MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kenya kwa msosi ni hovyo kabisa...japo naikubali Nairobi kuliko jiji lolote EA.
MK254
Kila mtu ana kile alichokiezoea kulingana na makuzi yake na asili ya watu wake, hii mipaka ya mzungu sijui kwanini huwavuruga Watanzania, unapaswa ufahamu hamna chakula cha nchi ila kila jamii au kabila lina aina yake ya misosi.
Kwa mfano Wasukuma wa Tanzania wanapenda ugali, na ndivyo ilivyo kwa Waluhya wa Kenya, ukienda kwa Wapare wanapenda makande, na ndivyo ilivyo kwa Wakikukuyu wa Kenya.
Ukishuka kwenda Pwani za nchi zote mbili unakuta huko ni mwendo wa biriani, hivyo ni vigumu kusema chakla fulani ni cha Wakenya au Watanzania maana hii ni mipaka ya mzungu iliyokuta jamii za watu wanaishi kwa tamaduni zao.