusi mpe madaraka, chakula, pombe na mwanamke baasi. Blacks wengi south wanaishi kwa kutumia credit cards - gari kwa mkopo, chakula supermarket kwa mkopo, furniture kwa mkopo, shule kwa mkopo, pombe mkopo, nyumba mkopo yaani kila kitu ni credit card...maisha yao wameyaweka rehani kwa makaburu.
 
Uwezo wako wa kufikiri ni mkubwa na wangi wanauwezo mdogo wa kufikiri kwa sababu ukitaja tu democrasia mtu anawaza kachama kake.

Nakushauri usichoke hata watu wawili au watatu wakielewe umelisaidia taifa
J.k alijitahidi kufata values za kidemocrasia uhuru wa habari uhuru wa kujieleza mpaka akaruhusu mjadala wa katiba,uliona jinni Maufisadi yalivyokuwa yanaibuliwa,uliona mawazili na watumishi wanavyo wajibishwa.rushwa, uwizi,uuwaji una shamiri gizani.tutaendeleaje tukiwa gizani tutapataje haki ikiwa mahakama zinatiwa mfukoni,tutapataje viongozi tunao wataka wakati tumenyimwa uhuru wa kuchagua
 
Naomba unijibu hili;

Kwanini mwaka 1960-1980 ambapo kulikuwa na udikteta Korea ndio kulikuwa na Maendeleo makubwa—infact ndio Korea ya leo kiuchumi ilijengwa hapo—kuliko miaka hiyo ya 1940 unayoisema kuwa ilikuwa na Demokrasia?
 
Korea ipi unazungumzia hapa!? 😳😳😳 South Korea hujawahi kuwa na dikteta tangu 1948.

Naomba unijibu hili;

Kwanini mwaka 1960-1980 ambapo kulikuwa na udikteta Korea ndio kulikuwa na Maendeleo makubwa—infact ndio Korea ya leo kiuchumi ilijengwa hapo—kuliko miaka hiyo ya 1940 unayoisema kuwa ilikuwa na Demokrasia?
 
Swala la udicteta we mwenzetu umelitolea wapi? Mleta mada kaongelea democracy.

Pia kwenye kutenda mambo maovu demokrasia ndio kinara, kinacho fanya watu wasitambue hilo ni wanatekeleza maovu kwa weledi mkubwa (wanahadaa uma),
Mfano; USA.

Ila kwenye udicteta mambo hadharani hakuna unafiki.
 
Korea ipi unazungumzia hapa!? [emoji15][emoji15][emoji15] South Korea hujawahi kuwa na dikteta tangu 1948.
Genral Park alikuwa nani kama sio Dikteta? Huyu alikuwa na utawala wa kiimla wa kijeshi. Uliitwa puguk kangbyon—rich nation, strong army.
 
Naomba unijibu hili;

Kwanini mwaka 1960-1980 ambapo kulikuwa na udikteta Korea ndio kulikuwa na Maendeleo makubwa—infact ndio Korea ya leo kiuchumi ilijengwa hapo—kuliko miaka hiyo ya 1940 unayoisema kuwa ilikuwa na Demokrasia?
Kipindi hicho hata Afrika, karibu yote, ilikuwa na mfumo wa chama kimoja tu. Mbona hali zetu kiuchumi ni hoi. Kulikoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…